Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi,TAAMULI HURU: 4R zitumike kuponya makovu ya Mapinduzi ya Zanzibar
Jumapili ya Tarehe 12 January 2025, imedondokea siku ile ile ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyotokea Jumapili ya Januari 12, 1964. Tanzania imeadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakati Wazanzibari wengi wanashereheka kuyapongeza Mapinduzi hayo (na wengine hadi kuyapa utukufu kwa kuyaita Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambalo teno Utukufu, kwa dini mbili kuu, Wakristu na Waislamu, Utukufu ni KWAKE YEYE tuu na utukufu ni WAKE YEYE tuu, Mwenyeenzi Mungu mwenyewe, hivyo kuita kitu kingine chochote kitukufu ni kama kufuru!), kuna Wazanzibari wengine, japo wachache, siku hii ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwao ni siku ya kumbukumbu chungu na mbaya, kwa kutonesha makovu ya mapinduzi hayo, kwa kuwapoteza wapendwa wao, kutokana na umwagwaji damu wa Mapinduzi hayo na baada ya Mapinduzi.
Japo hakuna ubishi kabisa, kuwa Mapinduzi ya Zanzibar, yameleta neema na kheri Zanzibar, lakini pia ni ukweli mchungu kuwa mapinduzi hayo yalimwaga damu za watu, na pia yalisababisha maumivu makubwa kwa waliopinduliwa ambao wanaishi na makovu ya Mapinduzi hadi leo, hivyo makala ya leo ni kutoa wito, kuzitumia 4R za Rais Samia, kutibu makovu ya Mapinduzi hayo, na keleta siasa za utengemano Zanzibar.
Kule kwenye mtandao maarufu kuliko mitandao yote ya kijamii nchini Tanzania, Jamii Forums, shamra shamra za kuisubiria siku hii ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilianza siku nyingi kabla kwa kushamirishwa na Fake News kuwa Sultan mpinduliwa angerejea Zanzibar kwa ziara rasmi na angehudhuria maadhimisho ya mwaka huu.
Hilo la Sultani kurejea mimi nikalidaka na kuchangia kwa kulitolea mapendekezo yangu kumi kwa SMZ.
Ndipo kaka yangu mmoja, kutoka Zanzibar, naomba kumtaja kwa jina moja tuu Kaka Chalz, ni kaka yangu alinipokea RTD, ile mwaka 2000, akatufundisha kazi ya utangazaji, hivyo tunawaheshimu sana kaka zetu hawa, na hata tunapokosea, hawaachi kutupigia simu kuendelea kutuongoza mpaka leo mpaka kesho, Asante Kaka Chale!.
Basi Kaka Chale akaniuliza una uhakika na chanzo chako cha habari kuwa hii ni habari ya kweli?, nikamjibu kwa vile imetangwa na Jamiiforums, kwa jina maarufu JF, ni chombo cha kuaminika, ingekuwa fake, JF inatumia mfumo wa Jamii Check kubaini fake news na kuzifuta, hivyo itakuwa kweli.
Ndipo nikaipitia ile habari kwa mara ya pili kuisoma source, nikakuta ni mtu kutoka Oman!, nikamtafuta kaka yangu mwingine Zanzibar huyu ni Mzee Salim Said Salim, mwandishi wa siku nyingi, tunamuita jina la Mzee SSS, yeye ana nasaba kidogo na ukoo wa Sultan, Salim akawapandia kwa simu, Oman, familia ya Sultan wakakanusha kuwa hiyo habari ni fake news!. Asante Mzee SSS!.
Ndipo nikawasiliana na Mkuu wa JamiiForums, Maxence Mello, kumweleza hiyo habari ya Sultani kurejea ni fake news. Nikamrudia Kaka Chale, nikamshukuru kwa angalizo lake, ila nikamwambia baadhi ya yale mapendekezo yangu 10 kwa SMZ, mengine bado ni muhimu kwa Zanzibar ya sasa, yafanyiwe kazi!.
Baada ya lile jibu la Familia ya Sultani kule Oman kukanusha ile fake news, Sultani alishinda siku moja tuu, na kesho yake akaitwa kwa Mola wake, akatwaliwa!. Nikamshauri Kaka Chale, SMZ iseme kitu!, haikusema!. Ukimya huo wa hata kupeana pole za msiba, ukanikumbusha bado Zanzibar kuna fukuto za Mapinduzi.
Huu ni mwaka wa uchaguzi, na hakuna ubishi siasa za Zanzibar, licha ya uwepo wa SUK, bado zinaathiriwa na mzimu wa machozi, jasho na damu, zilizomwagika wakati wa mapinduzi na kuna watu bado wana makovu ya mapinduzi yale ambapo 4R za Rais Samia, zikitumiwa kikamilifu zinaweza kuyatibu!.
Hivyo matokeo ya baadhi ya chaguzi za Zanzibar, ni matokeo yale yale ya ule uchaguzi wa mwaka 1963. Mfano mzuri ni uchaguzi wa mwaka 2015, kuna msemo wa Kiingereza unaosema numba haziongopi!.
Matokeo ya NEC ya uchaguzi wa 2015 kwa Zanzibar, yamethibitisha pasi shaka kuwa uchaguzi wa Zanzibar wa 2015, kama usinge futwa, Maalim Seif Shariff Hamad wa Chama cha Wananchi CUF ndie angelikuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Zanzibar kwa kutumia kigezo cha matokeo ya uchaguzi wa urais wa JMT, uliosimamiwa na NEC kule Zanzibar ambao uchaguzi haukuwa na dosari, katika uchaguzi huo, mgombea wa UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa, alimshinda mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli.
MGOMBEA KURA HALALI ASILIMIA
DR. JOHN POMBE MAGUFULI 194,317 46.5%
EDWARD NGOYAYE LOWASSA 211,033 50.50%
IDADI YA KURA HALALI 417,882
Hii maana yake Zanzibar upinzani unaweza kushinda, sasa kwa vile bado kuna hostilities za machungu ya Mapinduzi, siku upinzania ukishinda Zanzibar, kutaibuka kulipiza kisasi!.
Nilishauri
Zanzibar iitumie R ya Reconciliation, ianzishe truth and reconciliation commission watu waruhusiwe kutoa machungu yao ya mapinduzi, kwa kiingereza ku vent ili kuponya maumivu, (to heal) na machungu ya mapinduzi.
Neno Matukufu kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar lisiendelee kutumika yaitwe tuu Mapinduzi ya Zanzibar na vibwagizo Mapinduzi Daima na Tutayalinda kwa gharama yoyote tuachane nayo ili kuponya wapinduliwa.
Falsafa hii ya 4R za Samia itumike hadi Zanzibar mshindi wa kweli wa uchaguzi wa Zanzibar atangazwe mfano mzuri ni
Hivyo nawashauri Rais Samia, na rais Dr. Mwinyi, kubalini kutibu makovu ya Mapinduzi, ili kuzimaliza siasa za hostilities, ikitokea upinzani umeshinda Zanzibar, hakuna haja kufunika kombe mwanaharamu apite, iwe ni kupokezana kwa amani na upendo.
Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Rejea

- Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tuyaenzi kwa 4R za Rais Samia?, JMT Tuitendee Haki Zanzibar?, Tuwatendee Haki Wazanzibari? Mshindi Halali Apewe?
- Je Zanzibar Inahitaji Truth & Reconciliation Comm。Kuponya Makovu ya Mapinduzi, ili Upinzani Ukishinda,Upewe?。Sis & Bro,Can You Please Do The Needfu?。
- Kama 4R za Samia,Zimeweza Kutanzua Mtanziko Siasa za Bara,Kwanini Zisitumike ZnZ, Kutibu Makovu ya Mapinduzi,Uchaguzi wa 2025,Mshindi Halali Apewe?