Kama 75000 inamtosha mwanafunzi kwa siku moja

Underdog

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2014
Posts
343
Reaction score
444
Kama 7500 inamtosha mwanafunzi wa chuo kwa matumizi ya siku moja, kwa nini wabunge nao wasijengewe hostel wakae humo halafu wawe wanalipa 500 kwa siku kama wanafunzi wa vyuo, halafu badala wawe wanapewa zile laki mbili kwa kikao kimoja basi wapewe 7500 kwa siku huku wakisubiria mishahara yao. Naombeni maoni yenu wadau
 
Underdog, utakua unaongelea wabunge wa nchi nyingine lakini si Tanzania ninayoifahamu mimi.
 
Last edited by a moderator:
Pole Mkuu, naona umewaza mbali saana. Ukipata nafasi ya kuwa Mbunge, uyatoe maoni hayo kama yalivyo.
 
Rekebisha kwanza kichwa cha habari chako. Halafu, soma kitabu cha Kusadikika cha Hayati Shaaban Robert
 
Underdog, utakua unaongelea wabunge wa nchi nyingine lakini si Tanzania ninayoifahamu mimi.
najua wabunge watagoma na inawezekana hata badala ya ukawa kikaanzishwa kikundi kingine cha kupigania posho(sijui watakiitaje), ila gap la wenye nazo na wasiokua nazo limekuwa kubwa mkuu
 
Last edited by a moderator:
Pole Mkuu, naona umewaza mbali saana. Ukipata nafasi ya kuwa Mbunge, uyatoe maoni hayo kama yalivyo.
mbona umechangia kama vile mtoto wa mbunge au ndo vile tena mkuu wangu
 
mbona umechangia kama vile mtoto wa mbunge au ndo vile tena mkuu wangu

Hapana,siko kamaunavyodhani,ila nahisi umeumizwa sana na hali unayopitia na nimefurahishwa na jinsi ulivyowaza.Najua miaka michache ijayo unaweza kuwana bahati ya kupata dhamana kubwa; naomba uwakumbuke wana Vyuo na wanyongewengine wa nchi hii.
 
najua wabunge watagoma na inawezekana hata badala ya ukawa kikaanzishwa kikundi kingine cha kupigania posho(sijui watakiitaje), ila gap la wenye nazo na wasiokua nazo limekuwa kubwa mkuu

Hilo gap litaendelea kuwepo milele na milele hasa kwa nchi yetu.
 
Pole sana mkuu,hivi kesho mmesema ndio mgomo hapo UDSM??Pigeni shule Underdog ili baadaye uwe raisi wa nchi hii potelea mbali iwe Tanganyika,Zanzibar au Tanzania alafu kwa mamlaka utakayokuwa nayo utangaze posho kwa wabunge na wafanyakazi wote wa serikali ikiwemo wewe itakuwa sh 7500!
 
Last edited by a moderator:
Yan Mbunge Vs Mwanafunzi Mmh?
Hata Hamuoni Tofauti Iliopo Apo Jamani
Kumbuka Mchumia Juani Hulia Kivulini
Yataisha Hayo Mmyasemayo Tena Si Bada Ya Miaka Mitatu Au Mitano Si Una Maliza Chuo Icho Ndo Unaenda Kwingne Kwanin Uwe Unasoma Alafu Utamani Waku Wako Wapate Kama Una Chopewa Akati Unajua Kabisa We Upo Chini Yao Kwanin Iwe Ivo
Mbali Mbali Ni Ngumu Sana Ku Mfananisha Kwani Kua Chuo Nini Bwana Mbona Mnatoka Chuo Na Kuanza Kusugua Benchi Miaka Chungu Mzma Kama Unajiona Muhmu Sana Kama Mbunge
Mwanafunz Soma Sana Hela Zipo Tu Tama Yanini?
 
umeongea ukweli tatizo ni kwamba wanafunzi wenzako hawana akili kama yako. By the way poleni sn kwa matatizo mnayopitia.
 
naungana na wanafunzi. iongezwe japo 15 au 20 elfu kwa siku. kwani hawa wabunge wanafanya nini la ziada dodoma.
 

hiyo 7500inatosha tu wiki za mwisho unachukua slesi&maji ya kudownload, tena mkipewa nyingi hamsomi mda wote mpo mango garden,dar live,maisha club nk.
 
Ndg yangu suma mziwanda kageye mimi nilimaliza chuu kitambo sana. nionavyo mimi haitoshi. mambo ya madeni badae, deni haliui na wala usiliogope. tz deni la taifa ni karibia trillioni 30, wote tulioanza vyuo 1994 tunadaiwa., binafsi sijaona anayenidai walaa anayeniulizia. mbona kama watu binafsi tunq mikopo kwenye mabenki in terms of millions hatujafa na tunalipa taratibu?
7500/= haitoshi hata kidogo kwa maisha ya sasa. kwa nini per diem ya mtu anayesafiri kikazi mfano toka da mbeyaa kuja da isiwe 7500/=? au wabunge dodoma wasipewe hiyohiyo nawenyewe wakalale hostel? ndg yangu wake up.
 

hyo pesa ukitumia kwa matumizi elekezi inatosha ila ukiingiza na matumizi mengine ndo haitoshi,mbona mimi inanitosha nakula milo mi3,naul,maji nanunua
 
kwa mtu yeyote aliyewah kusoma chuo kikuu na mwenye akil timamu anajua kama haitoshi.kupenda elim bila kupenda walim na wanafunzi ni kiin macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…