Kama amedhamiria kweli kuondoka mwache aende.

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Kama amedhamiria kweli kuondoka mwache aende. Wapo watu wengine kuondoka kwao ndio mwanzo wa maisha mengine mazuri zaidi nje ya huyo mtu aliyeondoka au uliyemuondoa

Maana matokeo ya upendo wa kuhurumiwa kwasababu ulimng'ang'ania basi utakufanya kuwa mtumwa na utakuwa umechagua maisha kunyenyekea, kunyanyasika na kutumikishwa

Mapenzi hayataki utumwa wa kulazimishana. Mapenzi ni hisia kama hana hisia na wewe tena basi huna thamani kwake tena (huhitajiki)

Siku ukielewa kwamba, si kila mtu ameumbwa kwa ajili yako na wapo watu pia WAPITAJI tu kwenye maisha yetu. Ndipo rafiki, utaacha kulazimisha upendo mahala ulipofika kikomo.

Kumwacha aende nao ni upendo mkubwa mno kuliko kumng'ng'ania mtu aliyeamua kuondoka atakupiga matukio na mwisho utamwachilia tu ila utakuwa uko hoi kwa manyanyaso mazito.
 
Attachments

  • 1731698541102.jpg
    1731698541102.jpg
    210.3 KB · Views: 5

So what?
 
umeachana huko unataka nasisi tuachane never we pambana na kasongo wako
 
Back
Top Bottom