Kama AMRI 10 na sio Sheria za Musa tu ziliishia Msalabani; nini Maana ya DHAMBI kwa dunia?

amri ya upendo sio amri mpya bali sheria ya mungu imeBASE humo
 
Facts:

Yesu hakufuta sheria alitoa tafsiri sahihi tu.

Pia Yesu ndiye mbadala wa sanduku LA agano.
 
dhambi hii dhambi hii itaisha lini mungu wangu siku hizi adi wanakolomije wana foji vyeti#dhambi -ina maana kwenda kinyume na makubaliano au agano la eneo fulani au jamii fulani mf:unatakiwa uwe na vyeti halali ukifoji vyeti fake ni dhambi coz jamii yetu hairusu ishu hyo NOTE:siyo kila dhambi ni dhambi
 
Yesu ndio Sanduku la agano. Weka nyama hapa mkuu umeandika kitu mtambuka
Wakati wa agano la Kale, Sanduku la agano lilikua linakaa mahali patakatifu pa patakatifu.
Mahali hapa alifika Kuhani mtakatifu tu. Na alikua anafungwa mnyororo ili akikawia kutokana, watajua kua Mungu atakua amempiga na radi ( yaani ) amekufa, wanachofanya wanamvuta kumtoa kwa mnyororo waliomfunga nao mguuni. Manake hakuna atakayethubutu kuingia.

Mahali hapa liliwekwa sanduku la agano. Walilokua wakitembea nalo kila waendapo, kama ishara.

Wakati wa agano jipya:-
Yesu ndiye anayefananishwa na kuhani mkuu anayesimama pale mahali patakatifu pa patakatifu Kumtolea Bwana dhabihu.

Wakati Kristo alipokufa msalabani na lile pazia la hekalu lilipasuka katikati na kufanya watu wote kuona mle ndani jinsi kulivyo.

Ilikua ishara kua kila MTU anaruhusiwa kuingia.

Now, Ufalme wa Mungu Ni kwa kila individuals.

Agano la mwanzo lilifanywa na Moses kuwatoa wana waisrael kule utumwani Misri.

Now Agano la pili ni la damu ya msalaba. Alilolifanya Yesu Kristo.
Ni kupitia agano hili unaishi nalo (i.e. Sio tena kwenda nalo) kila mahali.

Nitaandaa maandiko kuweka sawa.
 
Nimeelewa kiasi mkuu, vipi kuhusu hawa makuhani waliopo duniani ambao watu tunakwenda kuwatubia au wakituwakilisha kwa Mungu linganisha na maelezo yako hapo juu
 
Nimepewa kiasi mkuu, vipi kuhusu hawa makuhani waliopo duniani ambao watu tunakwenda kuwatubia au wakituwakilisha kwa Mungu linganisha na maelezo yako hapo juu
Iko hivi..
Yesu alikua ana karama zote za Unabii, utume, ualimu, uchungaji, uinjilisti, utume.
Akazigawa kwa wanafunzi wake kwa kadri ya Roho wake alivyowajaalia. Kupitia hawa Injili(Habari Njema ya Ufalme wa Mungu) inahubiriwa ulimwenguni kote.

1 Corinthians 12:27-28
[27]. Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. [28]. Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.....


Ephesians 4:5-6,8,10-12
[5], Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. [6] Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.


[8]. Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.
[10] Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote. [11]Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; [12] kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

Kuhusu Ukuhani wa Yesu.

Hebrews 4:15
[15] Kwa kuwa hamna KUHANI MKUU asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.


Hebrews 8:1-2,11
[1]Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, [2]. mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu........


.....[11]Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa MAANA WOTE WATANIJUA, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.


...Just a nutshell..
 
Warumi 10:1-4
[1]Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
[2]Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
[3]Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.
[4]Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
 
Hatujajua dhumuni lako kwa kuandia hayo. Embu tuambie dini yoko ili tuwezekuku jubu vizur, tuanzie hapo
Unataka kuleta udini! Sikosei wewe muislamu? Unatakiwa kuongelea hoja iliyopo hapa siyo dini ya mtu. Na siku zote kaa katika hoja siyo nje ya hoja kama unajadili jambo au utajichanganya. Tatizo mmefundishwa kukariri na ubishi, siyo ku reason with facts and evidence. Pole sana naona Madras imekuharibu.
 
Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
mkuu shusha nondo hapo, maana inaonekana kuna kitu cha kujifunza.
ninavyoelewa ukiwa wa kristo huvunji sheria,
Yaani ukiwa mtoto wa jaji au mwanasheria hatutegemei uwe champion wa kuvunja sheria bali tunategemea utakuwa huru maisha yako yote maana unajua zaidi ya wengine maana unaishi na mwenye sheria.
Ukimwamini Utamtii.

Hebu weka sawa hapa mkuu...
 
imani ipi hiyo mkuu au ni yako binafsi uliyojiwekea kama independent and free being
atakuwa ni msabato ndo wanaokomaa na amri hizi kumi na zaidi wanaikazia sabato na huku wanazini.
hakuna aliye salama maana dunia yote imkosa na mtu asije akajisifu kuwa ni kwa kufuata hizo sheria ila huruma ya mnyaazi Mungu Jehovah
 
Kuna kitu unataka watu wafikie wakione lakin umekiacha katika Fikra zako

Nashindwa kuchangia sababu sijajua yan nachangia nini au sijaelewa umemaanisha nini kwa huu uelewa wangu mdogo
 
kilichotokea pale msalabani ni sadaka au malipizi ya dhambi zote. ukifanya dhambi badala ya wewe kutoa sadaka ya dhambi unatumia damu ya yesu kuiondoa dhambi yako, ndivyo ninavyoelewa mimi, japo nami ninamengi ya kuuliza.

Sadaka ya damu ya mtu si ya kichawi na kishetani hiyo?
 
Safiiii kabisa safi saana.barikiwa mkuu.

ROHO MTAKATIFU tunakushukuru maana ww ni mwema sana.Endelea kutufundisha maana tunahitaji tujue zaid.Si kwa akili,damu wala nyama tumeyatambua haya ila ni neema yako inayo tufanya tujue haya na uweza utokao juu.

~Tunajifunza kwako BWANA YESU.

~KWELI ANAKUJA YESU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…