Ukishakuwa mtoto hutendi dhambi bali unafanya makosa, pia ukiweza kufuata amri hizzi kuu mbili tayari umetimiza zote zilizobakia kwa maana ni sehemu ya hizi kuu mbili za upendo kwa Mungu na kwa jirani.
Dhambi ni Uasi wa sheria za Mungu.
Amri kumi Zinaonyesha Upendo kwa Mungu na Kwa mwanadamu. Yesu hakutoa sheria mpya.
Sheria haikoi, ila inakuonyesha makosa, na kukuelekeza kwa Yesu ili Utakasike ufae kwa Ufalme wa Mungu.
Kila mwanadamu anayevunja sheria anatenda dhambi bila kujali ni mtoto wa Yesu au wa dunia.
"Hapo ndipo penye subira ya WATAKATIFU, Hao wazishikao amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu" Ufunuo 14:24
Yesu Ni mwokozi wako kwa sababu KAKUOKOA, Kutoka Dhambini na atakuchukua siku ya mwisho (Glorification)
Yesu ni Bwana wako, pale unapotii maagizo Yake na sheria zake. Hakuna mwana anayesema anampenda Baba yake huku anavunja maagizo Yake.
Katika hilo bibilia Iko wazi. Hakuhitaji ufafanuzi.
Mwamini Yesu, Tii maangizo yake zikiwemo amri kumi ambazo ndani yake Imo sabato Ya SIKU ya Saba.
Upendo bila utii, ni ukaidi na maigizo.
Mungu akubariki mtakatifu wa Bwana,