Nimekuwa nikimsikiliza sana Gambo kwa mengi anayosema. Ukweli nimetokea kuwa mtu ambaye namfurahia sana, kwa kuwa amekuwa mtu anaetoa kauli makini zenye kujenga bila hofu katika kuielekeza na hata kuikosoa serikali ambayo inaongozwa na chama chake.
Mtazamo niliokuwa nao juu ya Gambo akiwa RC Arusha na nilionao juu yake leo hii ni tofauti sana. Ameni-impress sana, hata nahofia CCM huenda muda wowote wakampa uwaziri ili kujaribu kumnyamazisha, kama ilivyo kawaida yao. Weka siasa pembeni, Gambo ni mtu anaongea vitu very constructive Bungeni. Sikumtegemea hilo kabisa.
Pamoja na kauli nzuri, zenye mantiki anazotoa Gambo, bado nakumbuka mitafaruku na kwa kiasi fulani unyanyasaji aliofanya kwa Chadema akiwa RC Arusha. Hata kama hakufanya hayo maovu yeye, alikuwa na na jukumu la kuwalinda watu wa Arusha kama RC pale. Nimemuelewa sana, kwamba alikuwa katika mazingira magumu na ilibidi tu afanye aliyofanya, au asifanye aliyotakiwa kufanya kama RC. Wengi wanasema kwa nini hakujiuzuru, lakini ni wazi kwamba angefanya hivyo ingekuwa kutangaza vita hadharani dhidi ya raisi wa wakati huo, kwa hiyo isngekuwa vema kwake kujiuzuru.
Hata hivyo, namshauri Gambo, kama kweli anayosema leo yanatoka moyoni, basi awaombe radhi Chadema hadharani, hata ndani ya vikao vya Bunge. Na wapo wengi walikuwa katika mazingira ya Gambo, nao wanaweza kufanya hivyo.
Kuomba radhi ni uungwana, na tunajua ni kweli awamu iliyopita ilifanya unyanyasaji wa juu dhidi ya Chadema kama Chama na viongozi wake mmoja mmoja. Basi Gambo fungua njia, omba radhi yaishe, na itakufanya uzidi kuwa na watu wengi wanaofurahia sana pointi zako za makini ukiwa Bungeni.