Kama bado maisha magumu Dar hama nenda haya

Kama bado maisha magumu Dar hama nenda haya

Hii ni kweli mkuu! Haswa mbeya iko vzr sana na uchawi, moro sijawah kukaa

Ila mwanza iko juu zaidi..


Kama unanguvu pambana na dar utatoboa pia
kutoboa ni ngumu sana hiyo mikoa kuna vita za nguvu za giza sana sishauri mtu kwenda kuanza maisha kule kama hupendelei vurugu za hivyo itamchukua miaka mingi kukaa sawa labda nawe uwe mpenda shirki ili uende nao sawa.
 
uzi mzuri but nimeshakaa mikoa yote uliyoitaja afadhali kukomaa dar esalam, ukishindwa nenda morogoro au mwanza hiyo mikoa uliyoitaja inasumbuliwa sana na 1. UCHAWI 2. UBINAFSI 3. MZUNGUKO MDOGO WA FEDHA. ukienda jipange kisaikolojia.
Point.
Ila nilivyoizoea Dar sidhani kama nitaweza ku migrate.
Labda kama ningezaliwa hiyo mikoa ya big 4.
Ila sikatai kule Kuna fursa sana sana. Uende ukiwa miaka under 45. Kama ni zaidi unapotea ukitokea Dar
 
Hii ni kweli mkuu! Haswa mbeya iko vzr sana na uchawi, moro sijawah kukaa

Ila mwanza iko juu zaidi..


Kama unanguvu pambana na dar utatoboa pia
ukiona MKOA una dominance ya kabila Moja au mawili usiende ushirikina nje nje hasa hizi biashara za maduka.

Morogoro, DODOMA, Arusha, Dar es salaam

At least huko mchanganyiko ni mkubwa kwa Moro na DODOMA nazungmzika Moro town na DODOMA city huko bush ni mwendo wa kupuliza tu.

There is no success like dar success.
 
Ukitaka kukimbia Dar ni uende nje ya nchi. Nchi yote hii kutoka ni ngumu sana.
 
Kwa kusini ni sehemu nzuri kama huna kitu kbsa cha kuanzia lkn kama unakitu tayar nenda kanda ya ziwa ila bukoba chato usiende kbsa

Kanda ya ziwa popote unaweza kuanza,kuhusu chato bkb nadhani ibaki kuwa mitazamo binafsi.

Ila kama una lengo la kumiliki ardhi ya kuyossha nenda mikoa ya kusini.
 
Sio rahisi Mtu kutoka dsm hasa sisi vijana maana dar ndo Sehemu pekee unaweza pata pesa ya chap chap ukizingatia na Maisha ya dar. Matajiri wengi wapo huku .

Kama una fani
Kipaji
Elimu basi usicheze mbali na hili jiji la kitajiri.
 
Jiji lina vijana wengi sana ambao kwa namna moja ama nyingine wamekulia ama kuzaliwa kabisa katika jiji la Dar es salaam na wengi wao wameishi maisha ya hadhi hapo miaka ya 90s-00s, wakazi wengi wamezaliwa sinza -kinondoni na baadaye kuamia Tabata na maeneo mengine

Wengi wao kwa sasa ni watu wazima kabisa yaani ni 20s plus na raman ya maisha ni haisomeki kabisa kwa upande wao, mbaya zaidi wapo wenye elimu ya TIA , UDSm na vyuo vingine vingi vya mjini, lakin kiukweli maisha yao ya kesho hayapo kwenye mboni za macho yao

Nimefanya utafiti mdogo pia kwa wakazi wenye maendeleo makubwa kwenye jiji la dar es salaam zaidi ya asilimia 90 bila kupepesa macho ni wageni tena wale wageni waliokuja ukubwani wakitokea mikoa kama kilimanjaro, mbeya , njombe, mwanza na mengineyo, kama unataka kuamini hilo nenda kariakoo kwenye maduka makubwa utagundua baada ya uchunguzi ya kwamba wamiliki wengi wa hayo maduka ndio wamiliki wa real estate kubwa kwa dar es salaam na pia hao hao ndio wamiliki wa majengo zaidi ya asilimia 95 ukitoa ya serikali

Kwa kijana kama ramani hazisomi kabisa na hauna kitu kabisa nenda mikoni na moja ya mkoa ambao na shauri ni pamoja na upande wa nyanda za juu kusini jumuisha kuanzia Iringa, Njombe, Songea, mbeya, songwe, sumbawanga, katavi ni moja ya mikoa ambayo mambo mengi wapo nyuma yaani namaanisha fursa nyingi ni mbichi haswa

Ukifika kwenye moja ya mikoa hiyo jifunze tamaduni zao na namna gani wanaishi na kuwa humble sana usionyeshe wewe ni watofauti ni watu wanaopenda vya kwao na wanapenda kuwapa fursa wakwao lakini wengi wao bado hawana macho yakuona fursa sasa kwa wewe mwenye elimu yako na umeishi kwenye jiji kubwa kama dar basi nirahis kuziona fursa na kuzifanyia kazi

Nimependekeza kwa kuanzia upande wa nyanda za juu kusini mwa nchi yetu kutokana na gharama nafuu pia za maisha kuwa ni chini zaidi ya maeneo yote ya Tanzania kwa hiyo chochote unachozalisha ni rahis zaidi kukutunza bila kukitumia

Jambo jingine kwa mtafutaji usitumie sana muda mwengi kuishi kwenye maeneo hayo unapopata faida ya kujitosheleza basi sogea mbele kwenye miji iliyochangamka kama Mwanza, shinyanga-Kahama, geita huko utapata changamoto zaidi ya biashara lakin utakuwa haraka tena mara mbili au zaidi ya ulichotoka nacho nyanda za juu kusini,

Ukifata mlolongo huo kwa miaka 5 hadi 10 ukajitosheleza rudi tena dar es salaam ukiwa na mtaji wa kutosha pamoja na uzoefu wa kutosha kwenye kazi zako haswa kwa mfanya biashara itamsaidia zaidi

WASHINDAO NI WALE WANAOJARIBU NA KUANGUKA LAKINI HAWAKATI TAMAA🫶
Mkoani labda upate kazi au uamue kwenda kufanya kilimo ila kwa hustle za mtaani tu bora ukomae dar. Mkoani mzunguko wa hela ni mdogo sana
 
Back
Top Bottom