Tufike mahali tuwe tayari hata kumfunga paka kengele.
Tanzania ni nchi nzuri sana yenye kila kitu watu, madini, ardhi, mafuta, gesi, mito, maziwa hadi bahari.
Mvua za uhakika na urithi mkubwa wote bure toka kwa Mola. Iweje tufikie kufarakana kwa sababu za kisiasa?
Kwamba ni CCM, Chadema, ACT, NCCR au CUF? Aah wapi! Mbona kote ni manung'uniko tu? Ni Pole pole, Vicky Kamata au Bashiru?
Watoto mezani hawaachi kushtakiana mbele za mama zao. Huyu kanifanya hiki, huyu kanifanya vile. Mambo ya kawaida.
"Wajibu wa mama mwema ni kuwaweka wanawe pamoja na maisha ya furaha yakaendelea." -- Askofu Bagonza.
"Yupo mbaya wetu mahala anaye tugombanisha. Siku tukimpata zitakuwa ama zetu ama zake." -- Jabali la Muziki.
Kwenye angle pale anaonekana mtu mwingine nyuma ya usukani. Pole pole anamwita "parallel power." Hao wanalazimisha rais kuwajibika kwao.
Wana ujasiri wa kudai, rais ni taasisi. Taasisi hii imetajwa wapi katika katiba? Ina kampeni vipi? Wajumbe wake wanapatikana je? Wajumbe wao leo ni kina nani? Au ndiyo hawa wasiojulikana, tukapate kujua waliko kina Moses Lijenje?
Inasemekana wajumbe wake hao wako kila mahali na katika kila idara wanayoiita nyeti. Si mahakamani, polisi hadi JF. Kina Sabaya ni baadhi yao. Wameigeuza nchi kuwa yenye huzuni na vilio badala ya kuwa yenye furaha na bashasha.
Hawa ndiyo wenye kukaanga mbuyu na kutuachia wenye meno kutafuna.
Hawa si wa kuwaacha. Hawa ndiyo walio wabaya wetu. Katiba mpya ndiyo dawa yao.
Maudhui ya uzi huu kwa sehemu kubwa yangali yanaishi:
Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa