Uchaguzi 2020 Kama CCM waliiba uchaguzi wa 2020, kwanini mnajipendekeza kwake?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Sijui ni kutokujielewa…sijui ni ujinga…sijui ni kutokujua unataka nini…sijui ni kutokujua kuwa hujui…sijui ni nini hasa!

Manake sielewi. Kama CCM waliiba uchaguzi wa 2020. Uchaguzi uliowapa ushindi John Pombe Magufuli na Samia Suluhu Hassan ushindi mkubwa sana, iweje leo Rais Samia apendwe sana na watu waliokuwa mstari wa mbele kudai kuwa chama chake kimeiba uchaguzi.

Au labda tatizo ni ‘low expectations’ walizonazo hao watu wanaompenda sana Samia sasa hivi?

Kwamba haiba ya upole na sauti ya upole na jinsia ya Rais Samia ni tosha kuwafanya wale walioichukia timu yake ya wakati sasa wabadili gia zao za mawazo angani na kuanza kuunga mkono juhudi za Rais Samia?

NB: Kuna baadhi ya majibu toka kwa watu fulani fulani hivi tayari nimeshajua yatavyokuwa.

Nawasubiri tu.
 
Nani anajipendekeza kwake ?

Tutamnyoa kwa wembe ule ule

Huyu bibi naye kaingizwa king eti wanatengeneza chanjo utoto mtupu

Nchi haina uwezo wa kutengeneza hata sitiki za meno halafu itengeneze chanjo ya corona!!

Huyu bibi amezengukwa na makundi ya wapigaji wahuni wanataka kumpiga na yeye anachekea tu wezi!!

Hakuna mtu anambembeleza huyu watu walitaka muafaka wa kitaifa ili nchi watu waishi kwa amani tu ili mambo yarekebishwe!!

Sasa kagoma ngoja tumnyooshe kama tulivyomnyoosha Magufuli akifika 2025 viatu vizito atakimbia mwenyewe IKULU nyumbani wacha tu wamdanganye wapambe fake!
 
Kwani alieiba kura ni Samia au Mwendazake? Katiba ya JMT inasema katika kutekeleza wajibu wake rais wa JMT halazimishwi kufuata ushauri wa mtu yeyote yue, sasa kumu attach Samia na uharamia wa yule jamaa ni kumuonea tu...
 
You are caping hard for her 🤣🤣.
 
Mara nyingi wanasiasa wa Tanzania wanacheza mdundo wa maslahi kulingana mapigo ya mpiga ngoma......
 
Nguvu ya Chama cha Siasa, na chama chochote, ni wanachama siyo viongozi. Nitatoa mifano kuthibitisha hoja yangu.

Uchaguzi wa 2015, CHADEMA ilitegemea nguvu ya Lowassa na kundi la wanasiasa aliohama nao kutoka CCM. Walifanikiwa kupata idadi kubwa ya madiwani na wabunge hadi kuongoza baadhi ya Halmashauri. Kwa kuwa walitegemea nguvu ya viongozi hawakuweza kuaminiwa kuunda Serikali.

Uchaguzi wa 2020, CHADEMA pia ilitegemea nguvu ya Lissu, wakiamini kushambuliwa kwake ungekuwa mtaji wao wa kisiasa. Badala yake chama kiliambulia Mbunge mmoja tu.

Mifano hiyo miwili inadhihirisha kuwa bado viongozi wa CHADEMA hawajaona umuhimu wa kutumia nguvu ya wanachama. Wanachofanya ni kuwatumia wanachama kufanikisha malengo yao binafsi ya kisiasa. Kumpamba Rais, mama Samia, lengo lao kuu wanalijuwa viongozi na si wanachama. Hata dai lao la Katiba, lengo ni la viongozi kuingia mdarakani.

Umefika wakati kwa viongozi wa CHADEMA kuishi kwenye kaulimbiu yao ya "PEOPLES POWER" na si vinginevyo.

Eda ni ada yenye faida, wahenga walinena.
 
Wapinzani wa Tanzania ni hovyo kabisa, bora upinzani wa nchi kama Malawi au Zimbabwe.
 
Sijui ni kutokujielewa…sijui ni ujinga…sijui ni kutokujua unataka nini…sijui ni kutokujua kuwa hujui…sijui ni nini hasa!

Manake sielewi. Kama CCM waliiba uchaguzi wa 2020. Uchaguzi uliowapa ushindi John Pombe Magufuli na Samia Suluhu Hassan ushindi mkubwa sana, iweje leo Rais Samia apendwe sana na watu waliokuwa mstari wa mbele kudai kuwa chama chake kimeiba uchaguzi
Hakuna anayejipendekeza bali kuna tofauti kubwa ya uongozi baina ya Magufuli na Samia! Magufuli alikuwa hardliner katili na alikuwa tayari kuua wakati Samia amechukuwa msimamo wa kati na ameonyesha yuko tayari kwa mazungumzo. Hivyo kwa msimamo huu watu wanataka mazungumzo yafanyike sasa na siyo baadaye.

Kwa Magufuli it was just a matter of time kuwa watu wangefika mwisho wa uvumilivu na angekabiliwa na upinzani ambao hangetegemea. Hivyo angeua watu wengi sana ili kulinda utawala wake lakini asingefanikiwa. Matokeo yake yangekuwa uasi usio na kikomo na nchi ingeathirika sana kiuchumi.

Hivi sasa watu wanataka kutumia fursa hii ambayo angalau kunaweza kupatikana mabadiliko ya amani kabla hajapatikana dikteta mwingine.

Pia kumbuka Samia kwa Uzanzibari wake hana cha kupoteza kwa mabadiliko yo yote ya kisiasa!
 
Mkuu hiyo kauli ya kuibiwa kura njia tu ya kujifariji baada ya kushindwa kila uchaguzi lazima waseme hivyo ndio kawaida hiyo.

Hivi mkuu uliwahi kuona wapi mtu unaibiwa kura mil 12 kweli!!?

Yaani we una kula mil 1 mwenzako 12 mil alafu eti umeibiwa, umeibiwaje mikura yote hiyo?

Hakuna kitu hapo ni kudemka tu na biti la kuibiwa ili kujipa imani.

Sasahivi wako bize na kutaka kumnyoa mama huku mwenzao akiwa busy kuimarisha chama chake, anapandisha mishahara vijana wa chuo kawapandishia boom wazee vijijini humo ambao hasa ndio wapiga kura wanafurahia umeme wa REA alafu uchaguzi ukifika uwaambie eti mama hafai nani atakuelewa unadhani na safari hii wasipo kuwa makini hata hiyo mil 1 sidhani Kama watapata na akigombea tena yule mropokaji ndo kabisa.
 
Nguvu ya Chama cha Siasa, na chama chochote, ni wanachama siyo viongozi. Nitatoa mifano kuthibitisha hoja yangu.

Uchaguzi wa 2015, CHADEMA ilitegemea nguvu ya Lowassa na kundi la wanasiasa aliohama nao kutoka CCM. Walifanikiwa kupata idadi kubwa ya madiwani na wabunge hadi kuongoza baadhi ya Halmashauri. Kwa kuwa walitegemea nguvu ya viongozi hawakuweza kuaminiwa kuunda Serikali.

Uchaguzi wa 2020, CHADEMA pia ilitegemea nguvu ya Lissu, wakiamini kushambuliwa kwake ungekuwa mtaji wao wa kisiasa. Badala yake chama kiliambulia Mbunge mmoja tu.

Mifano hiyo miwili inadhihirisha kuwa bado viongozi wa CHADEMA hawajaona umuhimu wa kutumia nguvu ya wanachama. Wanachofanya ni kuwatumia wanachama kufanikisha malengo yao binafsi ya kisiasa. Kumpamba Rais, mama Samia, lengo lao kuu wanalijuwa viongozi na si wanachama. Hata dai lao la Katiba, lengo ni la viongozi kuingia mdarakani.

Umefika wakati kwa viongozi wa CHADEMA kuishi kwenye kaulimbiu yao ya "PEOPLES POWER" na si vinginevyo.

Eda ni ada yenye faida, wahenga walinena.
Kama nguvu ya CHADEMA ni viongozi wao ccm isingetumia mabomu kupata kura
 
Kwa akili yako nani anajipendekeza kwake. Kumdai katiba na tume huru ni kujioendekeza ?!.

Yule mwingine alikuwa jambazi la kisiasa. Lililoingia kwa bahati mbaya na uzuri Mungu amemaliza manung'uniko ya wananchi. Huyu wa sasa hawezi kufanya ujambazi ule. Kwa ni diplomat na asingependa sifa zake zife kuwaridhisha wahafidhina . Pili angalau ni democrat kidogo kulinganisha na aliedhani atadumu navyo milele .

After all wewe Nyani Ngabu ulikuwa ukimnanga mama mwanzoni. Kulikoni ?!
 
Unashangaa kura milioni 12 kuibiwa! Kwani katika vituo vya kura kulikuwa na wawakilishi wa upinzani? Hukumbuki hata katika majumuisho idadi ya kura za Masasi zililingana na kura za Rorya kitu ambacho si cha kawaida. Huna habari kuwa hadi leo tume ya uchaguzi imeshindwa ku- reconcile kura kwa nchi nzima?
Mkuu hiyo kauli ya kuibiwa kura njia tu ya kujifariji baada ya kushindwa kila uchaguzi lazima waseme hivyo ndio kawaida hiyo.

Hivi mkuu uliwahi kuona wapi mtu unaibiwa kura mil 12 kweli!!?

Yaani we una kula mil 1 mwenzako 12 mil alafu eti umeibiwa, umeibiwaje mikura yote hiyo?

Hakuna kitu hapo ni kudemka tu na biti la kuibiwa ili kujipa imani.

Sasahivi wako bize na kutaka kumnyoa mama huku mwenzao akiwa busy kuimarisha chama chake, anapandisha mishahara vijana wa chuo kawapandishia boom wazee vijijini humo ambao hasa ndio wapiga kura wanafurahia umeme wa REA alafu uchaguzi ukifika uwaambie eti mama hafai nani atakuelewa unadhani na safari hii wasipo kuwa makini hata hiyo mil 1 sidhani Kama watapata na akigombea tena yule mropokaji ndo kabisa.
 
Mkuu hiyo kauli ya kuibiwa kura njia tu ya kujifariji baada ya kushindwa kila uchaguzi lazima waseme hivyo ndio kawaida hiyo.

Hivi mkuu uliwahi kuona wapi mtu unaibiwa kura mil 12 kweli!!?

Yaani we una kula mil 1 mwenzako 12 mil alafu eti umeibiwa, umeibiwaje mikura yote hiyo?

Hakuna kitu hapo ni kudemka tu na biti la kuibiwa ili kujipa imani.

Sasahivi wako bize na kutaka kumnyoa mama huku mwenzao akiwa busy kuimarisha chama chake, anapandisha mishahara vijana wa chuo kawapandishia boom wazee vijijini humo ambao hasa ndio wapiga kura wanafurahia umeme wa REA alafu uchaguzi ukifika uwaambie eti mama hafai nani atakuelewa unadhani na safari hii wasipo kuwa makini hata hiyo mil 1 sidhani Kama watapata na akigombea tena yule mropokaji ndo kabisa.

Nimecheka kwa nguvu huu utoto ulioandika hapa.
 
Sawa we cheka tu huku ukisema utoto uchaguzi ukifika utakuja tena hapa kulia mnaibiwa kura na kura viapo vya kuingia barabarani
 
sasa si uhamie huko unasubiri nn, wanaume wapo wengi tu hawajaoa kule!.
Umejuaje hilo kama ww sio muhanga wa hao wanaume. Aisifiae mvua imemnyea.. bila shaka vibunzi yao tayar vishapita kwenye to.bo lao
 
Back
Top Bottom