Kama chuki kweli Clouds fm mnatisha kwa Lady J dee

Joined
Aug 23, 2013
Posts
71
Reaction score
10
Daaaa pamoja na kwamba kiasi flani mnawainua wasanii wa Hapa nyumbani ila hampo sawa kwa msanii Lady j dee! kama haujanielewa sikiliza clouds fm wiki ijayo kwenye wimbo wa BEN POL. Jikubali pale anapolitaja jina la j dee. wameminya ile mbaya. Najiuliza kumshirikisha jide tu kunaweza pelekea usipate sapoti ya media hii ambayo inajiita Radio ya watu! Watz bwana! yaani mtu kueleza ukweli jinsi anavyoibiwa kosa. Hata kama hammpendi j dee basi wimbo ni wa ben paul basiii hakuna haja ya kulibana jina la jdee. Radio gani ya watu yenye ubaguzi? Walipeni cha kwao ila msiwaibie kwa kigezo cha kuwanyima airtime kwenye kiredio chenu. ikumbukwe kwenye vikwazo ndo fursa hizo. siungi mkono huo utaratibu wenu. wewe Kusaga na nani na nani........ mjipangeeeeeeeeeeeeeeee.
 
Ahaaaaaa., ngoja aje kibonde asome atakujibu kesho
 
Unaonekana unawakubali kiaina ila basi tu kwani hakuna radio zingine za kupiga nyimbo za JD
 
Hizo redio nyingine hata kuzisikilizaga naona kichefuchefu tu, hasa redio hiyo; ndiyo kabisaaaa!
 
Hivi ile kesi ya ruge kumstaki jide inaendeleaje au imeishaje?
 
Binafs naona Jide anazidi kufanikiwa,YAHYA WAKE ANACHEZWA REDIO ZOTE,NA ANASHIKA NAFASI YA JUU KWENYE HIZO CHART,JAMBO AMBALO HATA WASIPOPIGA YEYE ATA-SHINE,RIZKI YA MTU HAIPO KWA MTU,ILA MUNGU HUIPITISHIA KWA MTU
 
tena jide kajipanga balaa kuna bonge la ngoma kafanya na juma nature linakuja
 
J.Dee ni moto wa kuotea mbali! Clouds mnahangaika bure, habaniwi huyu dada,Nawashangaa sana mnaoendelea kusikiliza Kiredio uchwara....!Kazi majungu na wizi tu..Jay Dee kaza buti mama achana na viredio mbao kama hivyo......
 
JIDE anakipaji cha hali ya juu, kwasasa it is too late kummbania wangelitaka hili basi wasingekubali hata kumuingiza smooth vibes enzi zile anatoka na albam ya "machozi".
 
Jide keshawaambie hata akifa, Ruge na Kusaga wakitia timu msibani wapigwe mawe na waombolezaji, tena radio yao isitangaze habari za kifo chake. Naona nao wameamua kutii mapema kwa kutolitaja jina lake.
 
Kuna muda waweza zuia jambo kama si kilichelewesha halafu ikipita hiyo kipindi ni kwamba huwezi tena kizuia!!!

Inakuwa kama kuzuia upepo kwa mikono!!!!

Huyu dada kwa sasa hawawezi tena kumchafua au kumkalia relini
 
Karedio kenyewe hata kwenye tuneIn hakapo halafu wanaringa ndo mana siku hizi mi nasikiliza tbc taifa na nyumbani ni nyumbani na nikijisikia kuchoka na ka smart phone kangu nasikiliza redio za mbele na sio haka karedio ka kinafiki ,,, big uo yahaya unaishi wapi
 
Hicho kibibi mbona chenyewe kwenye ule waraka wake kiliandika kwamba hakitaki Ruge na Joey waende kwenye msiba wake na kama ikitokea wakienda basi washabiki na wapenzi wake wawapopoe mawe...sasa kwa nini Clouds waendelee kukipa promo?

Hivyo kama unazungumzia chuki basi anza kwanza na hicho kibibi. Hakina bifu ya kweli na Clouds zaidi ya kutafuta kiki tu.
 
nimesha sahau kama kuna kitu inaitwa clouds fm, c ckiliz radio ya majungu na unyonyaji. PUMBAVUUUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…