Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Mdogo wangu ni retired Dr. Juzi alikuwa anaangalia kumbukumbu ya kifo kwenye tv. Moja ya tangazo aliloliona ni tangazo la mgonjwa aliyefariki miaka 12 baada ya kumfanyia upasuaji, alishtuka na kuumia sana.
Mdogo wangu aliumia si kwa sababu nyingine bali anaeleza kuwa wao madaktari ni walinzi wa uhai na kiapo chao ni kuokoa maisha. Anaposhuhudia uhai ukitoka mikononi mwao pamoja na juhudi kubwa walizofanya uumia sana. Daktari utibu kwa akili za kawaida lakini pia kila hatua umshirikisha Mungu awape ulinzi na mwongozo wa Nini wafanye, anasema huyu ndugu yangu.
Story na machungu aliyonayo yakanifanya nijiulize ni namna gani baadhi ya matangazo kwenye social media na vyombo vingine kwa habari yanawaumiza watu tusiowajua? Lakini nikasema ukitenda kwa haki maumivu ya kile ulichokiona yataambatana na faraja kutoka kwa Mungu.
Lakini nilipoanza kutafakari nikakumbuka juzi nilisoma kumbukizi ya Mawazo aliyeuawa Geita, Leo nikaona wanamzungumzia Ben Saanane aliyetekwa na kupotea tusijue alipo, nikakumbuka kuwa kuona kilichotokea Zanzibar kwenye uchaguzi nk nikajiuliza Hawa waliotenda haya waonapo matangazo wanaumizwa Kama madaktari? Wakiumizwa ujifariji kwa kipi ilihali awakufanya kwa haki?
Ewe mwanadamu, social media na viweka kumbukumbu vimewekwa kukumbusha uliyowatendea wanadamu wenzio, hatutachoka kuwakumbuka waliotangulia, vivyo hivyo atutachoka kukukumbusha huko uliko kwamba huu uhai ulitoka kwa maelekezo yako, kwa mikono yako au kufedha zako.
Hii dhambi haina toba zaidi ya kukiri hadharani. Kuua toba yake ni kukiri adharani, Mwenyenzi Mungu hana siri