Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Vyema. Tujadili mantiki ya hoja bila ushabiki wa kidini.Kamanda, unaonaje wewe unayepinga ukathibitisha kuwa hayupo?
Nimethibitisha mara nyingi sana kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, kwa "proof by contradiction".
Kwa mfano wa "the problem of evil".
Kuwezekana kuwepo kwa mabaya katika ulimwengu ulioumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni contradiction.
Kama Mungu huyo yupo na ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kuwepo?
Contradiction hii inaonesha Mungu huyo hayupo, habari za kuwepo kwake ni hadithi za kutungwa na watu tu katika jitihada za kupambana na mazingira yao na kuelezea vitu ambavyo hawana majibu ya kuvielezea.
Ndiyo maana ukisoma misahafu unaona Mungu huyo anapewa tabia za watu, mara Mungu kakasirika, mara Mungu kashangaa watu wamemuasi kawaletea gharika. Mungu anayejua kila kitu kitakavyokuwa kabla hakijawa atashangaa vipi watu wamemuasi?
Kama alijua mambo yatakayokuja, uasi ambao alishaujua utatokea ataushangaa vipi?
Conclusion, huyo Mungu ni hadithi za kutungwa na watu tu, hayupo.
Kama unabisha, thibitisha Mungu huyo yupo.