Hayo tunayo shuhudia kwa Waarabu yawezekana hawa viongozi wetu wanafikiri ni picha za filamu au michezo
ya maigizo, ama wana fahamu ila kutokana na uwezo mdogo wa kufikiri na kutafakari wanadhani ni 'mlipuko' wa ghafla from nowhere.
Ila kwa mtu yeyote aliye makini atafahamu kuwa hayo wanayofanya waarabu ni matokeo na matunda ya
ufisadi wa muda mrefu ambapo watawala walijifanya viziwi na vipofu!
Yapaswa ifahamike kuwa hali ya kuchoswa, kukata tamaa kutokana na ufisadi,dhuluma na ukandamizaji
unaofanywa na Watawala ndivo vinavo sababisha haya tunayo yaona TUNISIA na MISRI hatimae Tanzania.
Haya sio madogo kamwe na wala sio ya kupuuza kwani hata hao waarabu ilikuwa hivihivi.Ilianzia kwa
makundi madomadogo kama wanafunzi wa vyuo, vifaru na mabomu vikatumika kuzima fikra hizo bila utatuzi
wa kidiplomasia. Na punde muda ulipofika Taifa zima likahamasika vifaru na mabomu ya awali ikawa havifai tena mbele ya nguvu ya UMMA.
So it is just a matter of time!
'The more men you make free, the more freedom is strengthened and the greater is security of the state'
state'(Fredrick Douglas-1869)