Kama Elimu ni bure, kwanini Afya pia isiwe bure?

Kama Elimu ni bure, kwanini Afya pia isiwe bure?

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
915
Reaction score
1,082
Elimu ni bure . Afya nayo kwanini isiwe bure?

Naomba kufahamu serikali ilichukua kipaumbele gani kutoa elimu bure na sio Afya.
 
[emoji419] Elimu bure .... Afya nayo kwanini isiwe bure? Naomba kufahamu serikali ilichukua kipaumbele gani kutoa elimu bure na sio Afya.
Kama Marekani taifa kubwa wameshindwa kutoa huduma za afya bure, wanatumia bima itakuwa sisi ?! Labda ugombee ubunge upeleke hoja binafsi bungeni ya kuomba ongezeko la angalau sh.50 kwenye bei ya mafuta ili pesa itakayopatikana ipelekwe hospitalini ili watu watibiwe Bure !!
 
Ujajibu kilichoulizwa. Elimu bure imekuwaje bure na AFYA sio bure? au bajet ya elimu na Afya ikoje ndo nataka nieleweshwe.
 
Hakuna chochote cha bure. Someone somewhere is paying for that.

Tofauti ni namna tu ya unavyolipia, elimu inalipiwa indirectly kupitia kodi, matibabu unalipia kwa njia zote mbili (direct sehemu ya huduma na kupitia kodi).

Mimi binafsi napenda kulipa directly, sio tunatozana mikodi kibao kwa huduma za hovyo.
 
Elimu ni bure . Afya nayo kwanini isiwe bure? Naomba kufahamu serikali ilichukua kipaumbele gani kutoa elimu bure na sio Afya.
Hakuna kitu cha bure duniani ukiona unapokea kitu bure ujue kuna mtu kalipa kwa niaba yako anakudanganya bure.

Waalimu inalipa serikali, vitendea kazi inalipa serikali bado unaambiwa bure unakubali wa TZ kwa kupenda bure.
Pamoja na kuwa serikali inalipa bado kuna changamoto nyingi tu huko kwenye bure.

Hata afya bila serikali kuchangia tusingemudu gharama za matibabu. Ukitaka kujua gharama za matibabu nenda Agakhani Dsm huduma nzuri ila utamu utauona kwenye gharama.

Ukitaka kujua afya serikali inachangia pakubwa fananisha hospital binafsi na hospitali za umma ndio utajua serikali inachangia nini.
 
Hakuna kitu cha bure duniani ukiona unapokea kitu bure ujue kuna mtu kalipa kwa niaba yako anakudanganya bure...
Hata shule binafsi. Hizo hela serikali inapata wapi kama sio zetu walipa kodi. Jitambue Tanzania inawezekana Elimu kuwa bure na Afya kuwa bure.
 
Hata shule binafsi. Hizo hela serikali inapata wapi kama sio zetu walipa kodi. Jitambue Tanzania inawezekana Elimu kuwa bure na Afya kuwa bure.
Kwa kodi ipi?

Unasikiliza budget ya serikali au unaongea tu.

Makusanyo ya ndani yaani kodi hayatoshi budget ya mwaka ili budget itoshe kuna mikopo, fedha za misaada

Nenda kwenye tovoti ya wizara ya fedha kaangalie budget yetu ya mwaka huu fedha ya kodi ni shilingi ngapi?

We unadhani mataifa tajiri kwa nini yana nguvu kwa mataifa maskini. Kwa sababu mataifa maskini hayajitegemei kwenye budget
 
Back
Top Bottom