Tumeona malanzimeni wamekuwa wakiongezwa toka wawili mpaka wanne, je kama ataongezwa mchezaji wa 12, unahisi atacheza upande upi uwanjani katika timu husika?
Itabidi awe na uwezo wa kuishinda gravity au atakuwa na flying powers ili awe anapita juu ya vichwa vya wachezaji wenzake. Yeye atakuwa maalum kwa 'kutungua minazi' na kuirudisha chini mipira iliyopigwa juu sana.
Mbona nafasi ipo...kwa sisi tuliosoma kidumu fagio mechi za mpira wa miguu ilikuwa ni kati ya darasa na darasa.Tulikuwa tunacheza zaidi ya kumi na tano na gemu linanoga.
Ukifuatilia historia utagundua mpira ulikuwa unachezwa na idadi kubwa ya watu.aliyeleta hivi vijisheria ni muingereza.