The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Kichwa kiko wazi. Nashindwa kumuelewa tapeli na askofu wa kujipachia Josephat Gwajima. Anajitahidi kutupiga changa la macho akijifanya kulaani utekaji na maovu ya chama chake. Ukimchunguza, licha ya kuwa. tapeli wa kidini kama wengine wanaowahadaa na kuwaibia mazwazwa na wavivu waliokata tamaa, ni chawa wa kunuka.
Nashauri na kutahadhari, tumtahadhari kiumbe huyu ambaye wengi hawajamstukia. Sawa na machawa wengine waliobwagwa kwenye uteuzi wakaendelea kuunga juhudi, si Mpina wala wengine bali anaweza kuwa pacha wa Kabwe na tapeli la ubwabwa aliyejificha nyuma ya uaskofu wa kujipachika. Naweza kumuita mawala au njala mbaya.