Kama Haji Manara hasingekuwepo, Mpira wa nchi hii ungekuwa ulishakufa siku nyingi

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
242
Reaction score
676
Kama Haji Manara hasingekuwepo. Mpira wa nchi hii ungekuwa ulishakufa siku nyingi. Kaburi lake lingekuwa limeota nyasi, na Msalaba wake ungekuwa umeanza kufutika maandishi. Huu ni ukweli mchungu unaouma. Ila inatulazimu tu tuupokee. Ili kweli ituweke huru Kwenye hii dunia ya dhambi.

Ujio wa Haji Manara Kwenye mpira wetu. Ni kama ekarist iliyotua juu ya meza ya kasisi. Au tezi bii kwenye viganja vya mikono ya Imamu. Vyote ni ishara ya kwamba ndani ya nyumba ya Allah. Kuna uhai wa misa na ibada.

Ujio wa Haji Manara msimbazi, umeleta chachu, msimsimko, na ushindani wa ndani na nje ya uwanja. Kwenye mpira wetu wenye maneno mengi. Yanayoishi mbali na sayari ya uhalisia. Haji anahitajika kuliko wallet iliyosheheni kibunda cha noti za elf kumi kumi. Kwenye mfuko wa suruali ya mzinzi.

Ulimi wa Haji umebarikiwa ushawishi na uhamasisho wa kiwango cha juu mno. Ni watu wachache sana wanaotunukiwa Karisma ya namna hii.

Kabla ya ujio wa haji pale msimbazi. Mpira wetu ulikuwa unasumbuliwa na saratani ya unyonge viwanjani na ukosefu wa hamasa. Lakini ujio wa Doctor Haji umevitibu kiufasaha vitu hivi.

Leo timu nyingi zinaandaa matamasha nakuiga kauli mbiu (Slogan). Bila kumrudishia sifa na heshima muasisi Haji Manara. Kuiga kitu kizuri sio dhambi. Dhambi ni kukiiga na kukifanya chini ya kiwango.

Hamasa aliyoileta Haji ndani ya mpira wa nchi yetu. Nikitu ambacho hata akifa leo, na sisi tukagoma kukitambua. Maandishi yatayokuwa juu ya kaburi lake. Yatakuwa yakifanya kazi ya kuzisuta nakuzihukumu nafsi zetu. Kwenye swala la hamasa Haji ameleta mapinduzi ya kutisha.

Kwa hili tumrudishie sifa kabla pumzi hazijaota mbawa ndani ya matundu ya pua zake. Na mauti kulifunga jalada la uhai wake.

Binafsi, naiomba wizara ya utamaduni sanaa na michezo. Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Bila kujali tofauti ya itikadi na vyama. Wakae kama kamati. Wajadili jinsi ya kumjengea sanamu ya ukumbusho haji manara. Tusisubiri afe ndio tuanze kumuandikia tanzia ndefu za pongezi.

Tukiitenda hii dhambi, kesho mbele ya kiti cha haki tutaikosa pepo kijinga.

Tukiweka ushabiki wa Simba na Yanga Kando. Na tukaamua kuiishi kweli. Haji Manara ndiye kiumbe aliyeufufua msisimko kwenye soka letu. Msimsiko ambao ulikata roho sababu ya mpira wetu kuendeshwa bila mipango, malengo, na itakavyo kasi ya dunia ya leo.

Mashabiki wa Simba wenyewe wana msemo wao. Msemo wenyewe ni huu. Eti, ALIYEMLETA HAJI MANARA MSIMBAZI. MOJA KWA MOJA PEPONI."
 
Tumekusikia hadji. Hongera kwa kujipa promo. Endelea zaidi na zaidi.
 
Anajua kazi yake na anaifanya ipasavyo.., sifa unazompa hapa ni recognition tosha kabisa.., hayo ya kujenga mpaka sanamu tutakuwa tuna- make a mountain out of a molehill
 
πŸ˜€πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜…
 
nimeshindwa kuendelea kusoma,uandishi huu hatari sana
 
Matumizi mabaya ya mawazo
 
Wakati washabiki wa Yanga tuna Ubongo wa Simba wamejaa Kamasi kichwani, Ndio maana
Wanatuita Ombaomba wakati Timu ni ya kwetu WANANCHI tunaochangia ni sisi wenyewe
wananchi sasa ombaomba ni nani hapo kati yetu na yule anayetegemea mfuko wa GABACHORI?
 
MO akiondoka SIMBA mbwembwe zote kwishney.....

japo manara amechangia hamasa...sikatai
 
Haji ana ukorofi na utoto mwingi...

Mwili wake upo Simba ila roho yake ipo Yanga...



Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…