Kama hali ikiendelea hivi bila mvua mpaka mwezi wa Sita, mwaka huu utakuwa mgumu sana

Kama hali ikiendelea hivi bila mvua mpaka mwezi wa Sita, mwaka huu utakuwa mgumu sana

Artifact Collector

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
6,617
Reaction score
10,205
Kwenye Ile mikoa ambayo msimu wa Masika unaanza mwezi wa 11 hali ni mbaya mingine mpaka sahivi hakuna mvua ni msimu wa mvua. Na hii mikoa ndo mingi inayozalisha chakula kingi.

Tofauti na Ile inayopata mvua mwezi wa tatu mpaka mwezi wa Sita mwanzoni

Kama una hela weka akiba ya hela kwa sababu ya scarcity vyakula vitaenda kupanda, kama una akiba ya chakula weka akiba ya chakula, Kuna uwezekano hali ikawa mbaya sana kuanzia June na kuendelea

Watumishi wa kiroho huu ni mda wa kuombea mvua msisubiri Hali ikiwa mbaya mkasema mlitabiri sababu viashiria vyote vimeshaonekana
 
Kama una hela weka akiba ya hela, kama unaakiba ya chakula weka akiba ya chakula, Kuna uwezekano hali ikawa mbaya sana kuanzia June na kuendelea
thinkstupid.png
 
Kilimo cha kutegemea mvua kimepitwa na wakati.
Serikali inatakiwa iwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji nchi nzima.
Inawezekana hata kwa kutumia mikopo mradi ndani ya miaka miwili kila mkulima akawa na uwezo wa kulima muda wowote provided tuna maji ya kutosha.
 
Ila wewe kweli hamnazo hayo maji ya kumwagilia nchi nzima mtayavuta bahari ya Hindi,
Vyanzo vya maji (mito) inakauka kabisa nenda vijijini utajua!!!
Duuuu poleni Simanjiro (Manyara) kwa ukame unawakumba mpaka mifugo inakufa
 
Kwenye Ile mikoa ambayo msimu wa Masika unaanza mwezi wa 11 hali ni mbaya mingine mpaka sahivi hakuna mvua ni msimu wa mvua. Na hii mikoa ndo mingi inayozalisha chakula kingi

Tofauti na Ile inayopata mvua mwezi wa tatu mpaka mwezi wa Sita mwanzoni

Kama una hela weka akiba ya hela kwa sababu ya scarcity vyakula vitaenda kupanda, kama unaakiba ya chakula weka akiba ya chakula, Kuna uwezekano hali ikawa mbaya sana kuanzia June na kuendelea

Watumishi wa kiroho huu ni mda wa kuombea mvua msisubiri Hali ikiwa mbaya mkasema mlitabiri sababu viashiria vyote vimeshaonekana
Ndiyo maana waafrica hatuendelei Kwa kuwa na mawazo finyu Sasa Mungu anahusikaje na mvua,? hao wachungaji Kwa kujua huo ugonjwa wameendelea kujitajirisha
 
Tupeni muda kidogo tufanye shooting madarasa ya mama kwa ajili ya kuonyesha tibisii...........tujipimie urefu wa kamba zetu then tutakuja kuwafariji watu wa manyara kwa kufiwa na mifugo yao kutokana na ukame mkali, kwa aina ya viongozi tulio nao kwa sasa prepare for the worst......
 
Kwa mtu anayeijua Jografia ya Tanzania hatakiwi kutoa comment kama hii ya kwako.
Kwani maji ya mito yanatokana nini, mfano Kilombero ifakara mito imekauka na chemchem zimekauka sababu ya uhaba wa mvua.

Mito na chemchem zinategemea sana mvua ili zititiririshe maji ndo maana jangwan hamna mito wala nchemchem
 
Kilimo cha kutegemea mvua kimepitwa na wakati.
Serikali inatakiwa iwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji nchi nzima.
Inawezekana hata kwa kutumia mikopo mradi ndani ya miaka miwili kila mkulima akawa na uwezo wa kulima muda wowote provided tuna maji ya kutosha.
Maji hayo utapataje hydrolysis kiini chake mvua labda useme maziwa ya maji baridi
 
Kwa mtu anayeijua Jografia ya Tanzania hatakiwi kutoa comment kama hii ya kwako.
Kwa hiyo ww ndiyo unajua jografia,, basi kawaambia serikali ifanye kilimo cha umwagiliaji,, wakati hapa nchini aslimia 5 ndiyo wanategemea hicho kilimo hicho,, usifikiri kila sehemu kuna mito, sehemu nyingine wanategemea mvua
 
Back
Top Bottom