Sidhani kama umefikilia vizuri point ya kuhusu viwanja Mkuu, jiulize kitu kimoja nani anatakiwa afanye vizuri kati ya Yanga anaetumia uwanja mzuri game zake almost nusu za ligi au Dodoma Jiji ambae anatumia almost robo tatu ya mechi zake kucheza kwenye viwanja vibaya?
Mfano ni hivi, chukua mtoto ambae anasoma shule ya kata na anafanya vizuri kitaifa mbele ya wanafunzi wanaosoma feza school, kumbuka huyo mwanafunzi hana mazingira mazuri ya kujisomea,hana walimu wazuri,hana material mazuri,hana marafiki washindani, hya mtoe shule ya kata na mpeleke feza school ambapo huko zile negativity zote huko ni positivity
je we unahisi wapi atafanya vizuri zaidi kati ya mwanzo alipokuwa shule ya kata na alipohamia shule ya Feza? Kwa akili ya kawaida tu team ndogo zilitakiwa zicheze vizuri katika uwanja wa Mkapa au wa Azam kuliko zinavocheza viwanja vibovu vya mikoani na ndomana kwa team zenye falsafa ya kucheza mpira mzuri waga wanatoa upinzani mzuri Sana kwa Simba, Yanga na Azam pindi zinapocheza katika kiwanja kizuri
Hizo team ni kama Geita gold, Biashara, Dodoma Jiji,KMC,Ruvu Shooting, Mbeya City,Namungo na ata Gwambina hizi ni team ambazo zina falsafa ya kucheza mpira mzuri, na waga zinacheza mpira mzuri sana dhidi ya hizi team kubwa tatizo linakuja kwenye ubora wa wachezaji waliopo hizi team ndogo
Team kubwa zina wachezaji wenye quality compared na hizi ndogo na ndio hao ambao wanaamua mechi ata katika viwanja vibovu, kwahiyo viwanja sio issues maana ata team ndogo zinapocheza kwa Mkapa waga wanapata matokeo, kama issue ni viwanja kuna team kama Kagera sugar,mtibwa sugar, pia Azam wana viwanja vizuri sana kuliko ata pitch ya Mkapa ila hawanaga cha home Wala away wao Kila siku vilio tu