Kama hamwezi kuwaandalia watoto wenu Maisha mazuri waachieni Wanaoweza

Kama hamwezi kuwaandalia watoto wenu Maisha mazuri waachieni Wanaoweza

October 2pm

Senior Member
Joined
May 2, 2023
Posts
106
Reaction score
282
Kwema Wakuu!

Ninyi mlidanganywa kuwa mtoto arithi elimu pekeake. Juzijuzi hapa nikawaambia urithi wa mtoto sio elimu pekeake muache kukimbia majukumu yenu. Mkaanza kunitúkana na kunirushia matusi na maneno yakaraha mkidhani ndio nafuu yenu. Nikasema Sawa!

Yaani kwa akili ya kawaida ati umsomeshe mtoto mpaka sijui degree moja au tufanye degree tatu. Alafu umuache hapo ati ndio umempa urithi. Umelogwa wewe sio bure.

Niliwaambia Kumpa elimu mtoto sio sehemu ya urithi na hata kwenye mirathi hakuna kitu kama hicho achilia mbali kisayansi. Hili sitaeleza tena.

Sasa juzi sijui kulikuwa na mashindano sijui uchaguzi wa chipukizi kitu gani huko CCM. Jambo ambalo lilizua zogo mitandaoni. Oooh! Wanaandaa watoto wao! Ooh! Wanataka yaangalie haya majitu ya hovyo. Malafi! Mara ooh! Hivyo vitoto ni vidogo sio haki kabisa.

Najua hampendi ukweli wangu. Lakini pia najua mnajua mimi sijali kuwa mnapenda au hampendi. Lakini ninachotaka mjue ni kuwa hakuna mtu yupo kwaajili ya kuwaandalia watoto wako Maisha au mafanikio yao.

Wakati ninyi mkidhani kuzaa pekee inatosha. Msiwaonee wivu na chuki wanaosomesha watoto wao.
Na wakati ninyi mkisomesha watoto wenu na mkidhani inatosha. Msiowaonee wivu wale wanaowasomesha na kuwaandalia kazi au miradi au makampuni yao.

Oooh! Watoto wao hawana akili. Sawa hawana akili lakini wazazi wao wanaakili ndio maana wamewazidi karibu kwa kila kitu.

Kama sio mbeleko ya Baba yake asingekuwa pale alipo. Wewe mbeleko ya Babaako uliitupia wapi?

Sio kosa kisheria mtu kumrithisha mwanaye cheo au madaraka. Sio kosa kumrithisha mtoto wako Kampuni au miradi uliyomuandalia. Ilimradi usivunje sheria.

Wakati wewe ukiwaza kumuandaa mtoto wako aje kuwa Mwalimu, Daktari, Mhasibu au mwanasheria n.k. na Watu hawakuonei shida. Elewa kuwa wapo Watu wanaowaandaa watoto wao kuwa Rais, Mawaziri, wabunge, Mkuu wa Majeshi n.k. Sasa kwa nini wewe umuonee mwenzako kijicho.

Kila mtu apambane kwa nafasi na uwezo Wake. Wewe kama umeshindwa sio kila mtu atashindwa kama wewe.

Dunia ni ileile haijabadilika ila uongo ndio unabadilika. Ukweli ni kuwa kila mtu atapambana kwaajili ya familia yake. Kila taifa litapambana kwaajili yake. Na sio vinginevyo.
 
Sasa mtoto kumuigiza ccm ndo umemsaidia kuwa well informed and satisfied with his or her career sometimes we're entertain shit because we no longer thinking deeply.
 
Back
Top Bottom