Kama haupotezi marafiki kubali kuwa haukui na haujitambui

Kama haupotezi marafiki kubali kuwa haukui na haujitambui

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Mtu anayejitambua huwa hawi na marafiki walewale muda mrefu ni nadra
Marafiki huja na kuondoka kutokana na hali iliyopo kipi mnashirikisha

Rafiki akija shukuru na akiamua kuondoka shukuru

Watu wanaojitambua hawana marafiki wa muda mrefu, hawa ni rahisi kuwa maadui na mara hupenda kubadilisha
Mfano
- Kikwete aliwahi kuwa rahisi wa Lowasa, ila walikuja kuwa mahasimu

- Diamond Platinumz alikuwa rafiki wa Alli Kiba, Sasa ni mahasimu.

- Gambo alikuwa rafiki wa Makonda Sasa ni maadui

Hiyo ni baadhi ya mifano
 
Naona kama umechanganya mambo hapo.
Kupata marafiki wengine na kuhitilafiana na wa zaman!!.
KWeli kukua huendana na kukutana na watu wapya, lakini haina maana ya kulazimika kugombana na watu wako wa zamani!!
 
Kila mtu anavyo kua kwenye sekta yoyote atataka ang'ae kuwazidi hata aliowakuta,

Mara nyingi kila mtu yupo kwenye laini ya kutaka kushinda , amini ya kuwa na ikatokea mtu akanotice kila mmoja anajikataa au kuanza kutengenezeana bifu,, chuki na wivu

Urafiki mara nyingi ni mutual benefits na sii vinginevy
 
Naona kama umechanganya mambo hapo.
Kupata marafiki wengine na kuhitilafiana na wa zaman!!.
KWeli kukua huendana na kukutana na watu wapya, lakini haina maana ya kulazimika kugombana na watu wako wa zamani!!
Ndo hoja yangu haswa ndo maana nikasema kuwa marafiki huja na kuondoka
Mfano urafiki wa Makonda na Gambo, hawa walikuwa marafiki awamu ya Magufuli ila Sasa ni matokeo kuwa Makonda anahitaji nafasi ya Gambo ili atimize ndoto na Gambo hakubali Kwa moto mmoja, hiyo ni nature urafiki ukifika wakati wa kuvunjika hakuna wa kuzuia
 
Kuna tofauti kubwa kati ya URAFIKI na mtu wa KARIBU......

Tuna watu wengi wa karibu kutokana na mazoea na kukutana mara kwa mara tunawaona kuwa ni marafiki zetu!!!!!
 
Kwa kiasi fulani nimejaribu kumuelewa mtoa mada.

Wakati mishemishe zenu nii sawa na malengo yanayofanana mnashirikiana kufikia malengo.

Mkishafikia malengo kiasi fulani ukaribu au bond inapungua.

Kama hamna malengo mengine ya muda mrefu mnajikuta mnakuwa na competition ya kiaina.

Mmojawapo aligundua kuna ushindani na hakuna win win situation tena ni rahisi kila mtu kuendelea na mishe zake au mnaweza kuwa sio lazima maadui ila washindani sababu kubwa kila mtu anakuwa na assume anamjua kiundani mwenzake.
 
Kutokana na umri unavyokwenda,kila kitu hupungua,
hakuna kinachodumu milele,huu ndio ukweli wenyewe,

Kila mtu ana marafiki katika hatua tofauti za maisha yake but ni wachache sana waliobahatika kua na marafiki wale wale katika hatua zote,

sisi sote tunakua,tunahamia maeneo mapya,tunakutana na watu wapya,na mara nyingi tunashindwa kudumisha marafiki wa zamani kama ilivyokua kutokana na sababu mbali mbali,

Kwa kiasi fulani nakubaliana na mleta mada kua,katika stage zako za maisha ukijiona hupati marafiki wapya,basi kuna kitu hakipo sawa kwako,ila sikubaliane nae kua,ukiwa na rafiki wa muda mrefu,basi atageuka kua adui kwako,

Kua na maadui kwenye maisha ni jambo la kawaida sana,ukijiona kua huna maadui,hii nayo huashiria kua,kuna kitu hakipo sawa kwako katika utafutaji wa maisha.
 
Nimekuelewa sana mkuu
 
Back
Top Bottom