- Thread starter
- #21
Umenikumbusha mbali sana,Kumbuka kale kamsemo "uwoga wako = umasikini wako ".....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umenikumbusha mbali sana,Kumbuka kale kamsemo "uwoga wako = umasikini wako ".....
Una akili lakini umeamua kujitoa fahamu ili kutetea utawala dhalimuMsijitoe ufahamu. Katiba mpya ni kwa ajili ya kila Mtanzania. Asiyetaka katiba mpya ni kichaa.
Unapaswa kufanyiwa tohara ya akili ili upate ufahamu japo kidogo tuKuanzisha mjadala wa Katiba Mpya Ni kuanzisha FuJo Za wakati wa Jakaya
Kuna watu watataka uanzie ulipoishia wakati kuna watu watataka uanzie kwenye Rasimu ya Warioba kuna wengine wataibuka uanze upya kabisa
Magu tuletee Reli ya kisasa, mabarabara,stgler gauge, Na mengineyo
Hizo Vurugu Za Kisiasa wanaziweza kina Jakaya WeWe Ni Mtu wa kazi tu
Huo ndio ukweliMsijitoe ufahamu. Katiba mpya ni kwa ajili ya kila Mtanzania. Asiyetaka katiba mpya ni kichaa.
Mjadala wa chuo kikuu ulikosa mwelekeo baada ya professors wachokoza mada kutaarifiwa kuwa JPM yupo Nkurumah Hall. Huu ni ujinga wa kitaaluma na uzezeta wa kiprofesa Tanzania.*Anaandika Dotto Bulendu.*
Inawezekana waliotufundisha na wale tuliosoma nao ambao wana nafasi ya kusema na kushauri wameamua kukaa kimya.
Hivi hatuoni ama tunaona wachache ama tunaoona hatuoni vizuri?
1.Asilimia kubwa ya watumishi katika sekta binafsi nchini Tanzania sasa hawana uhakika na maisha,wengi wana zaidi ya miezi sita bila mshahara,hili halihitaji mjadala juu ya mwelekeo wa nchi yetu na namna ya kuinasua sekta binafsi?
2.Leo ukitembea mikoa yote mabango ya matangazo yapo matupu,yawezekana makampuni yamepunguza kwa kiwango kikubwa bajeti ya matangazo kutokana na mazingira ya biashara,hili halihitaji mjadala juu ya hali ya biashara nchini?
3.Makampuni kila kukicha yanatangaza kupunguza watu na hivi juzi shirika la umma(TTCL),limetangaza kupunguza watumishi wapatao 555,(kwa mujibu wa Tangazo lililoonekana mtandaoni),na tunaambiwa wanaopinguzwa eti hawajui kutumia teknolojia,hivi inaingia akilini?sekta binafsi ndiyo inapunguza kila kukicha huku ikisimama kuajiri,hili nalo halihitaji mjadala?ama sisi wengine tunatazama haya mambo vibaya?
4.Kundi kubwa la vijana waliohitimu elimu ya chuo,taasisi za juu na vyuo vikuu na bahati mbaya hata lile lililokwenda JKT baada ya kumaliza elimu ya juu,lipo mtaani linasubiri ajira kwa mwaka wa tatu sasa,hawa watu tunawapeleka wapi?hivi suala la ajira kwa vijana siyo mjadala?ama sisi wengine tunatazama mambo vibaya?
5.Walio kwenye ajira ndani ya sekta ya umma na binafsi karibu mwaka wa tatu sasa wanakilio cha nyongeza ya mishahara,hivi hili nalo siyo mjadala?tunajua athari za watu kukaa wakilalamika moyoni?
6.Tunaambiwa mpaka sasa viwanda zaidi ya 3000 vimejengwa nchini,tukiuliza viko wapi?maana vile alivyojenga Mwalimu kuanzia Tabora mpaka Mara,akaenda Mbeya Mpaka Kilimanjaro vingi bado ni maghala ya vyuma chakavu.Maana Mwalimu akijenga viwanda karibu mia nne na mashirika ya umma karibu 180,matokeo yake yalionekana kwa macho kila kona ya nchi,hivi elfu 3 na zaidi vipo wapi na vinafanya nini?Ama sisi hatutazami vizuri haya mambo?
7.Kuna watu walipotea(Ben Saanane,Azori Gwanda),mpaka leo hatujui wapo wapi?waziri wa Mambo ya ndani alipata kuulizwa kuhusu walipo watu hawa,akasema yawezekana wamekwenda kutembea!hivi kweli hili ni jibu sahihi?ama sisi wengine tunatazama mambo haya vibaya?
8.Juzi nilikuwa nasafiri kwa usafiri wa Anga,wakati natafuta tiketi nikashangaa kukuta ndege ya shirika la umma,bei zake ni juu kuliko ndege za makampuni binafsi?nikajiuliza mbona tulikubaliana ndege za serikali zitakuwa nafuu kwa kila mtanzania?au sisi tunatazama haya mambo vibaya?
9.Nenda leo vituo vya mafuta uine kasi ya upandaji wa bei ya mafuta,unajiuliza mbona zamani bei ilikuwa ikipanda tunasikia sauti za walaji na serikali inajibu?leo kila mtu anayasikilizia haya mambo moyoni.Au sisi ndiyo tunatazama haya mambo vibaya?
10.Haya tuliambiwa miaka mitano iliyopita kuwa Gesi ndiyo mwarobaini wa shida za watanzania,baadae Gesi si hoja tena sasa ni umeme wa maji,unajiuliza hivi uwekezaji wetu kwenye gesi umetupa faida ama lah?au sisi ndiyo tunatazama haya mambo vibaya?
11.Tukienda Halmashaurini tunaambiwa aaaah,siku hizi mambo yamebadirika kila kitu serikali kuu ndiyo maana mambo hayaendi,unajiuliza mbona hili halijadiliwi?ama sisi ndiyo tunatazama vibaya?
12.Jana Rais kauliza ipo wapi sekta binafsi?kwani zabuni zote alizotangaza sekta binafsi haikumudu,kama Rais anakiri kuwa sekta binafsi ni dhaifu na tuna sera ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi,kama sekta binafsi ni dhaifu je serikali izibeze ama ilikuze?
13.Uandikwaji wa katiba ama kutokuandikwa si matakwa ya kiongozi,chama ama kikundi cha watu,ni suala la mazingira,wakati na mabadiliko ya kifalsafa.
14.Sasa tunashuhudia baadhi ya wakuu wa Wilaya na mikoa wanatatua matatizo kwa njia ambayo unabaki kujiuliza hivi hii ni sawa?
15.Lissu alipigwa Risasi mchana katikati ya makao makuu ya nchi,Mohamed Dewji alitekwa na watu wasiojulikana,kila tukisubiri kuona watuhumiwa wanasakwa,wanakamatwa na kufikishwa mahakamani tunaona siku zinaenda,au sisi wengine hatutazami mambo sawasawa?
Haya mambo hayaaa?Nawaza sana mimi.
Ila napongeza juhudi zote za ujenzi wa reli ya Kati ,tukifanikiwa masikini wengi watapata nafuu,ila ni vizuri tukafungua uwanja wa mjadala juu ya maendeleo endelevu ya taifa leo.
Nawaza tu baada ya kuutazama mjadala wa jana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ukiona kiongozi anasema tuendelee kuishi katiba yenye viraka viraka jua kabisa kuwa ana dosari kwenye kufikiri kwakeHii katiba mbovu iliyopo ndio inamfanya atawale atakavyo badala ya kuongoza, hivyo katiba mpya yenye afya kwa taifa itamuondolea ukichaa anaoufanya jambo ambalo ni ndoto kwake
Fafanua tafadhali.Una akili lakini umeamua kujitoa fahamu ili kutetea utawala dhalimu
Unapaswa kufanyiwa tohara ya akili ili upate ufahamu japo kidogo tu
Sorry mkuu nimejichanganya nilikuwa namquote Pohamba post #17Fafanua tafadhali.
[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]Tatizo ni kiongozi kichaa kuongoza wastarabu.Ilitakiwa tuandamane kupinga huhu useng_
You are rightHata wajerumani na waingereza wali jega SGR ya wakati huo, kutoka Dar mpaka Kigoma. Situngewaacha tu kama shida yetu ilikua reli. BINADAMU HAISHI KWA MKATE TUU.
Msijitoe ufahamu. Katiba mpya ni kwa ajili ya kila Mtanzania. Asiyetaka katiba mpya ni kichaa.
We ni kipofu au kiziwi?Tanzania inakatiba yake, Sidhan kama kuna nchi haina katiba. Baati nzuri tuna Rais anaye ongoza kwa kufuata katiba na hamumunyi maneno.
*Anaandika Dotto Bulendu.*
Inawezekana waliotufundisha na wale tuliosoma nao ambao wana nafasi ya kusema na kushauri wameamua kukaa kimya.
Hivi hatuoni ama tunaona wachache ama tunaoona hatuoni vizuri?
Haya mambo hayaaa?Nawaza sana mimi.
Ila napongeza juhudi zote za ujenzi wa reli ya Kati ,tukifanikiwa masikini wengi watapata nafuu,ila ni vizuri tukafungua uwanja wa mjadala juu ya maendeleo endelevu ya taifa leo.
Nawaza tu baada ya kuutazama mjadala wa jana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Sorry mkuu nimejichanganya nilikuwa namquote Pohamba post #17
Kwanini suala la katiba ulihusishe na mambo vyama vya siasa?Hahahaha Magari ya Kampuni Moja yamegongana yakigombea abiria
Pole Swahiba wangu
Lete hoja tupambane Kwa hoja Na ndio Utamaduni wetu wa JF
Sheria zipi zimevunjwa?,unaimba ka juha bitch!Haiwezekani kujiita mzalendo wakati hauthamini ungozi unajali utawala wa kikatiba, haiwezekani kujiita mzalendo wakati unaivunja katiba wazi wazi. 2020 tuna mhitaji atakaye tuahidi kutuletea katiba mpya atakaye iheshimu katiba ya nchi, uzalendo haupimwi na ujenzi wa flyover, uzalendo haupimwi kwa kuwa na ndege nyingi, hata Mobutu aliyafanya hayo Kongo .
Ndio maana hata sisi tunasema kama hautaki katiba na sisi pia hatukutaki, nchi lazima iongozwe kwa kufuata katiba na wala si kwa mapenzi tu ya mtu anavyo jisikia .
Tunamhitaji kiongozi atakaye ziheshimu sheria za nchi ajalishi awe anatokea CCM au hata upinzani, watanzania tuwaogope sana viongozi wasio penda kufuata sheria za nchi, katiba ndio sheria mama inayo ongoza nchi, katiba ni sheria ambayo wananchi wote huwa tumeziweka na kukubaliana kuwa zinafaa kutuongoza.