Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

Mwenzako anakwambia kuna mfuniko😂😂😂,
Hii argument haiendi kokote, huu muda kama una buku kumi katafute odds zako sikilizia kesho
Hana uwezo wa kufanya uchambuzi wenye mantiki juu ya mada husika kwa sababu anaonekana hana msingi mzuri wa sayansi (achilia mbali fizikia na jiografia).

Sayansi anuhali (general science) ni mgogoro tupu kwa huyo jamaa yenu.

Mbishi huyooo; lakini kusoma akaelewa, aaaghhhhgh!!!
 
Sayansi msingi wake ni kitu kinachoingia akilini baada ya utafiri na ufafanuzi.

So unapokutana na mtu hajaridhika na majibu basi ni fika kwamba majibu hayajitishelezi.
 
Sijasoma sana relativity, lakini nimemsoma Einstein na nimegundua alitumika kupotosha na kutunga nadharia ambayo itaficha ukweli.
Ukweli ni nini? Utaujuaje huu ukweli na huu uongo?
 
🤣🤣
 
Jamaa unayofikiria hayana ushirikiano 😂😂😂
Kwa hyo ulitaka gesi iwe inafungwa kwenye gazeti? 😂😂
Huyo hajui maana ya pressure. Period.

Kama unataka umweleweshe, mwanzie maana ya shinikizo au mgandamizo.

Muulize maswali ya udadisi, utagundua kitu.
 
Bro ,umeshajibiwa kuwa ni Gravity...
Gravity ina effects kulingana na uzito wa matter....Heavier the matter,the more it is affected.....
Mimi naona hii gravity ni ubabaishaji tu,inaact vipi according to weight na kwamba eti the heavier the matter the more it is affected.

Ndege kifaa inaruka juu zaidi ya ndege kiumbe.

Wakati huo ndege kifaa ni nzito kuliko ndege kiumbe.

So tulitegemea hii ndege isiweźe kuruka juu zaidi ya ndege kiumbe kwani ni nzito hivyo ingeathiriwa na gravitational force.

Kwa mantiki hiyo dhana ya kwamba grav.force inaathiri kitu kizito zaidi sio kweli,mbona imeshindwa kuathiri kifaa kizito ndege na inamuathiri binadamu ambae ni mwepesi kuliko ndege ?

Eti mkuu Bob Manson hii imekaa sawa kweli ?
 
Sayansi msingi wake ni kitu kinachoingia akilini baada ya utafiri na ufafanuzi.

So unapokutana na mtu hajaridhika na majibu basi ni fika kwamba majibu hayajitishelezi.
Ameambiwa mara tatu tatu kwamba uwepo wa mgandamizo wowote ule, sharti pawepo na kitu chenye uzito.

Na kila kitu kinachochukua nafasi, kina uzito.

Kwa vile hewa pia ina uzito, nayo ina mgandamizo.

Uwepo wa mgandamizo huu hautegemei kitu husika kiwemo kwenye chombo funge (closed container), mathalani gesi kwenye mtungi wake.

Lakini sasa yeye anadai lazima pawepo na chombo funge ili hewa iwe na shinikizo/mgandamizo.

Huoni hapo tatizo ni kukosa msingi wa somo la sayansi? Tena sayansi ya darasi la 5!
 
Dah!

Hivi ikitokea kitu kizito na chepesi vikaanguka chini, unadhani ni kipi kitakuwa na kishindo zaidi? Kwa nini?
 
Hewa ina uzito kama wewe.

Sababu inayokufanya wewe usiruke juu na kutoka nje ya uso wa dunia, ndiyo hiyo hiyo inayofanya hewa isitoke nje ya uso wa dunia.

Gravity.

Ushaelewa?
Mada ilipaswa kuishia hapa.
 
Hsya ni maelezo yasiyoingia akilini.

Mwenye kuyaamini haya maana yake ana amini sayansi,yaani maelezo hayaingii akilini inabaki kuamini tu kama tunavyoamini Dini.

Maelezo yakiwa mengi bado sio ishaara ya kwamba jambo hilo linaeleweka.

Hivyo msijikite kwenye maelezo pekee,bali mjikite kwenye maelezo yanayoeleweka na kuingia akilini.

Mnaturudisha kwemye Dini ya sayansi,yaani ni chenga tupu hakuna logic kabisa😁
 
Swali la mtoa mada linawafanya mtumie kila kanuni kutetea majibu yenu.

Mara newton,mara ozond layer,mara mzunguko wa dunia,mana gravitation.

hayo yote ni maelezo yasiyoingia akilini,labda tuyaamini kama tunavyoamini Dini,ila akilini hayaingii tunabKi kuaminishana tu.
 
Sasa ulitakiwa upinge hoja kwa hoja yenye mashiko.

Unajua ugomvi mkubwa kwenye hii mada ni kwamba upande mmoja unaeleza uhalisia wa mambo ilhali upande wa pili unapinga tu ili tu kupinga!

Sasa mmoja anasema eti gravity ni utapeli! Really?

Wakati uwepo wa kila kitu ni uthibitisho wa uyakinifu wa kani mvutano.

Pingeni kwa hoja basi!
 
Tupo kwenye birika lenye mfuniko. Hii inaleta mantiki.
 
The force that attract towards it's center
Hiyo center iko wapi ?

Mfano tu sumaku
Unawaza sahihi kabisa.

Ndio maana hapa hakuna anayekuja na jawabu moja linalomake sense.

Wote wanakuja na majibu ambayo hayo majibu yenyewe yana utata.

Mtu anasema gravitational force wakati hiyo gravitational force yenyewe kuithibitisha ni tatizo.

Mtu anasema kwa sababu eti dunia inazunguka,wakati kuthibitisha kama dunia inazunguka pia ni ishu.

So wanakuja na majibu ya kukariri darasani wakati wewe umeuliza swali linalotaka common sense kulifahamu basi waje na majibu yenye common sense kabisa yenye logic.
 
Ningekuona mwenye busara kama ungesema kwa nini unadhani hayo yaliyofafanuliwa hayaingii akili mwako.

Yaani, usikatae wala kupinga jambo fulani tu.

Eleza sababu ya kutokubaliana nalo. Ndiyo maana umepewa maelezo anuwai na mifano mbalimbali.

Huo ndio mjadala wenye tija.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…