Kama hili ni kweli, basi walimu waonesheni umuhimu wenu.

Kama hili ni kweli, basi walimu waonesheni umuhimu wenu.

mbwiganyuki

Senior Member
Joined
Nov 3, 2012
Posts
156
Reaction score
103
Kuna tetesi zimeenea ya kwamba, serekali imesema kuwa wanafunzi wote watakaofeli mtihani wa kidato cha pili mwaka huu, waruhusiwe kuingia kidato cha tatu huku wakipewa kozi maalum kwa ajili ya kurudia kufanya tena mtihani wa kidato cha pili hhhahaaa, ngoja nicheke kidogo..

Haya tuendelee, binafsi nilipozipata tetesi hizo nilighadhabika sana kwakweli, japo mimi si mtu wa kughafirika hovyo hovyo, lakini kwa hili sikuwa na budi kufanya hivyo, hasa ukizingatia namna ambavyo wale waliokahidhiwa dhamana ya kuongoza sekta hii nyeti ya elimu wanafanya ujinga ujinga.

Unajua, miezi kadhaa iliyopita wizara iliushangaza umma wa watanzania kwa kufanya marekebisho ya alama na madaraja ya ufaulu katika mitihani yote ya taifa ngazi ya sekondari na kuongeza daraja la tano na kuondoa daraja sifuri, suala lililozua mjadala nchu nzima, hata hivyo baada ya wadau kupinga uamuzi huo, kwa aibu waliotoa uamuzi huo wa ajabu wakabadilisha uamuzi huo.

Sasa muda mchache baada ya division five kulalamikiwa, leo tena tunasikia kimbwanga kungine eti wanakuja na hili la kuwavukisha darasa watu wasiokuwa na sifa hata kidogo.

Niwe muwazi tu hapa! Kiukweli hili si suala la kulifumbia macho kabisa, kwasababu ni hatari sana kufanyia mchezo suala la elimu ndugu zangu, hivi kwa mtindo kama huu tunatengeneza taifa la aina gani hasa? Lakini pia lazima tuwaulize hawa watu watuambie ni nini hasa maana ya elimu bora? pengine hawaelewi maana yake halisi, lakini pia lazima watuambie nini maana ya mtihani na lengo kuu la kuwatahini watu ni lipi? endapo mtu anafanya mtihani, anafeli, halafu tunamruhusu aendelee na ngazi ambayo hajafikia vigezo vyake tunamaanisha nini?

Unadhani kwa hali kama hii, marais wa miaka ya mbeleni watavunja mabaraza mangapi ya mawaziri kwa kuwa na watu wasio kuwa na uwezo wa kuendesha mambo ya nchi?

Kuna hatari kubwa sana hapa, maana kwa siasa na mambo ya nchi yetu yalivyokuwa ya kipuuzi hawa hawa wanaofeli leo, miaka kadhaa mbeleni watajipenyeza penyeza na hatimaye kuwa viongozi wa nchi hii hii, sasa kwa misingi na uwezo mbovu walionao unadhani watakuwa na uwezo gani hasa wa kufanya na kupanga mambo?? kama sio kufanya ujinga ujinga

Ndugu zangu walimu, sorry maofisa elimu, watu pekee wenye dhamana kubwa katika kuiokoa elimu ya nchi yetu ni ninyi wenyewe, ambao wao ni wataalamu katika kuwaandaa wanafunzi wasomi wa nchi.

Sasa kwasababu ninyi ni wasomi na wataalamu pia, ni wakati wa wenu kuionesha serekali kwamba ninyi si watu wa kawaida kawaida tuu kama wadhaniavyo wao, kwamba, wakishatoa maamuzi, basi ninyi ni watu wakutekeleza tu! Kwamba ninyi hamtakiwi kuhoji lolote lile, lakini hapana, si sahihi hata kidogo, na hapo ndipo tatizo la nchi yetu linapoanzia, dhana hii ni mbovu na inatakiwa kupingwa vikali mno, kwasababu tumejifunza kwamba watu hao tuliowapa nguvu ya kufanya maamuzi ya nchi hawana uwezo huo!

Hivyo ndugu zangu (wataalamu wa elimu) endapo tetesi hizi zitakuwa ni za ukweli, basi nawaombeni kwa nia ya dhati kabisa ya kutaka kuiokoa elimu yetu na taifa letu zuri Tanzania, mkiwa na akili zenu timamu na mkiwa mnatambua ya kuwa, jukumu la kizazi kimoja ni kuhakikisha uwepo wa kizazi kingine cha baadae chenye ustawi bora, nawaombeni muungane kwa pamoja, bila uwoga wowote, na kwa kutumia uelewa mlio nao mgome kuwafundisha wanafunzi hao watakaoingizwa kidato cha tatu kihuni huni.

Lengo si kuwakomoa hao watoto/ wadogo zetu, hapana, bali lengo ni kuwaonesha ulimwengu kuwa watoto hao hawastahili kabisa kupewa sifa hiyo kwasababu hawana sifa zinazostahili, wao binafsi pia wanalijua hilo na hawaamini kuwa ni kweli au wanaota tu!

Tena kwa pamoja na kwa sauti moja na kubwa muiambie serekali hii ya Tanzania kwamba, iache kabisa kufanya mchezo na mambo ya msingi kama elimu.

Iambieni serekali ya kwamba hampo tayari kufanywa kama wajinga
na wanasiasa, maana ninyi ni weledi (professionals) hivyo mnafanya kazi kitaalamu kwa hiyo hampo tayari kuona utaalamu wenu unadharauliwa kiurahisi namna hiyo, kwasababu maamuzi yaliyochukuliwa si ya kitaalamu kabisa hivyo hamuyaungi mkono hata kidogo.

Mkifanya hivyo,hakika nawaambieni, taaluma yenu itajijengea heshima kubwa mno na jamii ya wale wanaoelewa mambo itawathamini sana kwa maamuzi hayo ya kuiokoa elimu yetu na taifa letu.

Safari hii najua mtaweza, maana mpo wachache wale wengine wa kada ya msingi hawahusiki hapa, hawa wengi wao ni waoga sana, pengine nadhani wanakosa kile kitu wazungu wanakiita "ideological power of education" ukiwa huna hicho kitu kiukweli unakuwa utashindwa kujiamini kwa kila kitu, hivyo si kosa lao, na wala siwasemi vibaya hapa, kwani kuwa mwaga ni hulka tu.

Ndugu Walimu wa sekondari, Sasa kwasababu safari hii mpo ninyi tu, ambao wengi wenu nina amini mnayo hiyo nguvu ya elimu, sasa mtaweza kusimama pamoja na
kuiambia serekali huo ukweli mzuri ili tuokoe elimu yetu.

..... Lets go Education Officers, lets tell them the truth... Tupo pamoja..
 
mkuu kama ulikuwa kwenye kichwa changu vile nina imani nitafanya hivi kwa sababu nipo kwenye hii sekta na pia nipo kwenye hicho kidato tajwa moja kwa moja ninaamini nitasimama.amen
 
mkuu kama ulikuwa kwenye kichwa changu vile nina imani nitafanya hivi kwa sababu nipo kwenye hii sekta na pia nipo kwenye hicho kidato tajwa moja kwa moja ninaamini nitasimama.amen

Safi sana bwana mkubwa, wakipatikana vijana kama wewe hao jamaa wataacha kufanya hayo mambo ya ajabu ajabu!
 
Safi sana bwana mkubwa, wakipatikana vijana kama wewe hao jamaa wataacha kufanya hayo mambo ya ajabu ajabu!

usisubiri mtu akuletee mabadiliko unatakiwe uwemo ndani ya hayo mabadiliko unayoyataka ndo nnachofanya
 
Back
Top Bottom