Kama hufanyi kitu hiki kimoja kila siku, una utapiamlo wa akili

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Rafiki yangu mpendwa,

Hata uwe umetingwa kiasi gani, kila siku lazima utenge muda na kula chakula. Sijawahi kukutana na mtu anayesema kwa wiki nzima hajala chakula kwa sababu hajapata muda.

Huo ni upande mmoja wa kulisha mwili wako. Lakini upo upande mwingine wa kuusafisha. Kila siku lazima uusafishe mwili wako na kuuvalisha mavazi ili kuusitiri. Hujawahi kutoka nyumbani ukiwa uchi kwa sababu huna muda wa kuvaa.

Ni muhimu kwako kula kila siku na hivyo unatenga muda wa kula, hata iweje huwezi kutotenga muda huo. Ni muhimu kwako kuoga na kuvaa nguo kila siku na hivyo unatenga muda wa kufanya hivyo. Pamoja na kulalamika mambo ni mengi na muda ni mchache, hujawahi kukosa muda wa kufanya hayo muhimu kabisa kwako.

Lakini kipo kitu kimoja chenye umuhimu kwako kama hivyo viwili nilivyoshirikisha hapo juu, ila umekuwa hukipi uzito wa kutosha.
Kitu hicho ni kulisha na kusafisha akili yako.

Kama unavyoulisha mwili wako chakula, unapaswa pia kuilisha akili yako chakula. Na chakula cha akili ni usomaji wa vitabu. Kama unavyousafisha mwili wako na kuuvalisha mavazi, ndivyo pia unapaswa kuisafisha akili yako na kuivalisha. Chakula na mavazi ya akili ni usomaji wa vitabu.

Kwa maana hiyo basi, kama husomi vitabu maana yake unatembea na akili yenye utapiamlo. Kama husomi vitabu unatembea na akili chafu na iliyo uchi. Haishangazi kwa nini matatizo na changamoto mbalimbali zinakuandama.

Mwili ukikosa chakula unakuwa dhaifu na kushambuliwa na magonjwa mbalimbali. Akili ikikosa maarifa inakuwa dhaifu na kudhambuliwa na changamoto mbalimbali. Kama unataka kuwa imara, iweze kukabiliana na kila aina ya changamoto inayokuja kwako na kuishinda, basi lisha akili yako maarifa sahihi.

Abraham Lincoln amewahi kusema akipewa masaa 6 ya kukata mti, atatumia masaa manne kunoa shoka lake. Kwa sababu anajua shoka likiwa kali, kazi itakuwa rahisi. Shoka ni akili yako, inoe kupitia usomaji ili uweze kufanya vizuri kile unachofanya.

Na jenerali Jim Mattis akasema kama hujasoma mamia ya vitabu ni sawa na mtu asiyejua kusoma na kuandika, utakuwa dhaifu na changamoto zitakuangusha kwa sababu uzoefu wako mwenyewe haukutoshi kupambana kwenye haya maisha.

Mimi mwenyewe, kutoka ndani ya nafsi yangu, huwa ninaamini kabisa mtu ambaye hasomi vitabu ana mtindio wa ubongo. Haiwezekani mbele yako kuwe na njia ya uhakika kabisa ya kukusaidia kupata unachotaka halafu huitumii na ukawa na akili sahihi.

Ujumbe mkuu hapa rafiki yangu ni soma vitabu. Siri za mafanikio zimefichwa kwenye vitabu. Changamoto yoyote unayokabiliana nayo sasa majibu yake yako kwenye vitabu. Hamasa unayohitaji ili kujituma zaidi kila siku ipo kwenye vitabu.

Usikubali kuendelea na maisha ya sasa ambayo yanakuwa magumu kwako kwa sababu hujanoa shoka lako. Usikubali kuendelea kujipa sababu kwamba husomi vitabu kwa sababu huna muda wa kusoma, unao sana au huna fedha za kununua, vingi unavipata bure kabisa.

Kila siku soma angalau kurasa kumi za kitabu. Kurasa nne unapoamka, kurasa tatu unapokula mchana na kurasa tatu kabla hujalala.
Kama huwezi kusoma kurasa 10 tu za kitabu kila siku, mbegu ya mafanikio makubwa haipo ndani yako na utataabika sana na haya maisha.

Karibu upate vitabu mbalimbali vya kusoma kwa kufungua www.amkamtanzania.com/vitabu na www.t.me/somavitabutanzania

Na kama unahitaji kusimamiwa kwa karibu ili uweze kusoma vitabu na kuyatumia maarifa unayopata kuboresha maisha yako, tuwasiliane kwa wasap 0717 396 253.

Rafiki yako anayekupenda sana,

Kocha Dr Makirita Amani.
 
Andiko zuri sana, lakini nafikiri msisitizo ungekua kujifunza jambo jipya bila kujali unatumia njia gani, inaweza kuwa kupitia mazungumzo na mtu mmoja mmoja, kuhudhuria semina, warsha na kujiendeleza kwa kujiunga kwenye kozi fupi kuongeza maarifa.

Vitabu ni njia bora na rahisi lakini sio njia pekee na inaweza isiwe rahisi kwa kila mmoja wetu kwa sababu tofautitofauti.

Jambo la msingi, hakikisha unaongeza ujuzi na maarifa kila siku kadri muda unavyoruhusu.
 
Andiko zuri sana, lakini nafikiri msisitizo ungekua kujifunza jambo jipya bila kujali unatumia njia gani, inaweza kuwa kupitia mazungumzo na mtu mmoja mmoja, kuhudhuria semina, warsha na kujiendeleza kwa kujiunga kwenye kozi fupi kuongeza maarifa.

Vitabu ni njia bira na rahisi lakini sio njia pekee na inaweza isiwe rahisi kwa kila mmoja wetu kwa sababu tofautitofauti.

Asante mkuu kwa mchango huu.

Ni kweli kujifunza kitu kipya kila siku kwa njia mbalimbali ni muhimu, lakini pamoja na yote hayo, bado usomaji wa kitabu cha aina yoyote ile unapaswa kupata nafasi kila siku.

Utulivu wa akili yako wakati wa kusoma, jinsi akili yako inajenga taswira unapokuwa unasoma, inafanya ikue zaidi.

Tafiti za sayansi ya ubongo (neuroscience) zinaonesha ubongo wa watu wanaosoma vitabu una muunganiko mkubwa kwa mishipa ya fahamu kuliko wasiosoma vitabu.

Ndiyo maana hapa specifically nimesisitiza usomaji wa vitabu, haijalishi ni kitabu cha aina gani, kuna manufaa ya ziada kiakili na kiutulivu wa maisha unayapata kwa kusoma vitabu, ambayo huwezi kuyapata kwa njia nyingine za kujifunza.
 
Huyo jamaa ni mgando, huwa ana amini njia ni moja tu kwa kila jambo. Kuna watu wanafanya mambo makubwa na hawana huo utaratibu wa kujisomea kila siku wala kila wiki.

Halafu hata sababu zake za kusoma vitabu hazishawishi. Naweza nikakubaliana naye katika umuhimu wa kusoma vitabu, lakini nikapingana na sababu zake zote zinazoongelea umuhimu huo.

Unaweza ukasoma vitabu halafu uksishia kuwa msimuliaji mzuri tu (theorist/nareator) na si mtendaji.
 
Mkuu usiwe mbishi, umepewa experience nyingine. Jifunze hilo otherwise unashawishi watu waine huo usomaji wako wa vitabu ni hobby yako tu wala hausaidii kitu zaidi ya ubishi.
 
Kwa maana hiyo basi, kama husomi vitabu maana yake unatembea na akili yenye utapiamlo. Kama husomi vitabu unatembea na akili chafu na iliyo uchi.
Haishangazi kwa nini matatizo na changamoto mbalimbali zinakuandama. Mwili ukikosa chakula unakuwa dhaifu na kushambuliwa na magonjwa mbalimbali. Akili ikikosa maarifa inakuwa dhaifu na kudhambuliwa na changamoto mbalimbali.
Kumekuchaaaaaa nimeishia hapa.

Naona wenye Masters mnatuchagua matusi ya kisomi.
 
Hahahah! eti chakula cha akili ni vitabu. Sasa akili ilikua toka lini na vitabu vilianza kuandikwa lini? Au ww ndo una utapiamlo wa akili mtu'angu
 
Andiko zuri sana, lakini nafikiri msisitizo ungekua kujifunza jambo jipya bila kujali unatumia njia gani, inaweza kuwa kupitia mazungumzo na mtu mmoja mmoja, kuhudhuria semina, warsha na kujiendeleza kwa kujiunga kwenye kozi fupi kuongeza maarifa.

Vitabu ni njia bira na rahisi lakini sio njia pekee na inaweza isiwe rahisi kwa kila mmoja wetu kwa sababu tofautitofauti.

Jambo la msingi, hakikisha unaongeza ujuzi na maarifa kila siku kadri muda unavyoruhusu.
Ni kweli kabisa Mkuu
 
Asante mkuu kwa mchango huu.

Ni kweli kujifunza kitu kipya kila siku kwa njia mbalimbali ni muhimu, lakini pamoja na yote hayo, bado usomaji wa kitabu cha aina yoyote ile unapaswa kupata nafasi kila siku.

Utulivu wa akili yako wakati wa kusoma, jinsi akili yako inajenga taswira unapokuwa unasoma, inafanya ikue zaidi.

Tafiti za sayansi ya ubongo (neuroscience) zinaonesha ubongo wa watu wanaosoma vitabu una muunganiko mkubwa kwa mishipa ya fahamu kuliko wasiosoma vitabu.

Ndiyo maana hapa specifically nimesisitiza usomaji wa vitabu, haijalishi ni kitabu cha aina gani, kuna manufaa ya ziada kiakili na kiutulivu wa maisha unayapata kwa kusoma vitabu, ambayo huwezi kuyapata kwa njia nyingine za kujifunza.
Mkuu unamaanisha kitabu kwa tafsiri ya kitabu tu? Fafanua. Mathalani digital platforms nyingi, YouTube, Sportify, Insta. Twitter, Facebook, whatsapp zina jumbe mbalimbali hizi zipo katika muktadha upi wa afya ya akili. Na je, magazeti unayaweka kundi lipi.
 
Huyo jamaa ni mgando, huwa ana amini njia ni moja tu kwa kila jambo. Kuna watu wanafanya mambo makubwa na hawana huo utaratibu wa kujisomea kila siku wala kila wiki.
Halafu hata sababu zake za kusoma vitabu hazishawishi. Naweza nikakubaliana naye katika umuhimu wa kusoma vitabu, lakini nikapingana na sababu zake zote zinazoongelea umuhimu huo.
Unaweza ukasoma vitabu halafu uksishia kuwa msimuliaji mzuri tu (theorist/nareator) na si mtendaji
Mawazo yake si shuruti na yaheshimiwe, japo katika uwasilishaji wake ni kama majumuisho lazimishi yasiyohitaji mjadala bali kuchukuliwa kama yalivyo. I in particular read questions and answers on research gate than papers just in %, and this is really amazin
 
Huyo jamaa ni mgando, huwa ana amini njia ni moja tu kwa kila jambo. Kuna watu wanafanya mambo makubwa na hawana huo utaratibu wa kujisomea kila siku wala kila wiki.
Halafu hata sababu zake za kusoma vitabu hazishawishi. Naweza nikakubaliana naye katika umuhimu wa kusoma vitabu, lakini nikapingana na sababu zake zote zinazoongelea umuhimu huo.
Unaweza ukasoma vitabu halafu uksishia kuwa msimuliaji mzuri tu (theorist/nareator) na si mtendaji
Hivi huwa hamuwezagi kujenga hoja ya kupinga au kukataa kitu bila kumshambulia mtu binafsi?
 
Mkuu unamaanisha kitabu kwa tafsiri ya kitabu tu?fafanua. Mathalani digital platforms nyingi, you tube, sportfy, insta. Twitter, facebook, whatsapp zina jumbe mbalimbali hizi zipo katika muktadha upi wa afya ya akili. Na je magazeti unayaweka kundi lipi,
Ndiyo mkuu,

Namaanisha kitabu kama kitabu.

Hizo njia nyingine unaweza kujifunza mengi na yenye manufaa.

Lakini kuna manufaa ya kiakili ya kusoma vitabu ambayo huwezi kuyapata kwa njia nyingine ya kujifunza.

Magazeti nayaweka kwenye kundi la junk food kwa akili, unachokipata huko hakina manufaa kiafya kwa akili.
 
Huyo jamaa ni mgando, huwa ana amini njia ni moja tu kwa kila jambo. Kuna watu wanafanya mambo makubwa na hawana huo utaratibu wa kujisomea kila siku wala kila wiki.

Halafu hata sababu zake za kusoma vitabu hazishawishi. Naweza nikakubaliana naye katika umuhimu wa kusoma vitabu, lakini nikapingana na sababu zake zote zinazoongelea umuhimu huo.

Unaweza ukasoma vitabu halafu uksishia kuwa msimuliaji mzuri tu (theorist/nareator) na si mtendaji.
Lakini mkuu wewe umeamua kumtusi bure muandishi ,maarifa mengi yameandikwa kwenye vitabu na ndoo maana ukiprlekwa shule karika mfumo wa kawaida lazima ukute vitabu shuleni vya kujifunzia na kufundishia.

Lakini pia muandishi siku zote anasema ukiwa msomaji wa vitabu na ukaviweka kwenye matendo lazima ubadilike na ufanikiwe.Kwanini hao wazungu wanapenda kusoma vitabu? Kuna siri gani huko kwenye vitabu?

Hiyo inatuonyesha wenzetu washajua tukitaka kufanikiwa lazima tupate maarifa ya kitu fulani kupitia kwenye vitabu au kwenda shule kabisaa.Muandishi anatupa kitu kizuri tusipende kumbeza bali tupende kuwashawishi jamaa zetu na nduguzetu wapende kutafuta maarifa kutoka kwenye virabu.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Huwezi kua broke unayekimbia bili ya umeme ya elfu kumi kisha ukawa comfortable kukaa chini na kusoma kitabu.

Haitatokea kamwe.

So yeah, utapiamlo ninao
 
Kitabu kilikuwa muhimu zaidi zamani ambapo kulikuwa na njia chache za kujifunza. Sasa hivi kuna njia nyingine bora sawa au zaidi ya vitabu mojawapo ikiwa youtube tutorials.

Kwa hiyo tuseme tu kujifunza kila siku, kwa kitabu au njia nyingine.
 
Lakini wakati huo huo unapata pesa za kununua vocha na kuweka bando kwenye simu kila siku.

Wakati huo huo unapata muda wa kubishana mambo mbalimbali yasiyo na tija kwako.

Wakati huo huo unapata muda wa kufuatilia maisha ya wengine.
 
Vocha naweka.

Kubishana kuhusu mpira na facts za uoimwengu.

kufuatilia maisha ya wengine hiyo ni njia ya wanawake wanaume hatujachongewa njia hiyo.
 
Kitabu kilikuwa muhimu zaidi zamani ambapo kulikuwa na njia chache za kujifunza. Sasa hivi kuna njia nyingine bora sawa au zaidi ya vitabu mojawapo ikiwa youtube tutorials.

Kwa hiyo tuseme tu kujifunza kila siku, kwa kitabu au njia nyingine.
Magazeti na majarida mbalimbali yalipoanza kuchapwa kwenye karne ya 18, watu walisema ndiyo mwisho wa vitabu.

Redio zilipoanza karne ya 19 watu wanasema ndiyo mwisho wa vitabu.

TV zilipoanza karne ya 20 watu wanasema ndiyo mwisho wa vitabu.

Na mitandao ya kijamii ilipoanza karne ya 21 watu wanasema ni mwisho wa vitabu.

Lakini katika nyakati zote hizo, vitabu vinesurvive, teknolojia zimekuja na kupita, vitabu vimebaki.

Hiyo inaonesha kuna kitu kipo kwenye kitabu ambacho huwezi kukipata sehemu nyingine yoyote ile.

Chukua mfano wa kitabu THE ART OF WAR au TAO TE CHING, vitabu vyenye miaka zaidi ya elfu tatu halafu niambie ni channel gani

YouTube unaweza kupata Madini kama yake?

Na uzuri ni kwamba, wale wanaotoa maarifa kwenye mitandao ya kijamii, wanayachimba kutoka kwenye vitabu.

Sasa kwa kuwa wengi siyo wasomaji, wanaona ni vitu vipya sana.

Tusome vitabu, kuna hazina kubwa huko ambayo huwezi kuipata sehemu nyingine yoyote.
 
Back
Top Bottom