Kama hufanyi kitu hiki kimoja kila siku, una utapiamlo wa akili

We jamaa unaongea tu bira kufikiria hari ya mtu kiuchumi, mazingira, kifamilia.

Yaani mimi niliyeko kijiji cha Chankabhagabho, nitakipatia wapi hicho kitabu cha kusoma kila siku, pia mazingira ya huku kijijini ni yakuamka na jembe la mkono una lala na jembe, hicho kitabu hata kikipatikana utakisoma saa ngapi unalala upo hoi.

Pia majukumu ya kutafuta kuni, maji ukateke mtoni tena kilomita za ajabu na utafute chakula, huo mda wa kushika kitabu utaupata wapi.
Nakukumbusha tu life is not fare. Kama ilivyo vidole vya mkono ndivyo tusivyo lingana kimaisha
 
Hapana mkuu hapa siungani nawe!!

Hivi nikisikiliza speech kutoka kwa watu kama Oprah , Obama, Kapiga,Nnauka nk kwenye semina mbalimbali sitakuwa na manufaa ya kiakili?


Umeelezwa vizuri sana kuwa siyo njia moja tu ya kunoa akili zipo nyingi usibishe!!
 
Lakini wakati huo huo unapata pesa za kununua vocha na kuweka bando kwenye simu kila siku.
Wakati huo huo unapata muda wa kubishana mambo mbalimbali yasiyo na tija kwako.
Wakati huo huo unapata muda wa kufuatilia maisha ya wengine.
And that is life broh!!

Hebu tusi complicate maisha, yote hayo ni sehemu ya maisha na yanaumuhimu wake, binafsi kusemwa , kumsema mtu huwa sioni kama ni tatizo, mfn mie nikisikia watu wananisema regadless ni positive au negative najifunza namna wanavyo ni perceive watu,kwangu inakuwa ni faida , pia kusemwa huweza kukufanya uache tabia fulani na ubadilike ,sioni shida, watu wanunue mabando tu kwa matumizi haijalishi ya namna gani.


Umbea unaondoa stress pia, ukutanapo na wenzio mnabadilishana mawazo then siku zinaenda.
 
akili za kichadema izi ushashiba mbaa sasa unaanza andika pumba

kusoma vitabu ni anasa, mshika jembe wa Kiranjeranje huwezimwambia afanye huo ujinga
 
Acha visingizio vitabu hta online unavipata tena ni bure huitaji hta kulipia chochote zaid ya bando lako ....km umeweza kuwa na smart phone huwezi kushindwa ku download vitabu pitia hii website pdfdrive.com kuna vitabu ya 10000 vya bure.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, kama wewe ni Mkristo basi soma biblia kila siku.
Kama ni Muislam soma kuran kila siku.
Kuna ugumu gani kwenye hilo?
 
Na hayo wanayoeleza kwenye hizo speech zao nzuri wameyatoa wapi?
Jibu ni vitabuni, wameyasoma kwenye vitabu na kuweza kuyawasilisha kwa namna tofauti.
Sasa kwa nini na wewe usiende kwenye chemchem ujichotee mwenyewe badala ya kusubiri upimiwe kwa kikombe?
 
Mkuu mbona tu unataka ubishi usio na manufaa kwa yeyote,
Sijamkataza yeyote kufanya hayo.
Ninachoshangaa ni mtu anasema hana muda wa kusoma vitabu wakati ana muda wa hayo mengine.
Point yangu ni kama husomi vitabu sababu pekee ni hitaki tu, maana yale yote unayotaka unapata muda wa kuyafanya.
 
Essence ya junk food ni nini katika tafsiri ya muktadha wa chapuo la kitibu? Hivi unafahamu wabobezi wa makala?
 

Kwa mara ya kwanza
Consigliere ameteleza mkuu!
Kukutana na new friends kila mara na kusoma vitabu bora usome vitabu!
 
Essence ya junk food ni nini katika tafsiri ya muktadha wa chapuo la kitibu? Hivi unafahamu wabobezi wa makala?
Mkuu,
Soma makala upendavyo, lakini tambua vitabu vina sehemu yake na manufaa yake makubwa.
Maana hata anayeandika makala, anafanya utafiti kwa kusoma vitabu.
Huwezi kulinganisha makala yoyote ile na kitabu.
Hivyo tuweke kipaumbele kwenye usomaji wa vitabu, pamoja na kutumia hizo njia nyingine za kujifunza pia.
 
Kwa aina hii ya akili nakushauri soma hata maphlet mkuu! Pls
 
Kweli kabisa sio kusoma vitabu pekee bali ni kujifunza. Mimi kwa aiku hizi najifunza sana kupitia YouTube kuliko vitabu

Hata kutembelea watu wanaofanya vitu vipya na unavyopenda inakuongezea maarifa.

Kuna njia nyingi sana za kulisha ubongo, vitabu ni mojawapo
 
Hili swali nitakuuliza kila siku na hizi nyuzi zako, hiyo namba mwishoni umeweka ya nini?[emoji848]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
wewe ni mjinga kama wajinga wengine tu na waganga njaa wote ndio mlivyo;
hivi vitabu unavyosema watu wasome ni vitabu gani hasa?,
vya nini?,
lengo la kusoma kitabu ni nini?,
chukulia mtu anasoma vitabu vyako hivyo vitamsaidia nini?,
mbona umekua mjinga kiasi hiki?,
najua hii ni biashara ila usiaminishe watu huo ujinga wa kusoma mawazo ya watu tu eti ndio umeshibisha akili,mimi namthamini mtu atakayeenda shambani kwa mkulima kuangalia anafanya nini kupata mazao bora kuliko msoma vitabu vyako;
acha kudanganya watu;
 
I beg to differ,chakula cha ubongo sio kusoma vitabu tuu.Vitabu ni njia moja wapo yakupata maarifa ila sio pekee.Vitu kama documentaries,kuongea na watu wenye maarifa,baadhi ya miziki na filamu,hotuba nk.vyote hivi hulisha ubongo. Hata hivyo hongera kwa chapisho lako na hata machapisho yako mengine yana vitu vya kujifunza.Ubarikiwe.
 
Kweli motivational speakers are born not made,mkuu huwa huchoki,huboi wala hupoi
😂😂
Ukishajua moto unaowaka ndani yako, hakuna anayeweza kuuzima.
Ukiwa umefanya kitu kazi na kikakupa matokeo, huwezi kumwelewa anayekipinga kwamba hakifanyi kazi wakati wewe mwenyewe ni shahidi.
Ndiyo hivyo tu mkuu.
 
Binafsi nakuelewa sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…