Kama hujarithi mali pambana sana

Kama hujarithi mali pambana sana

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Umaskini unachosa sana, umaskini unadhalilisha sana, umaskini ni wa kuichukia na kuikimbia, umaskini haufai hata kidogo, kwenye maisha kuna walio bahatika kushika pesa chini ya miaka 30, lakini kwa mifumo yetu ya elimu ya kibongo.

Kama hujarithi, hutokei familia bora ni ngumu sana kuwa na maisha bora ukiwa chini ya miaka 30, maisha bora kibongo bongo, uwe na financial freedom inabidi upambane sana, tena unaweza kuyapata ukiwa kwenye 50 uko, hata nguvu za kutumia unakua umeishiwa tayari.

Wakati huo wewe unatafuta Chimbo la kula wali maharage wa 2000, wenzio wanaenda aslay mihogo kula samaki za 30,000/= tusikate tamaa kuingia miaka 30 bila kuwa na chochote cha maana, tuendelee kupiganisha kutafuta pesa, mimi na amini bora kufanya /kujaribu kuliko kutokufanya kabisa.

Lakini inauma sana umefika 40, maisha ya maana huna, majukumu ni mengi, budget hazisomi, kwenye account hakuna hata balanced ya million 5 Dah Mungu atusaidie aisee.
 
Mali za kurithi haziwezi kukufanya kutoboa endapo kichwani haupo vizuri .

Nikiangalia story za kariakoo watu waliachiwa mali sehemu zenye potential Ila leo hii hawana kitu.

Inahitajika mikakati mingi kufanikiwa na sio urithi pekee

Tulikuja DSM tunalala nje ila leo hawa wazawa walioachiwa Mali za mamilioni hawana kitu na tumewapa Ajira.
 
Kweli mkuu, ninachokiona kwa watu wengi waliofanikiwa na uvumilivu na kupamba.
 
Back
Top Bottom