Kuna dada alikua na bf wake wakati wapo chuoni. Bf akamaliza kabla yake akapata kazi Njombe wakati huyo dada yuko chuo Mbeya. Kaka hakuwahi kumpa hata 500 ya vocha na anafanya kazi. Dada wa watu akavumilia tu labda atabadilika. Dada akamaliza chuo akapata kazi Arusha. Siku akaomba ruhusa kazini ili aende akamsalimie mpenzi wake Njombe. Mpenzi wake akamuelekeza basi la kupanda kabisa akishuka stand ampigie ampokee. Anakaribia kufika yule kaka akazima simu. Amefika Njombe ikabidi atafute hotel alale. Akawa anafanya mchezo wa kumtafuta mpenzi wake kwenye simu. Mara apatikane hapokei mara hapatikani. Siku ya tatu baada ya kufika akapata namba ya dada ake yule kijana ndo kumpa ukweli wote kuwa kijana ana mwanamke na mtoto anaishi nao aondoke tu na amsahau huyo mwanaume. Akarudi zake Arusha na kilio juu maskini.
Sasa kama alikua hamtaki kwanini kampotezea muda wake na gharama za kukaa hotel wakati angemwambia tu live dada wa watu ajiongeze.