Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,949
- 24,046
Siku hizi kumezuka na Motivational Speakers wenye kuwashawishi watu kuwa kazi ni Utumwa na kamwe hutokaa utajirike.
Kwamba, mwajiri wako atakutumia anavyotaka na kamwe hutokaa utajirike.
Muda wako unakuwa kwa ajili ya kuendelea kuneemesha muajiri wako, yeye akiendelea kutajirika huku wewe ukiendelea kuwa maskini.
Kwamba leo utaamua uamke saa ngapi, uvae jinsi unavyotaka uende popote unapotaka bila yeyote kukuuliza. Au leo uamue tu kwamba siendi kazini na wala huna wa kukufanya kitu.
Ndugu yangu, kama utaingia katika ujasiriamali kwa maneno kama hayo jua umeshaanguka. Unaenda kufilisika ndani ya muda mfupi.
Ujasiriamali ni kazi ngumu ambayo kila kitu kinategemea jitihada na akili zako mwenyewe. Kwa mwajiri, una uhakika kabisa mwisho wa mwezi napokea kiasi changu. Lakini kwenye ujasiriamali, inategemea nguvu na maarifa kiasi gani ulizojitoa.
Kama kazi ya mwajiri unaona mzigo, basi nakuhakikishia wewe kinachokusumbua ni uvivu. Na kwenye ujasiriamali wavivu hufungasha virago mapema sana.
Kazi ya mwajiri inakupa muda maalum wa kuingia kazini lakini kwenye ujasiriamali unatakiwa uamke mapema zaidi kuwahi kazini. Dunia haikuogopi ujilalie mpaka saa nne ndiyo utoke uende sokoni kununua vitu vya kuuza gengeni, alafu upate faida nyingi.
Ujasiriamali unakutaka uongeze nguvu na akili zaidi kuliko ile ambayo ulikuwa ukioffer kwa mwajiri wako.
Kama nidhamu yako ilikuwa ni ndogo, basi ujasiriamali unakutaka ujiongezee nidhamu zaidi na zaidi. Kama wateja walikuwa wakifika muda wa lunch, unawabinulia mdomo kuwa ni lunch time, kwenye ujasiriamali hata mteja akija ukila basi unaacha kula umhudumie mteja.
Usikimbilie kuacha kibarua chako kwa minajili ya kufanya kile ambacho unajisikia. Utafeli ndugu yangu.
Usikimbilie kuacha kazi yako kabla biashara yako haijasimama na kuwa na uhakika wa kipato.
Usikimbilie kuacha kazi kwa sababu umechoka barua za onyo kutoka kwa mwajiri kwa tabia zako za kutofikia malengo na utovu wa nidhamu, kwenye ujasiriamali utachapika na dunia bila huruma.
Lakini ukiupatia, utafurahia dunia.
Mungu akubariki.