Kama huna dawa ya panya fanya hivi kuwakomesha panya wanaokula nyanya

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,315
Biashara na uchumi hoyeeee.
Mara nyingi sumu ya panya huweza kusababisha hatari ya watoto kuokota masalia ya chakula cha sumu ya panya usipotoa mapema.

Nyanya mara nyingi hushambuliwa na panya usiku gizani. Wakomoe panya bila dawa. Ifanye taa yako kukesha usiku mzima mahali nyanya zilipo.

Saikolojia ya panya ni kuwa haibi kitu penye mwanga unaommulika. Kwa nini?Anahisi kuwa kwa mwanga huu mwenyewe ananiona.

Hii itasaidia kwa biashara zingine za chakula kuzuia panya wasikuharibie. Asante
 
Hiyo taa inatumia umeme au nishati ipi?
 
hao panya wa kwenu lakin sio wa huku tandika na sehem zingine za uswahili
panya wana jeuri ya kuhamisha mitego na wasizurike
leo ukawaletee habari za taa!
Huku kwetu mpaka Inzi wansumbua usiku wa giza totoro
 
hao panya wa kwenu lakin sio wa huku tandika na sehem zingine za uswahili
panya wana jeuri ya kuhamisha mitego na wasizurike
leo ukawaletee habari za taa!
Huku kwetu mpaka Inzi wansumbua usiku wa giza totoro
ombeni na nyie mpelekwe mabwepande
 
hizo nyanya zisiwe za biashara...maana utakuwa umewarahisishia panya kuchagua ile minyanya mikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…