Mkurya romantic
Member
- Jul 21, 2022
- 41
- 61
Kila mmoja hupata changamoto kwenye mahusiano yake na hakuna mtu ambaye amedumu kwenye mahusiano bila migogoro ya hapa na pale.
Unatakiwa utambue kwamba mahusiano ya binadamu hasa jinsia tofauti huwa yenye migogoro inayojirudia mpaka kila mmoja akiweza kuelewa hisia za mwengine.
Kama hujipendi wala hujiheshimu lazima utateseka sana kwenye mapenzi kwa sababu utakuwa unatumia nguvu kutafuta upendo sehemu ambayo sio sahihi.
Soma hadithi hii majina sio halisi kisha angalia kama inafanana na hali yako.
Margie ni mwanamke mwenye umri wa miaka 38 ameolewa miaka 12 iliyopita. Mumewe anaitwa Mickey.
Margie anafanya kazi nzuri yenye kumpa kipato kizuri na mumewe anafanya kazi tofauti na yeye anapata kipato kizuri.
Kutokana na ushawishi wa marafiki zake Margie walimwambia kwamba hawezi kuolewa na mwanaume kama Mickey.
Walimwambia kuwa Mumewe hana sura na maumbile yenye kuvutia sio Handsome hivyo anajiabisha kutembea nae pamoja.
Hali hiyo ilikuwa inampa hasira sana Margie na kwa sababu hakuwa tayari kutengana na marafiki wala kugombana nao alianza vituko kwenye ndoa.
Mumewe ni wale wanaume wapole sana hata mke akifanya makosa mume ndio huomba msamaha ili maisha yaendelee.
Mkewe alianza kwa tabia ya kumfokea sana mumewe mara kwa mara na ikafikia hatua akamtukana sana hata mbele ya watoto na marafiki zake.
Marafiki zake Margie walimsifia sana na kumwambia wewe ni mwanamke jasiri huwezi kuendeshwa na mwanaume kama huyo ambaye kutoka nae out unaona aibu.
Margie alianza tabia ya kuchelewa sana kazini na akiulizwa maswali anakuwa mkali sana mume anaomba msamaha yanaisha.
Hakuishia hapo alisaliti ndoa yake na mume anasamehe.
Alibeba mimba ya mtu mwengine mume akasamehe maisha yaendelee.
Margie aliamini mumewe hana ujanja wa kumuacha hivyo alifanya anavyotaka na tabia hii ipo kwa wanawake wengi kama akiona huna ujanja wa kumuacha atafanya atakavyo.
Kosa kubwa la mumewe ni kuonyesha passive behavior.
Kwa maana alikuwa anaumia ila analea maumivu,anafokewa analea maumivu,mke ansaliti analea maumivu, mke anarudi muda anaotaka analea maumivu.
Bila kujua anatengeneza tatizo kubwa kwake. Hofu ya kuachwa, hofu ya watoto kukosa malezi ya wazazi, hofu ya ndugu kumsema vibaya, hofu ya kuonekana hawezi kudumu kwenye ndoa zilifanya aishi kwa kubeba chuki moyoni.
Mickey kama wanaume wengine alijikuta anapata hasira, wivu na kuanza kumfuatilia mkewe.
Alianza kugombezana na mkewe kwa vitu vidogo hilo halikuweza kusaidia chochote.
Kila mkewe alipofanya makosa na yeye kuomba msamaha ilimpa nguvu mkewe na kuzidi kufanya udhalilishaji hadharani.
Mkewe alikuwa na tabia ya kususa chakula au kuondoka na kurudi kwao kisha Mickey Huanza kupiga simu na kubembeleza sana mkewe arudi.
Hali hiyo ilizidi kumpa nguvu Margie ya kufanya atakalo bila heshima.
Kama unaishi na mtu hakuheshimu ujue unampa nguvu za kunyanyasa.
Mickey alipata kujifunza njia ya "no contact technique."
Baada ya kujifunza aliacha tabia ya kulaumu, kumfuatilia mkewe wapi ametoka ,kufoka, kutukana,kumpa vitisho au kubembeleza chochote.
Mkewe alishtuka baada ya kuona mumewe hana habari nae.
Mwanzoni Margie alikuwa akichelewa kurudi mume anafoka sana kisha kesho yake mkewe anaenda kwao kisha Mickey ndio huomba msamaha.
Mickey aligundua makosa yake na kuacha tabia ya kumfuatilia mkewe kwa lolote lile liwe zuri au baya.
Mickey aliacha kuuliza umetoka wapi wala kumpa huduma badala yake Mickey alikuwa busy na kazi zake.
Mickey alikuwa na tabia ya kupiga simu ukweni mara kwa mara kama Margie akifanya makosa lakini ndugu zake Margie hawakutoa ushirikiano.
Mickey alikuwa analalamika kwa wazazi wake wa kuzaa nao walichoka kelele zake na kumwambia mpe talaka Mickey hakuwa tayari kwa kuachana naye.
Hali hiyo ilizidi kumtesa Mickey.
Baadaye alipogundua makosa hayo aliacha kabisa kumsumbua mkewe kwa lolote.
Aliacha kulalamika,kufoka,kumpa vitisho na kusema utanikumbuka n.k.
Margie alianza kushangaa baada ya kuona Mickey hana habari nae wala haulizi chochote.
Margie aliondoka ghafla bila kuaga ili kupima upendo wa Mickey ila Mickey hajapiga simu wala kutuma sms wala kuuliza chochote.
Kitendo hicho kilimpa maumivu makali sana Margie.
Kama unataka heshima acha watu huru utaona wanakosa ile nguvu ya kuringa kwako.
Kama watu wakijua kwamba unaweza kuishi bila wao utaona wanaanza kukuheshimu.
Kama mke akiwa anaamini kwamba mumewe hawezi kuishi bila yeye huanza kuleta vituko.
Ili mke au mume aweze kukuheshimu unatakiwa kuonyesha kwamba unaweza kuwa na furaha bila yeye.
Akiacha kupokea simu kwa makusudi kuwa busy usiulize chochote ataanza kupeleleza kama unasaliti na akishindwa kupata taarifa utaona tabia yake inakuwa tofauti.
Utapendwa na kuheshimiwa kama utaamua kujipenda na kujiheshimu mwenyewe.
Kujiheshimu ni pale mtu akiwa busy unamuacha mpaka akikutafuta.
Kujiheshimu ni kuacha watu wengine huru bila kuwalazimisha kubadilika tabia.
Kujiheshimu ni kuamua kujipa furaha mwenyewe.
Kujiheshimu ni kuacha kulazimisha watu wakuelewe.
Kama ukiacha kuwalazimisha watu kubadilika wao wenyewe HUBADILIKA.
Watu hupenda vitu adimu,watu watakupenda wakiona upo na furaha sio kutaka wao wakupe furaha.
Watu watakupenda kama kuna kitu unaweza kuwapa sio wao kukupa.
Utayaona maisha ni magumu kama unataka watu wakufute machozi badala yake kuwa assets sio kuwa mzigo.
Mtu kama hakuheshimu onyesha kuwa unajiheshimu.
Kama mtu hakusikilizi acha kuongea.
Kama mtu hajali hisia zako acha kumwambia ajali hisia zako badala yake jali hisia zako mwenyewe.
Ukiweza kuonekana unaweza kuwa na furaha bila yule anaekusumbua nguvu yake kwako inaisha na utamuona anakuwa na wivu sana.