Kama huna gari wala Usihangaike kuifungua hii thread. Achana nayo, itakuumiza moyo tu

Bill Lugano

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
1,189
Reaction score
6,450
Habarini. Jana nilipita sehemu fulani nikakuta wananchi wamejazana sana wanasubiria Usafiri. Nilikuwa na BMW nikatamani niweze wasaidia lakini sikuweza kiukweli.

Nikawa nawaza mwenyewe njiani, hivi maisha bila gari inawezekana kweli? Unaendaje sehemu yoyote ile? Ni mtihani sana, mimi naboreka haraka hata kutumia gari moja siku tatu mfululizo naona kama nitalichosha.

Ndo maana na-change leo BMW, kesho Benz, mara Jeep au Range Rover. Sababu naona maisha bila kuwa na gari mbili tatu ni mateso.

Huwa nasema mtu akishindwa sana angalau awe hata na Usafiri kama Harrier, Rav 4, Suzuki au Nissan. Hizi si mbaya you can move from one place to another.

Kwa mtu ambaye anategemea usafiri wa umma. Hivi maisha yake yanakuaje? Anaweza kweli kupanga ratiba? Anaweza kuwa na furaha? Ni ngumu sana.

Dar kila kitu shida. Mvua shida, jua shida. Mimi magari yangu huwa tu kuna kipindi nafanya mazoezi ya kushusha na kupandisha vioo ili visije sahau kushuka na kupanda.

Maana toka gari nmezinunua ni full time AC. Sielewi ningeishi vipi bila gari hapa nchini. Ni ngumu sana maisha yanakuwa magumu kama jehanamu nadhani sijui huko kukoje nasikia sikia maisha ni tough sana.

Mimi nashauri kijana ukimaliza tu darasa la saba tafuta usafiri hata ya milion 20. Uwe unakusaidia kwenye mizunguko yako ili upate akili baadaye uje kununua gari lenye akili.

Unajua magari ya Ulaya mengi ni Very Intelligent haya ya Asia mengi hayana Brain. Mimi gari zangu zinanitambua kwa alama za vidole, macho n.k

Natamani watu wengi wenye magari tungekuwa na ushirika angalau tufahamiane. Mimi spares zangu nachukua huko huko Ulaya na Marekani. sijui kama kuna maduka ya spares hapa Tanzania. Hivyo kama kuna mtu ana gari models za kuanzia 2017 mpaka leo za Ulaya na Marekani tuwasiliane.

Ukishindwa nunua hata Harrier au Vanguard au Rav 4. Usibaki sana nyuma nyuma katika maendeleo.
 
Pongezi ziende kwa serikali awamu ya tano na rais magufuli kwa kufanikisha hili
 
Nahisi KidukuLilo wa kweli katekwa somewhere huyu wa siku hizi uandishi wake unapwaya. Ile ladha halisi ya KidukuLilo haipo tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…