Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
KAMA HUNA HELA UTAZINGATIWA NA WACHACHE JAPO NAO KUNA MUDA WATAKUCHOKA ILA WATAKUFICHA. USIJUE 😔
Dunia ni katili sana kwa mtu ambaye hana pesa kuna muda utaona kama mwenye pesa anapendelewa ni kweli ndivyo ilivyo Dunia.
Waliosema mwenye nacho huongezewa haikuwa nadharia bali walijionea kwa vitendo kuwa DUNIA NI KATILI KAMA HUNA PESA.
Dunia na walimwengu wake hawana muda wa kumzingatia ambaye hana pesa bali wanatafuta namna ya kukuchukulia hata kidogo ulichonacho ili kikaongeze utajiri wao.
Ukikosa pesa faraja pekee utakayobaki nayo ni ile ya imani ya kidini kuwa MBINGUNI TUTAPEWA MILI MIPYA NA KUFURAHIA MAISHA na bahati mbaya hii inabbaki kuwa nadharia tu kwani hakuna aliyerudi kutwambia kuwa MASKINI HUKO MBINGUNI WANAFURAHIA MAISHA.
Ukiona Dunia ni katili sana kwako usianze kuilaumu bali tafuta tu pesa ili uingie kwenye mfumo wake .
Ili uingie kwenye mfumo wa Dunia kigezo moja wapo ni kuwa na PESA na hapo ndipo utaona ulikosa mengi sana kipindi huna PESA.
Ukatili wa Dunia kwa maskini iwe chachu tutafute pesa na isiwe chachu ya KUKATA TAMAA NA KUJIFARIJI KWA NADHARIA ZISIZO KUWEPO.
NB: WATU HAWAKUTENGA BALI WANASUBIRI UPATE KWANZA HELA NDIO WAKUZINGATIE 😊
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#fikia Ndoto Zako