Kama huna imani na hakimu mahakama ya mwanzo, he unaruhusiwa kuhamisha kesi kwenda mahakama ya wilaya

Kama huna imani na hakimu mahakama ya mwanzo, he unaruhusiwa kuhamisha kesi kwenda mahakama ya wilaya

Naomba kueleweshwa ,
Je unaweza kwenda wapi kulalamika , ili kesi ihamishwe toka mahakama ya mwanzo kabla ya hukumu,
Karibuni.
Uzi wa Novemba 2022 na leo ni Januari 2023, ngoja nijibu hata kama mtoa mada ulimaliza suala lako, wengine unaweza kuwafaa.

Mahali pa kulalamika ni hapohapo mahakama ya mwanzo kwa hakimu huyohuyo anayesikiliza kesi, unamwambia kuwa huna imani nae kusikiliza kesi yako kwa sababu zifuatazo; ana upendeleo dhidi yako, au ana maslahi na hiyo kesi au ana urafiki au undugu na mlalamikaji/mshtaki. Utaeleza kwa kina viashiria vya hiyo sababu yako.

Hakimu anaweza kukubaliana nawe na akajitoa kwenye kesi au anaweza kukutaka ujieleze rasmi, yaani anaahirisha kesi ili pande zote mbili muweze kuieleza mahakama juu ya hilo. Akiona kuna mashiko na pia kuna mahakimu wengine wataoweza kusikiliza kesi basi atajitoa na jalada litarudi kwa hakimu mfawidhi ambaye atampangia hakimu mwingine.

Usiombe kesi iende mahakama ya wilaya kwa kuwa mahakimu wa mahakama za wilaya kwa sasa wana sifa za kitaaluma sawa na wa mahakama za mwanzo, pia kwa sasa mawakili wanaruhusiwa kuingia kuwakilisha wateja katika mahakama za mwanzo

Kwa hiyo kukiwa na mazingira ya kukosa imani na hakimu unachoomba ni kubadilishiwa hakimu na sio kuhama mahakama
 
Back
Top Bottom