Frank Mazagazaga
Member
- Sep 11, 2018
- 44
- 58
Siku moja, nilimwambia rafiki yangu ambaye ni mfugaji,
“Kama huna pesa ya kununua incubator kubwa, kwa nini usijifunze kutengeneza yako mwenyewe?”
Aliniukuza
“Unamaanisha nitengeneze mashine inayoweza kutotolesha mayai kwa mikono yangu mwenyewe?”
Nilimwambia Ndiyo. Lakini Kwa kutumia vifaa sahihi na kuelewa jinsi mfumo unavyofanya kazi.
Akili yake ilikuwa imezoea kuona incubator kama mashine ya ajabu inayotengenezwa na viwanda vikubwa tu. Hakuwahi kufikiria kwamba mtu mwenye ujuzi, vifaa sahihi na mpango mzuri angeweza kutengeneza incubator yake nyumbani.
Lakini hakujua kwamba gharama kubwa wakati mwingine haiko kwenye kutengeneza mashine, bali kwenye kutokujua vifaa gani vinahitajika na jinsi ya kuviunganisha.
Alipoanza kujifunza, aligundua kwamba incubator.
Ni mfumo unaohitaji vitu vinavyofanya kazi kwa kushirikiana.
Kwanza, kuna Temperature and humidity Controller, kama XH-W1099 au kifaa kingine kinachofaa kwa mfumo husika, ili kudhibiti joto.
Kisha kuna heater, inayozalisha joto linalohitajika.
Kuna feni, inayosaidia kusambaza joto kwa usawa ndani ya incubator.
Kuna mfumo wa udhibiti wa unyevunyevu, ambao unaweza kuhusisha humidifier au njia nyingine inayofaa kulingana na muundo wa mashine.
Na kama unataka mfumo wa kugeuza mayai kiotomatiki, kuna egg-turning motor na mfumo wake wa kuendesha tray.
Lakini vifaa hivyo pekee havitoshi.
Anahitaji pia kuelewa jinsi ya kuweka sensor mahali sahihi, kuchagua chanzo cha umeme kinachofaa, kuhakikisha hewa inazunguka vizuri na kupima mfumo kabla ya kuanza kutotolesha.
Hapo ndipo alipoanza kuelewa tofauti kutengeneza incubator inayofanya kazi kwa usahihi.
### SIRI ILIKUWA KWENYE UJUZI
Aligundua kwamba hakulazimika kuanza na mashine kubwa yenye uwezo wa kutotolesha mamia ya mayai.
Angeweza kuanza na incubator ndogo, akajifunza misingi ya mfumo, akapima joto na unyevunyevu, kisha akaboresha muundo wake kadiri ujuzi na uwezo wake vilivyoongezeka.
Na hapa ndipo watu wengi hukosea.
Incubator ya gharama nafuu haimaanishi incubator iliyotengenezwa kwa kubahatisha. Inamaanisha kutumia vifaa vinavyofaa, kupunguza gharama zisizo za lazima na kuelewa kazi ya kila kifaa.
### SWALI NI HILI…
Je, unapata shida kutengeneza incubator yako mwenyewe?
Je, unapata shida wapi utapata vifaa vya utengenezaji wa incubator?
Unaweza kuanza kwa kujifunza jinsi incubator inavyofanya kazi, kutambua vifaa sahihi na kutengeneza mashine yako, pia unaweza pata vifaa sahihi kupitia 0657 923 089
Jifunze kutengeneza incubator yako mwenyewe kwa gharama nafuu, bila kubahatisha kwenye vifaa na miunganisho ya umeme.
Kama una nia ya kuanza, anza kujifunza kazi ya kila kifaa: temperature controller, heater, feni, mfumo wa unyevunyevu na mfumo wa kugeuza mayai. Kisha jifunze jinsi ya kuviunganisha kwa usalama na kuvipima kabla ya kuweka mayai.
Kwa sababu wakati mwingine, fursa unayoitafuta dukani inaweza kuanza kwa kitu unachoweza kujifunza kutengeneza mwenyewe.