Kama hutaki Kumsaidia mtu acha lakini siyo kumsaidia na kuonesha uko nae katika Shida na Dhiki zake halafu akifanikiwa unatapa kuwa Umemuinua

Kama hutaki Kumsaidia mtu acha lakini siyo kumsaidia na kuonesha uko nae katika Shida na Dhiki zake halafu akifanikiwa unatapa kuwa Umemuinua

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mwenyezi Mungu ni SHAHIDI kama kuna Mtu ambaye nadhani kama Watu ambao tumejitoa Kuwapigania Watu wakiwa na Maisha yao ya chini na tungelipwa Fadhila zao ( hasa Pesa ) basi leo hii GENTAMYCINE ningekuwa nafukuzana na Tajiri Kibyongo wa Simba SC kwa Utajiri.

Lakini Masikini ya Mungu Mzanaki na Myao Mimi nimeumbwa tu na Furaha ya Kuwasaidia Watu ( hasa pale na Mimi pia nikiwa na huo Uwezo ) kwani hata Mimi pia kuna Nyakati nahitaji Msaada vile vile kwakuwa Maisha ya hapa duniani hayajawi kuwa na Formula kwamba Wewe kila Siku tu utakuwa nazo na Kuzikamata sana tu.

Ila kama kuna Kitu GENTAMYCINE kinaniuma na kunikwaza ni pale kuona Mtu Mwenyewe wala hakulazimishwa na Mtu kaamu Kumsaidia Mtu fulani ( iwe Ndugu au Rafiki au hata Mtu baki tu ) lakini yule Anayesaidiwa akishaanza tu kupata Mafanikio yule Mtoa Msaada anaanza Kumsengenya kwa Watu na Uswahili kibao tu.

Tuacheni Ushamba ukiamua Kumsaidia Mtu saidia na mwachie Mungu anajua jinsi ya Kukulipa kama ulisaidia kwa nia moja, ila siyo Kutegemea Fadhila ya Fedha kutoka Kwake ( Msaidiwa ) na kuanza Kumsengenya kwa Watu bila ya Wewe asingefika alipo sasa. Wewe ni Mungu? Wewe pia hukuwahi Kusaidiwa popote Maishani mwako?
 
Back
Top Bottom