Kama huyo mkeo hujamkuta bikra fukuza huyo mzinzi

wanaume wengi sio bikra ila wanataka kuoa mwamke bikra, wanaume wengi wazinzi na wachafu mno, wengi wanaacha hadi ndoa wanaenda kufanay uchafu wa kutupwa huko nje na wanataka wake zao wawe wasafi. wengi tulikuwa hivyo, Mungu ametuokoa.

Jambo kubwa la msingi kuelewa ni kwamba, vyovyote vile ulivyo, Mungu anaweza kukusafisha ukawa kiumbe kipya kabisa. kuna watu walikuwa wazinzi balaa, Mungu amewasamehe dhambi zao zote, wamekuwa wapyaa, kuna watu waliuwa mno, walikua majambazi mno, Mungu amewasamehe dhambi zote, wamekuwa kiumbe kipya. kuna watu walikuwa dhurmati, kuna watu walikuwa wafiraji na wafirwaji, walipomkimbilia Mungu amewasamehe dhambi zao zote, hata hatazikumbuka, wamekuwa viumbe vipyaaa ya kale yamepita na yamekuwa mapya. nawafahamu wanawake waliokuwa malaya mno walevi mno walanala baa wakizalilishwa na wanaume, Mungu alipowabadilisha wamekuwa viumbe vipya vyenye heshima na ya kale yamepita.

Waebrania 8:12 , kwasababu nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikumbuka tena.

Isaya 1:18 inasema, Haya njoni tusemezane asema Bwana, dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Mathayo 11:28 - 30 Yesu alisema, Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewana mizigo nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, namnyi mtapata raha nafsini mwenu, kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.

hivyo hivyo ulivyo, maadamu upo hai, jua Mungu amekupatia opportunity ya kuanza upya, yoote uliyoyatenda ukimpelekea yeye kwa kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, atakusamehe na atazitupa dhambi zako mbali kabisa hautahesabiwa hukumu tena, utakuwa kiumbe kipya kabisa. itabaki ushuhuda tu. Mungu anakupenda, anatamani umrudie hivyo hivyo ulivyo, haijalishi umefanya mambo mangapi ya ajabu, haijalishi umeua umefanya nini anasamehe, na ni nafasi amekupa, neema hiyo, wapo waliokufa kwa kutoitumia nafasi hiyo.

pia maisha yako yatabadilika, uwezo wa kushinda dhambi sisi wanadamu hatuna, tunawezeshwa na Mungu kushinda dhambi, na tunawezeshwa pale tunapokuwa tumekabidhi maisha yetu kwa Mungu, hapo ndio tunawezeshwa na dhambi tunaziona kama uchafu wa chooni, ila kama haujakabidhi maisha yako kwa Mungu kwa njia ya kuokoka kwa kupitia Yesu Kristo hata ujitahidi vipi dhambi ina nguvi itakushinda utafanya na kurudia tu, ni neema ilioje kwamba umepata nafasi kusoma huu ujumbe, ni neema iliyoje kwamba unapumua unawez akupiga magoti na kutubu dhambi wakati wengine wapo ICU hata hawajitambui, wanatamani wangepata hiyo neema uliyo nayo unachoichukulia poa tu.

amua leo kuokoka, maisha yako yatabadilika, ya kiroho na kimwili, aibu yako itafutwa, Yesu alikufa kifo cha aibu ili aibebe na aibu yako yote, atakufanya utakuwa sio yule aliyedharaulika sio yule aliyeaibika, tumeshuhudia watu wanabadilishwa maisha kabisa baada ya kuamua, wakasema sasa imetosha, nayakabidhi maisha yangu kwa Yesu yeye awe kiongozi wangu, wakabadilika na kuwa watu wakuu wa heshima na wemaweka historia katika hii dunia. masumbufu ya dunia ni mengi, hutayaweza peke yako na hata ukipata msaada wa shetani jua tu anakusogeza karibu akuchije, mwivi haji ila kuua na kuharibu ila Yesu amekuja ili tuwe na uzima tele. Mungu akubarikini.
 
WEWE MWENYEWE NI BIKRA MLETA HOJA ?
Kama jibu lako hapana basi huna haki kutoa hukumu kwa kuwa nawe kabla ni mwana wa zinaa mbele za Mungu na wanadamu kwa kufanya tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa kwa mujibu wa sheria na taratibu za madhehebu ya dini hata mpagani!
 
Mtizamo potofu..

*Kuna watu wanaoa wajane ,waliowahi kuolewa ambao ni wanawake wanaojihifadhi.

*Kuna wengine waliteleza kipindi Cha nyuma na wameamua kubadilika na kuwa wanawake wazuri wanaojiheshimu.

*Kuna wengine bikra zinatoka bila hata kuingiliwa na watu safi

*Kuna waliowahi kubakwa na watu safi .
 
sema tu unafiki wa wanadamu, ameoa bikra ameweka ndani, ila ana mchepuko nje ambaye ni malaya. thamani yake nini sasa kwake? au unawaweka wapi wanawake wajane ambao waliolewa bikra, waume zao wakafa, wanahitaji kuolewa tena, ila wana tabia nzuri, wanamcha Mungu. sio ivyo tu, wapo watu walikuwa wabaya waokoka wamebadilika kabisa wamekuwa viumbe vipya na wanamcha Mungu.
 
Nakuelewa, ko Vipi akiwa na mtoto 1??
Kwenye hilo Siwezi kusema ndio or hapana,

Ila angalia moyo wako unasemaje,angalia malengo yenu na mambo mengine yako vipi...moyo ukiona haya,uoga,hofu na mashaka kuwa na mtu mwenye mtoto/watoto ACHA MARA MOJA,
Pia kama mambo yako sawa kwenye jambo hilo bila hofu,uoga wala haya bhaas usisite kuchukua hatua ya kumuweka ndani.
 
mbona kwenye nyuz za fukuza msaliti mpo namba moja kutoa matamko, ya kwamba mzinz havumiliki vp leo mmepatwa na nini?? Mi nimetoa tu kanuni na adhabu kwa mwenye kustail hy adhabu
 
Una fikra za kijinga sana.
Yani kama una watoto wasirithi akili zako.
Cha muhimu mpate mwanamke anaejiheshimu na kujitunza .
We muoe bikra kama hajiheshimu utachapiwa tu aisee.
Nina bro wangu kaoa muarusha bikra ila asahivi wanamchapia mpaka kajuta na kuacha kaacha.
Hao viumbe hawatabiriki usije kujidanganya ukioa bikra ndio umeoa mke.
Yani mnataka mabikra ilhali mkipata wachumba mnaona mapenzi hayakamiliki mpaka muwavue chupi.
Anzeni ninyi kwanza kwa kujipiga MARUFUKU MSIDAI NYUCHI HALAFU MUONE KAMA HAMTAPATA BIKRA.
 
Nakuelewa kiasi chake, simple analyse, when person passes you a cigarette, will you smoke it or dump it🤓😆
 
Absolutely right, una oa lini shekhe gunman 🤓
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…