Kama ile Nairobi Express High way ingejengwa Dar

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Kenya Imejengwa barabara ya juu kwa juu kutoka Jomo Kenyata International Airport hadi katikati mwa Jiji, ni Barabara ya kama km 26 hivi kama sikosei na ni mwendo wa juu kwa juu.

Kinacho nishangaza sioni wala kusikia ikipewa promo na wanasiasa wala Raia wa Kenya wakiiuzungumzia kabisa hii Babara yao au kwa sababu ni ya Kulipia? Lakini mbona lile Daraja la Kigamboni lilipewa promo ya kutisha?

Hakuna Maandamano ya kupongeza wala hakuna vipindi maalumu au watu kuitwa studio wakapongeze na kusifia na kuabudu.

Hii ingejengwa hapo Dar kusingekalika kabisa, kungekuwa na Vipindi Maalumu vya kusifu na kuabudu kwenye Television station zote, Zingeisha tungwa nyimbo za kusifia. UVCCM wangeisha andaaa matembezi ya kupongeza, Bungeni sasa ndo kabisa ingekuwa ni mwendo wa kupongeza, Wale waigizaji wangeiasha andaa press confrence za kusifia.

Tanzania nashindwa kujua tunakwama wapi make sijui ni mambo ya Exposure lakini mbona waabudu wengine ni watu wana Exposure?
 
Na tuelewe kuna tofauti kubwa mno kati ya daraja na fly over!
 
Tanzania tuna ushamba mwingi kwakweli.

Kibaya zaidi hatuna ustaarabu pia, yaani hiyo barabara ya juu ingejengwa dar chini ya hizo nguzo zinazoshikilia barabara lazima ungekuta kumechafuliwa na machinga, mama ntilie,wauza mihogo, nk.

Yaani sisi Bado sana kiukweli Kenya wametuzidi kwa Mengi. Last month nilisikia Google wamefungua ofisi zao za Africa Hapo Kenya, Microsoft nao Wana ofisi zao kubwa Nairobi.

Wakenya Wana exposure sana, Tofauti na Sisi. Kitu kidogo cha kawaida ambacho ni matokeo ya usimamizi mzuri wa Kodi zetu kitasifiwa Hadi malaika washangae.

Nadhani Tatizo letu Bado ni elimu na kukosa exposure.
 
Viaduct Barabara ya juu haizidi km 8! Wacha upumbavu na hujui ukweli! Ati km 26 barabara ya juu!
 
Hujawahi kufika nairobi itakua
 
Mama angeshusha daraja toka Ubungo hadi fire,jangwani inapita juu kwa juu,na magomeni anaitawanya.
Dar pangekaa sawa!
 
Another 6,600 km of rural roads is currently under construction. The rironi mau-summit expressway scheduled to start late in the year(after the concessionaire got funding from various partners), will be the longest expressway in sub saharan africa at 181 km and it will include a 5 km elevated highway in nakuru.
Then it will be overtaken by Nairobi-Mombasa expressway(525 km), now taken by the koreans after bechtel failed to come to an agreement with GOK, but koreans have already come up with a design and financing model that they want to present to GOK on this big PPP project.
 
In total Kenya will have a 700+km long dual carriage way starting from Mombasa to Mau-summit Nakuru.
Hii battle ya barabara tumeachiwa South Africa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…