Kama inaonekana Rais Samia haongozi kwa maslahi ya Tanzania bara awamu yake ya kwanza ya uraisi, basi hali itaonekana mbaya zaidi awamu yake ya pili!

Kama inaonekana Rais Samia haongozi kwa maslahi ya Tanzania bara awamu yake ya kwanza ya uraisi, basi hali itaonekana mbaya zaidi awamu yake ya pili!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Nimetafakari sana juu ya jambo hili, katika mambo ambayo Watanzania bara wamekuwa wakimlalamikia Raisi Samia kwamba anafanya mambo fulani kama vile uraisi wake wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania ni kwa manufaa ya Zanzibar zaidi ya Tanzania kwa ujumla, au hata Tanzania bara.

Kumekuwa na suala la mikataba inayoathiri upande wa bara tu, kutokuwa makini na rasilimali za bara, uteuzi wa viongozi wa kutoka Zanzibar hasa sehemu nyeti na wizara zinazohusu bara, upendeleo wa Zanzibar kwenye nafasi za uongozi, nafasi za ajira za bara kupewa Wazanzibar , nk, mambo ambayo mara nyingi yameleta hamasa kubwa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania, kwamba Raisi wa Tanzania kimsingi ni Raisi wa Tanzania bara na anapaswa kutoka Tanzania bara ili kulinda maslahi ya Tanzania bara (Tanganyika).

Sasa najiuliza, ikiwa ni kweli haya mambo yanayolalamikiwa yapo, na yanafanyika ukizingatia kwamba Samia anahitaji kura za Watanzania bara ili aweze kuwa raisi katika awamu yake ya pili, Samia atakapofanikiwa kuwa raisi kwa awamu ya pili, hali itakuwaje?

Kumbuka, kama ni kweli haya malalamiko yana mshiko, basi akipita kuwa raisi awamu ya pili hatakuwa na simile tena, akijua baada ya miaka mitano ataondoka na hahitaji kuuma na kupuliza ili achaguliwe tena!

Nachelea tusije tukaingia katika kipindi kibaya kuliko ilivyowahi kutokea kuhusu uhusiano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa sababu tu Raisi wa Tanzania anatokea Zanzibar na kuonekana haweki mbele maslahi ya Tanzania bara na rasilimali zake!
 
Umeambiwa hii ni awamu ya magufuli ya kwake bado haijaanza, itaanza baada ya kushinda uchaguzi mkuu hapo baadaye. Awamu yake ya kwanza itaanza 2025 hadi 2030 na ya pili itaanza 2030 hadi 2035
 
Umeambiwa hii ni awamu ya magufuli ya kwake bado haijaanza, itaanza baada ya kushinda uchaguzi mkuu hapo baadaye. Awamu yake ya kwanza itaanza 2025 hadi 2030 na ya pili itaanza 2030 hadi 2035
Wanaofikiria hivyo wakasome Katiba, iko wazi sana juu ya jambo hilo, ikiainisha kwamba hii ni awamu ambayo inatambulika kisheria kuwa ni awamu ya kwanza ya uraisi wa Samia na amebakiza awamu moja tu
 
Ajabu ni kwamba viongozi wa Tanganyika wenyewe ndyo wanamsaidia kwa kumpamba kila kona.
Tatizo watu huwa wanajali maslahi yao binafsi kuliko maslahi ya nchi. Mtu anaona kwamba ikiwa mtu fulani ananitengenezea mimi kuwa tajiri, kwa nini nijali kama ni raisi wa Tanzania kutoka Kenya au hata India? Hainihusu ili mradi nafaidika na kuwepo kwake!
 
Kwa maana hiyo hakuna kiongozi wa kuaminika tena na maslahi ya watanzania yapo mikononi mwao wenyewe endapo wataamua kusimama na kutetea taifa lao.
 
Umeambiwa hii ni awamu ya magufuli ya kwake bado haijaanza, itaanza baada ya kushinda uchaguzi mkuu hapo baadaye. Awamu yake ya kwanza itaanza 2025 hadi 2030 na ya pili itaanza 2030 hadi 2035
JK Nyerere wakati anataka kung'atuka kuna kikundi cha watu walikuwa wanamshawishi asiondoke. Ila kwasababu ana akili alijua watu wale wanataka abaki kwa sababu ya maslahi yao binafsi.
 
Kwa maana hiyo hakuna kiongozi wa kuaminika tena na maslahi ya watanzania yapo mikononi mwao wenyewe endapo wataamua kusimama na kutetea taifa lao.
Wazalendo wa kweli nchini ni wachache sana, na mara nyingi huwa hawapo katika siasa.

Hivi ukiwaangalia watu kama Mwigulu, January, Rungwe, Kigwangwala, Majaliwa, Nchimbi, Kabudi, Sugu, Mbowe, nk, unaona kweli ni watu watataka kuwa maraisi wa kwa sababu wana nia ya dhati kuendeleza nchi hii?

Kwa mbali kidogo naweza kusema Biteko, Lisu, Mwinyi, Zito wanaweza kunishawishi, lakini hawa wengine hakuna kitu. Hata Gamba wa Arusha naweza kumpa the benefit of the doubt, lakini sio mtu kama Makonda!
 
Nimetafakari sana juu ya jambo hili, katika mambo ambayo Watanzania bara wamekuwa wakimlalamikia Raisi Samia kwamba anafanya mambo fulani kama vile uraisi wake wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania ni kwa manufaa ya Zanzibar zaidi ya Tanzania kwa ujumla, au hata Tanzania bara. Kumekuwa na suala la mikataba inayoathiri upande wa bara tu, kutokuwa makini na rasilimali za bara, uteuzi wa viongozi wa kutoka Zanzibar hasa sehemu nyeti na wizara zinazohusu bara, upendeleo wa Zanzibar kwenye nafasi za uongozi, nafasi za ajira za bara kupewa Wazanzibar , nk, mambo ambayo mara nyingi yameleta hamasa kubwa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania, kwamba Raisi wa Tanzania kimsingi ni Raisi wa Tanzania bara na anapaswa kutoka Tanzania bara ili kulinda maslahi ya Tanzania bara (Tanganyika).

Sasa najiuliza, ikiwa ni kweli haya mambo yanayolalamikiwa yapo, na yanafanyika ukizingatia kwamba Samia anahitaji kura za Watanzania bara ili aweze kuwa raisi katika awamu yake ya pili, Samia atakapofanikiwa kuwa raisi kwa awamu ya pili, hali itakuwaje? Kumbuka, kama ni kweli haya malalamiko yana mshiko, basi akipita kuwa raisi awamu ya pili hatakuwa na simile tena, akijua baada ya miaka mitano ataondoka na hahitaji kuuma na kupuliza ili achaguliwe tena!

Nachelea tusije tukaingia katika kipindi kibaya kuliko ilivyowahi kutokea kuhusu uhusiano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa sababu tu Raisi wa Tanzania anatokea Zanzibar na kuonekana haweki mbele maslahi ya Tanzania bara na rasilimali zake!
🤣🤣🤣acha nicheke tu
 
Hivi ukiwaangalia watu kama Mwigulu, January, Rungwe, Kigwangwala, Majaliwa, Nchimbi, Kabudi, Sugu, Mbowe, nk, unaona kweli ni watu watataka kuwa maraisi wa kwa sababu wana nia ya dhati kuendeleza nchi hii?
Hata mimi sioni🤣
 
Wanaofikiria hivyo wakasome Katiba, iko wazi sana juu ya jambo hilo, ikiainisha kwamba hii ni awamu ambayo inatambulika kisheria kuwa ni awamu ya kwanza ya uraisi wa Samia na amebakiza awamu moja tu
Ujamsikia aliye sema katiba ni kakitabu tu kakuchambia
 
Hata mimi sioni🤣
Halafu afadhali angalau hata Job Ndugai. Ila Ndugai akiwa raisi wa nchi, kama watu walimwona Magufuli dictator basi huyu ndio hafai hafai kabisa. Atawaua wapinzani wote na yeyote atakaepingana nae.

Unakumbuka kauli zake akiwa Speaker? "Naweza kukufukuza Bungeni mwaka mzima na hutanifanya kitu!"

Sasa mzalendo wa namna hiyo hafai kabisa kuwa raisi wa nchi.
 
Nyuzi za moto hizi

Unataka nitekwe? Acha nicheke tu ndugu. Unajifanya mzalendo harafu wazalendo wenzako wanatumwa ukatupwe Ununio.
Yeah, nakuelewa. Uzalendo halisi mara nyingine unahatarisha maisha ya mtu, historia siku zote imekuwa hivyo. Ukiondoka hakuna atakaeisaidia familia yako kwa sababu ulikuwa mzalendo wa kweli.
 
Halafu afadhali angalau hata Job Ndugai. Ila Ndugai akiwa raisi wa nchi, kama watu walimwona Magufuli dictaor basi huyu ndio hafai hafai kabisa. Atawaua wapinzani wote na yeyote atakaepingana nae.

Unakumbuka kauli zake akiwa Speaker? "Naweza kukufukuza Bungeni mwaka mzima na hutanifanya kitu!"

Sasa mzalendo wa namna hiyo hafai kabisa kuwa raisi wa nchi.
Nchi hii mpaka ifanyiwe Factory Reset. VIRUS kila mahali. Hakuna penye nafuu
 
Nchi hii mpaka ifanyiwe Factory Reset. VIRUS kila mahali. Hakuna penye nafuu
Kuna wakati nimewaza nikaona labda tuchukue formula ya Burkina Faso. Mtu mwenye busara pale JWTZ ashike nchi, tufute vyama vyote hivi vya siasa viliyopo ili tuanze upya, ondoa CCM, ondoa Chadema, ondoa ACT Wazalendo sijui, futilia mbali. Kisha baada ya miaka miwili turudi kwenye utawala wa kiraia tukiwa na vyama vipya.

Na tuhakikishe muundo wa vyama vipya vitakavyoundwa si kwa namna ya kubadili majina ya vyama vilivyopo. Kwa mfano, tunaweza hata kusema chama kipya hakiruhusiwi kuchukua zaidi ya 20% ya wanachama wa zamani waliokuwa nafasi za juu kama uwaziri, ubalozi, ukuu wa mikoa nk. Na tunaweza hata kusema tutakuwa na maximum ya vyama vinne tu vya siasa nchini.

Ningekuwa na uwezo ningekaa na JWTZ na kuwashauri kuwa hii ndio njia pekee ya kuinusuru nchi. Tumefikia mahali pabaya sana ndani ya sisa ya vyama kiasi kwamba vinatukwamisha kuendelea tukiwa na viongozi wazalendo halisi. Na kila siku tunakomaza jamii ya watu wanaojiona ni mabwana juu ya watwana, na hili linaingia hadi vyobo vya dola kama TISS, Polisi nk, na hata JWTZ wameanza kuambukizwa kirusi hiki kibaya.
 
Back
Top Bottom