Kama inaonekana Rais Samia haongozi kwa maslahi ya Tanzania bara awamu yake ya kwanza ya uraisi, basi hali itaonekana mbaya zaidi awamu yake ya pili!

Kama inaonekana Rais Samia haongozi kwa maslahi ya Tanzania bara awamu yake ya kwanza ya uraisi, basi hali itaonekana mbaya zaidi awamu yake ya pili!

Kuna wakati nimewaza nikaona labda tuchukue formula ya Burkina Faso. Mtu mwenye busara pale JWTZ ashike nchi, tufute vyama vyote hivi vya siasa viliyopo ili tuanze upya, ondoa CCM, ondoa Chadema, ondoa ACT Wazalendo sijui, futilia mbali. Kisha baada ya miaka miwili turudi kwenye utawala wa kiraia tukiwa na vyama vipya.

Na tuhakikishe muundo wa vyama vipya vitakavyoundwa si kwa namna ya kubadili majina ya vyama vilivyopo. Kwa mfano, tunaweza hata kusema chama kipya hakiruhusiwi kuchukua zaidi ya 20% ya wanachama wa zamani waliokuwa nafasi za juu kama uwaziri, ubalozi, ukuu wa mikoa nk. Na tunaweza hata kusema tutakuwa na maximum ya vyama vinne tu vya siasa nchini.

Ningekuwa na uwezo ningekaa na JWTZ na kuwashauri kuwa hii ndio njia pekee ya kuinusuru nchi. Tumefikia mahali pabaya sana ndani ya sisa ya vyama kiasi kwamba vinatukwamisha kuendelea tukiwa na viongozi wazalendo halisi. Na kila siku tunakomaza jamii ya watu wanaojiona ni mabwana juu ya watwana, na hili linaingia hadi vyobo vya dola kama TISS, Polisi nk, na hata JWTZ wameanza kuambukizwa kirusi hiki kibaya.
Mkuu🤣🤣
 
Umeambiwa hii ni awamu ya magufuli ya kwake bado haijaanza, itaanza baada ya kushinda uchaguzi mkuu hapo baadaye. Awamu yake ya kwanza itaanza 2025 hadi 2030 na ya pili itaanza 2030 hadi 2035
hii kama ni awamu ya Magufuli ambayo ni awamu ya 5 mbona mmeita ni awamu ya 6 ?
 
They dont care......infact It has been demonstrated that Evil makers live longer than righteoussness
They will also be judged for their terrible deeds, regardless of how long they live. How many bad leaders have there ever been? Where are they now?
 
They will also be judged for their terrible deeds, regardless of how long they live. How many bad leaders have there ever been? Where are they now?
Atleast they benefited alot on Earth, what holds in the Future so called Heaven is uncertain.
 
Ni kosa kubwa kisheria. Na haina faida kwa wananchi
Hata Traole alipopindua Burkina Faso alivunja sheria. Mandela na chama chake cha ANC walivunja sheria. Lakini huwenzi kusema kuvunja kwao sheria haikuwa kwa faida ya wananchi.

Kuna sheria inabidi zivunjwe kwa faida ya wananchi.
 
Atleast they benefited alot on Earth, what holds in the Future so called Heaven is uncertain.
Keep in mind that we are discussing crooked and malevolent politicians(leaders) what are they doing to benefit the planet?
 
Umeambiwa hii ni awamu ya magufuli ya kwake bado haijaanza, itaanza baada ya kushinda uchaguzi mkuu hapo baadaye. Awamu yake ya kwanza itaanza 2025 hadi 2030 na ya pili itaanza 2030 hadi 2035
Mbona inaitwa awamu ya sita?
 
Nimetafakari sana juu ya jambo hili, katika mambo ambayo Watanzania bara wamekuwa wakimlalamikia Raisi Samia kwamba anafanya mambo fulani kama vile uraisi wake wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania ni kwa manufaa ya Zanzibar zaidi ya Tanzania kwa ujumla, au hata Tanzania bara.

Kumekuwa na suala la mikataba inayoathiri upande wa bara tu, kutokuwa makini na rasilimali za bara, uteuzi wa viongozi wa kutoka Zanzibar hasa sehemu nyeti na wizara zinazohusu bara, upendeleo wa Zanzibar kwenye nafasi za uongozi, nafasi za ajira za bara kupewa Wazanzibar , nk, mambo ambayo mara nyingi yameleta hamasa kubwa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania, kwamba Raisi wa Tanzania kimsingi ni Raisi wa Tanzania bara na anapaswa kutoka Tanzania bara ili kulinda maslahi ya Tanzania bara (Tanganyika).

Sasa najiuliza, ikiwa ni kweli haya mambo yanayolalamikiwa yapo, na yanafanyika ukizingatia kwamba Samia anahitaji kura za Watanzania bara ili aweze kuwa raisi katika awamu yake ya pili, Samia atakapofanikiwa kuwa raisi kwa awamu ya pili, hali itakuwaje?

Kumbuka, kama ni kweli haya malalamiko yana mshiko, basi akipita kuwa raisi awamu ya pili hatakuwa na simile tena, akijua baada ya miaka mitano ataondoka na hahitaji kuuma na kupuliza ili achaguliwe tena!

Nachelea tusije tukaingia katika kipindi kibaya kuliko ilivyowahi kutokea kuhusu uhusiano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa sababu tu Raisi wa Tanzania anatokea Zanzibar na kuonekana haweki mbele maslahi ya Tanzania bara na rasilimali zake!
Inaonekana na nani?

Maslahi ya Bara ndio nini na yapi?
 
Back
Top Bottom