Nimetafakari sana juu ya jambo hili, katika mambo ambayo Watanzania bara wamekuwa wakimlalamikia Raisi Samia kwamba anafanya mambo fulani kama vile uraisi wake wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania ni kwa manufaa ya Zanzibar zaidi ya Tanzania kwa ujumla, au hata Tanzania bara.
Kumekuwa na suala la mikataba inayoathiri upande wa bara tu, kutokuwa makini na rasilimali za bara, uteuzi wa viongozi wa kutoka Zanzibar hasa sehemu nyeti na wizara zinazohusu bara, upendeleo wa Zanzibar kwenye nafasi za uongozi, nafasi za ajira za bara kupewa Wazanzibar , nk, mambo ambayo mara nyingi yameleta hamasa kubwa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania, kwamba Raisi wa Tanzania kimsingi ni Raisi wa Tanzania bara na anapaswa kutoka Tanzania bara ili kulinda maslahi ya Tanzania bara (Tanganyika).
Sasa najiuliza, ikiwa ni kweli haya mambo yanayolalamikiwa yapo, na yanafanyika ukizingatia kwamba Samia anahitaji kura za Watanzania bara ili aweze kuwa raisi katika awamu yake ya pili, Samia atakapofanikiwa kuwa raisi kwa awamu ya pili, hali itakuwaje?
Kumbuka, kama ni kweli haya malalamiko yana mshiko, basi akipita kuwa raisi awamu ya pili hatakuwa na simile tena, akijua baada ya miaka mitano ataondoka na hahitaji kuuma na kupuliza ili achaguliwe tena!
Nachelea tusije tukaingia katika kipindi kibaya kuliko ilivyowahi kutokea kuhusu uhusiano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa sababu tu Raisi wa Tanzania anatokea Zanzibar na kuonekana haweki mbele maslahi ya Tanzania bara na rasilimali zake!