OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Kwa wiki sasa nimekuwa ninasikiliza historia za viongozi madikteta Afrika. Nimesikiliza jinsi walivyoua na kunyanganya uhuru wa watu. Nimesikiliza kuhusu Samuel Doe, Iddi Amin Dada, Mobutu na madikteta wengi sana. Kwa kweli roho imeniuma sana viongozi wanaoaminika na kupewa madaraka na badala yake wanageuka na kuwa wauaji.
Mambo haya yanatajwa kutokea kwetu lakini kwa kiwango kidogo ukilinganisha na unyama walioufanya kina Mobutu. Katika kutafakari hilo nikajikuta namsikiliza kwa kina Eric Kabendera akisema kuhusu John Magufuli.
Lakini kama Jamii tunafanyaje? Je hiki kitabu tunakiacha kipite hivihivi? Tunaanzia wapi?
Taratibu zetu za kuwapata viongozi ziweje ili zipate kuchuja viongozi wa hovyo wenye kila dalili za kuvuruga nchi? Kuna vetting katika kuwapata viongozi wakubwa? Kama zipo ilikuwaje Magufuli akawa Rais pamoja na historia yake na uongozi na maisha binafsi kuwa na ukakasi?
Ipo mikakati ya Tundu Lissu na CHADEMA kuhusu vuguvugu la Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Je, ndio mahali sahihi pa kuanzia?
Natoa Hoja