Nilikutana na mhandisi kutoka Iran, amepata scholarship ya kusoma shahada ya uzamili Ulaya. Katka maongezi yetu nilimuuliza ni kwanini madaktari na wahandisi wengi wanatoka Iran, Syria Egypt nk?
Alinijibu kuwa katika jamii yao wamejengwa kufikia hapo. Yaani ukiwa na familia tangu watoto wakiwa wadogo unandaa sehemu yao ya kujisomea, wakishajua kusoma na kuandika unawaongezea maarifa kwa kuwanunulia vutabu mbali mbali. Mfano encyclopaedia.
Aliendelea kunifahamisha kuwa matokeo ya mtihani yakitoka, na wewe hukupata alama nzuri, wiki nzima hutatoka ndani. Hivyo ukijiandaa kwa mtihani unahakikisha uko vizuri kila idara. Katika familia ni lazima atoke mhandisi, daktari na mwanasheria kama mmezaliwa wengi.
Pamoja na kuwa nchi hizi uchumi wake umeyumba kutokana na matatizo ya ugaidi, lakini wana idadi kubwa ya raia walioajiriwa katika nchi za Magharibi tena kwa kazi za kitaalamu na hupeleka pesa nyumbani. Hizi husaidia hata mzunguko wa pesa.
Kazi za kitaalamu zinalipa vizuri Ulaya, kama Uhandisi, Daktari, Famasia nk. Kuna wakati Profesa Mzungu, daktari wa macho alikua anajiandaa kustaafu. Alikua anatafuta PhD student amfundishe kazi yake. Yeye alibobes katika tiba ya retinal. Alimpata kijana kutoka Syria ndiye alikidhi vigezo.
Tukiwa kama jamii tubadilike, tukimbilie walipo wenzetu. Watoto wetu wengi sasa wakiwa kidato cha pili anawaza pesa ya kwenda studio kurekodi. Tunahitaji wasanii lakini pia tuwaelekeze kuwa kuna vipaji vingi duniani.