Kama Kashfa Escrow ni "Richmond", Then, Lowassa Alionewa?, Kama Ni "EPA!" Then, Wahusika Wasionewe!

Kama Kashfa Escrow ni "Richmond", Then, Lowassa Alionewa?, Kama Ni "EPA!" Then, Wahusika Wasionewe!

Wanabodi,
Kama wizi huu ni sawa na ule wizi wa EPA, then, Watuhumiwa wa Escrow wasionewe!, kama watu walikwapua mabilioni yale ya EPA na wakasamehewa kwa kutakiwa kurudisha tuu, kwa nini na watuhumiwa wa Escrow wasitakiwa kurudisha tuu yaishe?!.

Kwa nini Bunge na Serikali yetu ifanye maamuzi tofauti kwa like scenario?!.

What a double Standard?!.
Paskali
Hili swali bado ni valid
P.
 
Wanabodi,

Azimio la Bunge kuhusu Escrow, limetolewa leo, na mjadala wa Escrow, umefungwa rasmi, wakati mjadala huu unaanza, nilisema humu, Hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za Wizi, Nawahakikishia Hakuna Atakayewajibika!. Jee leo baada ya mjadala kumalizika, vipi kuna yeyote aliyewajibika?!.

Kama kashfa ya Escrow ni kama Richmond, then je Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa alionewa?!.

Paskali

Kiukweli kabisa kwenye issue ya kashfa ya Richmond, Edward Lowassa alionewa, sasa ameondoka, kama alisamehe, then hata akiondoka kuna usalama, lakini kama hakusamehe hivyo kuondoka na kinyongo, then wahusika wakuu walio m fix Lowassa kwenye kashfa ya Richmond, wakae mguu sawa kwa kumuomba msamaha hata kifoni kabla mwili wake haujashushwa 6ft under, ili kuizuia karma ya kinyongo chake isiwatafune!.

Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Back
Top Bottom