Kama kawaida ya madaktari, huwa hawapendi kuguswa

Mimi sio daktari ila kushangilia mwenzako anapokosa ulaji ni dalili za uchawi na umaskini.
Mkuu, assume mpo kwenye project, kuna makundi 3 ambayo kila mmoja ana part yake ya kufanya, lakini uzito wa kazi ni almost the same japokuwa haufanani, umezidiana kidogo tuu.

Kwenye malipo mnapewa fungu 1 kisha ndiyo mnagawana, lakini kundi moja likajiwekea % kubwa kushinda wengine kwa sababu wao ndiyo wameshikilia mpini nyie mmeshikilia makali.

Katika situation kama hiyo hayo makundi mengine yaki-raise concerns zao watakuwa wanawafanyia uchawi hilo kundi lililojipendelea ama watakuwa wanaomba kuwe na fair distribution ya hilo fungu lililotolewa?
 
Umeongea upumbavu tu.. yaan kwa hako kamshahara unachomlipa daktar ka 1.5m ndo unaona asipigie kelele maslah kuzid pungua.. hiv ushawai enda hospital ukaona jins hao watu wanavyopiga kaz.. unadhan ni sawa na vikaz vyenu uchwara mnaenda ofisin mnakunywa chai . Lunch then kwaheri... Acha watu wapambanie maslah yao kama nyie wengne mmeridhia kuwa misukule sawa endeleen
 
Vita ya ma Dr na kada zingine za afya haijawahi kupata suluhisho
 
Natamani kuona mkeka wa posho za sekta zote za umma.
Na posho zote hizi, bado wengi wanababaisha. Dah!
 
Anyway nimejaribu kusoma replies zako nyingi naona kuna vitu sijui wewe unavijua zaidi kwa kuwa ni idara yako. Kwa namna unaandika kuna chances unaumizwa sana na hii issue, pole sana na nakuombea upate posho zaidi.

Ila nikushauri kitu kidogo tu, sehemu za kazi mara nyingi haziko fair. Huwa ziko fair kwa wateule wachache sana.

Kwa kusema hayo nakushauri utafute namna ya kupata kipato nje ya ajira yako. Tengeneza ka side hustle flani kufidia gaps za namna hii.

Fikra zangu zinanituma ulitaka kuwa daktari sema issue za cutoff zikakutoa nje ya mchezo na ukizingatia ada za vyuo vya pvt ni kubwa pole sana na ufanye kazi kwa moyo mweupe na make sure unapata pesa nje ya eneo lako la kazi.

Mfumo yetu ya ajira ni mibovu mno hata hao MDs mshahara tu wanaolipwa bado uko chini ya kiwango achilia mbali hizo posho tunazodebate hapa.

Na hii sio kwenye kada ya afya tu, ni almost kada zote kasoro kwenye siasa.

Ahsante.
 
Ingekuwa ni hivyo kusingekuwa na hiyo tofauti mkuu.. inaonekana hata mipaka yako ya kazi hujaijua vizuri, ungeijua usingekuja kulalama hapa
 
Mleta mada umeleta mada nzuri lakini umeamua kupotosha mambo kimakusudi. Ngoja tuweke pia ufafanuzi mwingine kutoka kwa wahusika wenyewe (NHIF na Jumuiya za Madaktari).

1. Consultation fee ni gharama ya kuonana na Daktari kimatibabu. Bila Daktari kukuona na kukuhudumia yeye mwenyewe NHIF haiwezi kulipa. Hivyo Daktari ndio anatumika kuingizia hospitali pesa kupitia medical consultation fee. Sio ajabu Daktari akilipwa 40% ya malipo hayo kwa kuwa bila uwepo wake na utaalamu wake kutumika basi hospitali haitaambulia hata senti tano. Kada zingine zozote kama uuguzi nazo zinapokea sehemu ya malipo hayo ya Medical consultation fee kutoka NHIF japokuwa hazihusiki moja kwa moja kutoa hiyo huduma.

2. Medical consultation ndio udaktari wenyewe, ndio kazi kuu ya Daktari na ndio jukumu kuu la madaktari wote duniani. Na hicho ndio NHIF inakilipa. Kiuhalisia kada nyingine yoyote haipaswi kulipwa hata senti tano kutokea kwenye medical consultation fee.

3. Daktari amezungukwa na kusaidiwa na watu wengine hususani kada ya uuguzi ili kufanikisha suala zima la medical consultation kiufanisi, na hivyo NHIF inatoa mgawanyo mwingine kwa kada zingine, lakini mgawanyo huo kamwe hauwezi kuwa sawa na mgawanyo mkuu wa Daktari.

4. NHIF inalipa pia gharama za huduma zingine ikiwemo vipimo vya maabara, vipimo vya radiolojia, Dawa, kulazwa, kusafishwa vidonda, upasuaji nk. Kada husika kama uuguzi, maabara, ufamasia nk. zinaweza kufaidika moja kwa moja na mapato hayo kulingana na mgawanyo waliojiwekea ndani ya hospitali husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…