Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Wanaenda kuua shirika la ndege, wanarudisha mradi wa BAGAMOYO ,wanaenda kumwaga ajira na kuongeza mishahara kupunguza machungu ili wapige vizuri mama anakazi kubwa sana
Mama anarudisha uchumi mikononi mwa watanzania, ajira, na madaraja kupanda, labda nyongeza ya mishahara na kupunguza machungu. Uchumi wa kati ubakie kwa wananchi siyo kwa nchi.
Binafsi naona ni sawa. Ili cake ya taifa tugawane hivyo siyo watu wachache tyu kufaidi peke yao.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mzee Mwanakijiji,

..nadhani makelele kuhusu ripoti ya CAG ni matokeo ya marehemu JPM kunyima wananchi nafasi ya kutoa maoni na kuikosoa serikali.
aah.. mbona maoni watu walikuwa wanatoa tu; mtu mwoga hakutoa maoni wengine walikuwa wanatoa kama kawaida. Sasa tofautisha "maoni" na "madai" (claims). Ukitoa madai ukiambiwa uthibitishe huwezi kukimbilia kusema ni maoni tu... na hasa madai ambayo yana matokeo yake... na kuna vipimo vingine. Lakini kutoa maoni na kuikosoa serikali mbona kulifanyika tu...
 

Kama akina nani waliokosoa serikali?

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 

..unasema kweli.

..utawala wa Magufuli ilikuwa unatisha, na ndio maana kuna watu, umewaita waoga, walikuwa wanaogopa kutoa maoni.

..lakini pia kama wewe ni mwanafunzi mzuri wa HISTORIA hutapata shida na haya yanayosemwa baada ya awamu mpya ya utawala kuingia madarakani.

..kila awamu mpya hapa Tz imekuwa na utaratibu wa KUZODOA serikali ya awamu iliyotangulia.

..kila awamu mpya hapa Tz hutengeneza " kundi pendwa " na " kundi adui. "
 
Are you religiously devoted to Magufuli or do you follow logic?

Kwa nini hatukusikia hasara za ATCL na habari kwamba route ya Chato haina tija kibiashara?

Kwa nini CAG hakuwa nanuhuru wa kutangaza madudu ya sehemu fulani wakati wa Magufuli?

Haya madudu yote Magufuli kafanya nini kuyamaliza? Mbona inaonekana kama kayalea as long as yalikuwa katika pet projects zake kama ATCL?
 
Mhuu umenena mzee ila anataka kutuaminisha ya kuwa hakuna upotevu wa fedha ya umma na awamu iliyopita ilikuwa safi inafikirisha mzee, ila pole mzee kwa kufiwa.
 
Kwa ufisadi uliofanya awamu ya tano uliofichwa na mfumo ni muhimu waziri mkuu PM ajitafakari maana report imeweka wazi ubadhirifu na kushindwa kusimamia maslai ya wananchi.

Mh. Majaliwa chukua hatua hatuhitaji madudu yaliyofanyika kipindi chako yajirudie tena umeahindwa kudeliver matarajio ya wananchi kwa serikali...kwa ufisadi na mambo yote uliyoyasimamia .
 
Wapigaji wamerudi kwa kasi ili mambo yao yaende kazi ni moja kuua legacy yote ya mwendazake alafu waanze kupiga kama ilivyoada
Umenena vema ...ila je watafaulu kwa mkakati huu?! Na Kama watafaulu je Watanzania watakaa kimya?!
 
Na yeye mwendazake aliona hili reasoning yetu iko chini ndiyo maana akajinasibu na mamiradi makubwa ya hasara kwa taifa, ili mradi watu wanaopenda kuona vitu, basi wamsifu na kumuabudu.
Ndiyo maana halisi ya mwendazake kuja na sentensi...nikiondoka Stigler itajengwa, reli itajengwa, ndege zitanunuliwa??
Psychological games!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Tatizo la mwendazake alifikiri nchi hii ni geto la masela akawa anaendesha nchi kama geto lake na hakutaka kuhojiwa na MTU yeyote. Nahii inathibitishwa na wateuliwa wake hawakupewa nafasi ya kusikilizwa wala kumshauri na ndio maana tunashuhudia mabadiliko kwenye nafasi nyingi za uongozi.
 
Nimesoma lakini sijaelewa unataka kufikisha ujumbe gani.
Mtoa mada anashindwa kuekeza kwamba pamoja na mazuri ya Magufuli kuna mauaji, kupoteza watu, unyang’anyi wa serikali kupitia TRA, DHULUMA za dhahiri, kutoshaurika na ubaguzi kimaendeleo, ukabila.

Na kwamba hayo yote ndiyo yame counterbalance mema ya Magufuli.
 
Upewe ulinzi haraka sana Mkuu.Mtu awaye na asiliewe hili...kwa Bwana Yule alikuwa mtukufu kwa kila kitu.
Haikuwahi na haijatokea kwa maneno yao kuwa Bwana Yule na Zaidi ya Yote.
 
Failed state, ivi unapokuwa na mashirika ambayo miaka nenda rudi yanajiendesha kihasara maana yake ni nin, lazima utafute njia za kupunguza hyo hasara kama haiwezekan ni bora kuangali njia nyingine. Cha ajabu tunatetea eti hata mashirika mengine yanapata hasara wakati tayari tunapoteza hela za watanzania ambazo zingewekezwa sehemu sahihi na kuleta matokeo chanya
 
Hongera kwa bandiko zuri, kulielewa lazima uwe na utimamu wa akili.
 
Nchi imepata hasara kubwa sana ndani ya miaka mitano ya dhalimu kuliko kipindi kingine chochote kile tangu tupate uhuru. Kaiacha kila sekta hoi bin taabani. Mwenyezi Mungu kainusuru nchi na maovu mengi sana ya kutisha.
Tuliambiwa kwamba magufuli alimaliza ufisadi.

Tuliambiwa kwamba tunajenga kwa fedha zetu wenyewe tutembee kifua mbere sisi ni matajri.

Tuliambiwa ATCL inapata faida sana mpaka wakaanza kugawa gawio serikalini.
 
Majambazi waliokubuhu hawajulikani kirahisi kwa kuwa hata Mali zao haziwi na majina yao kutuambia hana pavement nyumbani kwake ndio unamuona hakuwa mpigaji ni ujinga wako maana yote ni kiini macho nani asiyejua alihusika kuuza nyumba za serikali akiwa waziri barabara ya mwendokasi hasara kiasi gani tunaipata jagwani tuu pekee yake ndio urisi aliotuachia kwa ajili tuu ya poor design na upigaji uliofanywa chini ya wizara aliokuwa akiiongoza??? Unaongozwa na propaganda za kijinga unasahau maslahi ya nchi hiyo SGR Ilitakiwa kuisha tangu mwaka2019 na operation ianze mpaka Leo hola na bado haitaisha hata mwaka huu na sio kitu kigeni maana mkandarasi aliyepewa hiyo kazi hana historia mahali popote alipojenga reli ya aina hii yenye urefu huu na kumaliza kazi ethiopia yenyewe ameshindwa kumaliza na haya sio mageni alipigwa bungeni na akinazito kabwe na tukawaona wapinga maendeleo na tukawatukana na kuwaita pandikizi na wananchi tulikawalipa mshahara 2015 wa kuwafukuza bungeni kwa kutishiwa tukiwachagua tena hatutapata maendeleo kwenye majimbo yetu. injinia msimamizi anaendelea kulipwa na pesa za walipaka kodi kinyume na mkataba ili hali mkandarasi alitakiwa ailipe serikali kwanzia 2019 mpaka atakapomaliza kazi lkn hilo hatushughiuliki nalo unajua kwanini??? ngoja nikuibie siri wasimamizi wote ni ndugu na magufuli sukuma boy kwaanzia mkurugenzi wa shirika ndugu masanja kadogosa ambaye kitaaluma sio hata mhandisi na meneja mradi masanja machibya ambaye sijui ndio mtoto wa baba mkubwa sijui baba mdogo hapo sasa utaongea nini akati pesa inapigwa na mtoto wa mjomba kesi inamalizwa kifamilia na yeye mwenyewe alikuja kuikagua na kuendelea kumsifu mkandarasi ilihali akijua IPO nyuma ya wakati. Kunamengi sana ya kuandika ndugu zangu lkn kwa sababu ya uchungu na hasira siwezi kuendelea naomba niishie hapa na mwendazake alazwe mahali anapostahili.
 
Kwenye SGR nilitegemea CAG angesema Km 250 zilizotandikwa reli ni hewa, yaani hakuna kilichofanyika. Na kwamba pesa yote aliyolipwa Mturuki kalipwa pasipo kazi yoyote kufanyika.
Mema aliyofanya JPM kwa taifa hili hayafutiki kirahisi kama watesi wake wanavyotaka iwe. JPM kamwe hakuwa malaika kama ambavyo wewe na mimi tusivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…