Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
Unaongea opposite yake.Subiri kidogo, miradi yote tunayoiona itasimama, ndipo utajua tofauti kati ukweli na uongo. Kati ya Rais na mwimba taarabu.
Awamu zote za marais waislam nchi hii huyumba sana. Subiri tu ujionee.
Unaandika mithili ya layman. Kwani kuwa mpinzani lazima ujinasibishe na wapinzani unaowaita wamepotea?
Wewe binafsi ume compromise nafsi yako kwakua wengine wamepotea? Really?
Hivi misimamo na ideology za mtu huwa kwa wengine au wewe binafsi?
Kwahiyo huko nyuma ulifanya upinzani kwakua wengine walifanya?
Au kauli na matendo yako yanadhihirisha ulifanya mambo kwa chuki binafsi, chuki za kimaslahi, kikanda, kidini na kirangi? Seriously mtu mwenye upinzani wa Moyoni unaweza sema nilishindwa fanya upinzani maana sikumjua mpinzani wa kweli?
Seriously mtu wa kariba yako ulikuja kuwa simply brainwashed na siasa za watu aina ya akina Magufuli really?
Watu wanashangaa ATCL kupata hasara wakati waliambiwa shirika linaingiza faida.Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.
Watu wanajifanya kushangaa atcl kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara?by the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia tanesco, tpdc, ttcl, atcl, nhc, na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa atcl?
Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.
Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
Kinachoongelewa hapa ni UFISADI na wala sio kuisha au kutoisha kwa miradi.Subiri kidogo, miradi yote tunayoiona itasimama, ndipo utajua tofauti kati ukweli na uongo. Kati ya Rais na mwimba taarabu.
Awamu zote za marais waislam nchi hii huyumba sana. Subiri tu ujionee.
Nawaona chato gang mkijifariji kwa ujinga wenu. Tulikwambia uache umalaya wa kisiasa kumsupport mtu kwa sababu tu msukuma mwenzako alafu ukabisha. Kiko wapi sasa?? Magufuli alikuwa jizi na fedhuli kuliko kiongozi yeyote kuwai kutokea TanzaniaNa. M. M. Mwanakijiji
Ufisadi uliofanyika wakati wa miaka mitano ya Rais Magufuli tunaambiwa ni mkubwa sana. Kwamba, mabilioni ya fedha yameliwa na wajanja na kuwa fedha hizi zimeliwa na watu walioteuliwa na kusimamiwa na Rais Magufuli. Kwa haraka haraka - kama kawaida naona siku hizi - wakosoaji wa Rais Magufuli (na hapa nawazungumzia wale wa kisiasa) wameruka ruka kwa shangwe wakisema "si tuliwaambia!". Na kinachosikitisha kidogo ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wamejitambulisha kuwa ni wapinzani nao wamerukia kwa furaha tu na hata hawajui ni kitu gani wanaandaliwa. Sijui ni nani anayewalengesha hawa lakini kilichofanyika na kinachoandaliwa labda ni cha kutisha zaidi kuliko kilichotokea. Kuna mtu aliuliza (jamaa yangu Philemon Michael) wakati msiba ulipotangazwa maswali ambayo sidhani kama kuna mtu atakuja kuyauliza hadharani au kutaka kuyajibu yaeleweke. Na kuna mtu aliuliza tena wakati CAG amewasilisha Bungeni ripoti yake kwamba je hii ndio ile ile ripoti ambayo kama JPM angekuwa hai angekabidhiwa? Sijui jibu lake... Kama ni ile ile inawezekana hakukuwa na jinsi ripoti hii ingekutana na JPM meza moja... Kama ni nyingine... Magufuli alikuwa sahihi mara ya 1.
Hii miaka mitano tumeshuhudia miradi mikubwa ya kila namna na hata tukajisikia kuwa kuna kifu kinafanyika... lakini leo tunaambiwa lote ni changa la macho. Hizo hospitali hakuna zilizojengwa, hakuna masoko, hakuna vituo vya mabasi, hakuna shule zilizofanyiwa matengenezo makubwa, hakuna hiki wala kile na hata ndege tulizoambiwa zilinunuliwa kwa fedha taslimu kumbe hazikununuliwa... yaani, hata hii SGR na Bwawa la Umeme la Nyerere yote ni geresha tu! Kwamba kote huku watu walikuwa wanakula tu na tunachokiona hakipo na kama hili ni kweli basi Magufuli alikuwa sahihi mara 2.
Lakini kingine ni kuwa baadhi ya watu ambao waliteuliwa na Magufuli, walifanya naye kazi, na waliimba "maendeleo" "maendeleo" na hata kusifia kuwa tumeachiwa "urithi" kumbe si kweli; tumeachiwa madeni na ufisadi. Na kwa vile hakuna anayejitokeza kuwa na ujasiri wa kutetea walichokifanya kwa sababu kuna mtu anaitwa "Mwendazake" ameende na utetezi wake kumbe watu wamelia bure. Leo wengine (kina Ndugai) wanageuka wazi wazi; kumbe walikuwa wanaunga mkono uongo; walikuwa wanashangilia ulaghai, na walikuwa wanaficha ufidadi.. hapa watanyoshewa kidole wote kuanzia aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote (na wengi wamerudi au kuhamishwa) na kwa kweli inawezekana wabunge wote walioweza kuingia wakisimama nyuma ya Magufuli. Kama hili ni kweli kwamba ufisadi umetokea wakati watu wale wale ambao leo wanatufunulia ufisadi huo walikuwepo basi Magufuli alikuwa sahihi mara ya 3.
Swali kubwa ni usahihi gani ambao ninauzungumzia? Mwenye kusoma na aelewe. Kama kinachodaiwa na kushangiliwa leo ni kweli basi nchi haina kitu kingine cha kufanya bali kurudi kwenye uchaguzi mkuu mapema zaidi (labda Oktoba mwaka huu) kusafisha uchafu huu; ili wananchi wasisubiri kupigwa tena miaka mitano ijayo... Kama kina Majaliwa na wenzake wote hawakubaliani na assessment hii ya kuwa wamekuwa ni serikali ya kifisadi basi Waziri Mkuu aongoze kujiuzulu mara moja ili kumpa Rais nafasi kweli ya kuunda serikali anayoitaka ambamo ndani yake asirudi HATA MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA SERIKALI YA MAGUFULI. Ndio maana ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA.
Wakitaka kuendelea bila kuwajibika ni lazima kuna kitu kingine kinaandaliwa. Ajenda ya Magufuli haijafa, haitakufa na kwa hakina haitoachwa ife. Maana, kama ufisadi huu umefanyika kwa kiasi hiki basi inawezekana Magufuli alikuwa ni genius aliyepindukia. Yaani, kama ufisadi kama huu ungefanyika wakati wa Mkapa au JK hii nchi ingekuwa mbali sana!
Hawa wameingia kwenye great loss!! Ndio shida ya wauza maneno.Halafu Leo anasema yeye mpinzani
Juzi kasema serikali iko salama na Samia
Leo anatuambia kuna kitu kinaandaliwa..
Muuza maneno at his best
Ajenda gani?? Mshenzi wenu angekuwa msafi asingemtoa kwenye cheo chake Prof Assad. Ile ni ishara tosha hakuwa msafi na ni mchafu kuliko kiongozi yeyote kuwai tokea TanzaniaMuda utanena.....kuna ajenda na narrative inaundwa lakini haziwezi kuficha ukweli na kumbukumbu ya "urithi"
Kama mtu unaelewa unajua tu zile ni politics, hakuna namna atcl itapata faida. Hilo la kwanza.Watu wanashangaa ATCL kupata hasara wakati waliambiwa shirika linaingiza faida.
Tena linatoa hadi gawio.. Wewe ni mgeni?
Nime note kitu kimoja kutoka kwako nayo ni 'wapinzani' kumbe ulishajiweka tawi la watawala?
Ok ni haki yako lakini kwa binadamu kamili angehoji je, kwanini aliyeninasibu kuwa msafi mithili ya sufi apende kufanya mambo gizani kiasi kile?
Kweli mtu msafi ajiondoe kwenye mikataba ya uwazi?
Kwanini mtu msafi hakuitaji transparency ili umma umsaidie kuwa msafi?
Mnachofanya sasa ni nafsi zinawasuta, mmeachwa kwenye tope msijue nani atawachomoa, mli compromise nafsi zenu kwa vitu vya kipuuzi na kishenzi.
Kinachowauma zaidi mlizoea kuuza maneno sasa hakuna atakaewaamini tena.
Kwa tuliomfahamu Magufuli tangu enzi hatukua tayari kuuza nafsi zetu kwa sifa za kipuuzi na kijumla jumla namna ile.
Pole sana mtafute kazi ya kufanya sasa.MM
JIWE NI MWIZI, PERIOD! Unauaje legacy ambayo haipo?! Ni Wajinga tu ndio walikuwa wanamwamini Jiwe! Hivi kuna mwenye akili timamu asiyefahamu ukaribu wa Jiwe na Mkurugenzi wa Mayanja Constructions?! Mayanja ile ile ambayo ilipewa ujenzi wa Chato International Airport katika mazingira ambayo, ili kubana ushindani, wakaweka sharti kwamba Contractor atoke KANDA YA ZIWA TU!!! Ujenzi ulitakiwa uwe kwa 39 Billion lakini ikapanda hadi 42 Billion!Wapigaji wamerudi kwa kasi ili mambo yao yaende kazi ni moja kuua legacy yote ya mwendazake alafu waanze kupiga kama ilivyoada
ALITOKA KWA SHINIKIZO LA NDUGAI BAADA KUSEMA BUNGE NI DHAIFU NDUGAI ALIKATAA KUFANYANAE KAZI.Ajenda gani?? Mshenzi wenu angekuwa msafi asingemtoa kwenye cheo chake Prof Assad. Ile ni ishara tosha hakuwa msafi na ni mchafu kuliko kiongozi yeyote kuwai tokea Tanzania
Hivi kuna rais mdini kuliko mwendazake?Hawatakuelewa, watu wako bjze kummezea mate mlegeza macho kwa udini. Wanapiga nae pambio mnafiki namba moja wa taifa, limbukeni wa madaraka mkojoa kwa kukaa yule. Bullshit.