HTP umelia sana mkuu, na bila shaka umeumizwa sana kama wengi wengine wanavyoumizwa wanapoona mambo ya nchi yao yanakwenda shaghala baghala kila sehemu, na wanaoyasababisha mambo yawe hivyo wakijulikana na hakuna njia yoyote ya kuwawajibisha.
Wakati wote na sehemu zote ni lazima pawepo na 'Bhangusilo' mkuu, na hiyo huumiza sana inapokuwa bhangusilo hao ni matokeo ya upuuzi wa mtu mmoja tu kwa kufanya mambo yake nje ya taratibu zilizopo kwa kujisikia tu kwamba yeye anataka iwe hivyo hata kama hakuna ushahidi wowote wa matokeo yaliyokwishaonyeshwa na njia anazotaka yeye mambo yafanyike. Huyu mtu mmoja sasa ndie anayeshikilia uhai wa raia zake wote.
Hali hii ndio halisi ya taifa letu sasa, na hatutaenda popote wakati mambo yakiendelea hivi hivi.
Nikiangalia aya yako ya kwanza, unalia sana. Watu wenye elimu zao na wanaotaka kufanya mambo katika taratibu zinavyotakiwa katika maeneo yao, wanalia, hawajui wafanye nini.
Ushauri kwao wote, ni lazima, tena mhimu kabisa kufanya kazi ndani ya taratibu ya ujuzi wao walio nao na kazi zao zinavyoelekeza bila kumjali mtu mwingine yeyote toka nje, hata awe na cheo cha kumkaribia mungu au shetani.
Ukitimiza matakwa ya ujuzi wa kazi yako, hakuna sababu ya kuogopa chochote.
Tatizo la wasomi wetu sasa hapa Tanzania ni hili hili linalokuliza - njaa. Siasa imekuwa kila kitu na ndio sababu wataalam wetu mnapata taabu sana, kwa sababu mnajipendekeza kwa hao hao wanasiasa mpate fadhira na mjaze matumbo yenu, na ujuzi wenu mlioupata mnauweka pembeni
Kama si hivyo, kwa nini ulie sana namna hii mkuu wangu huku ukijua ujuzi unao, na kazi utafanya sehemu yoyote nchini au duniani?
Kwa hiyo, katika hili la kutumbuliwa kwenu, binafsi sina huruma nanyi, kwa sababu nyinyi mmekuwa sehemu ya tatizo kwa kujikomba komba kwenu ili mpate uteuzi na kusahau matakwa ya kazi zenu.
Sehemu ya pili ya mada yako.
Hapa pia wataalam hao hawawezi kujitoa moja kwa moja kwenye lawama, ingawaje sehemu yao ya lawama ni ndogo; na inawezekana pasiwepo na lawama kabisa. Nitaeleza.
Maabara yoyote ile inazo taratibu zake za kupokea sampuli, kufanya vipimo na kutoa majibu ya vipimo.
Sampuli zimeletwa toka nje ili zifanyiwe vipimo.
Kosa linaweza likatokea katika mfumo wa kukabidhiana/kupokea sambuli hizo na utambulishi wake. Sasa hapa sijui taratibu za maabara husika ni upi.
Je, kuna uwezekano wa kuvurugwa taratibu za kupokea sampuli hizo, kiasi cha kuvuruga na kupenyeza zisizohusika? Hili niliache likining'inia, kwa sababu sijui utaratibu kwenye maabara hiyo upoje. Lakini hapa ndipo panapoweza kuwa na udhaifu unaoweza kuwapa watumbuliwa lawama.
Vipimo, sioni tatizo kubwa katika eneo hili, kwa sababu aina ya vipimo vinavyofanyika hapa ni kufuata 'protocol' tu na hakuna mambo mengi ya mtu kuingiza makosa katika upimaji.
Ubora wa vipimo - hili haliwezi likawa kosa la waliotumbuliwa, kwa sababu wao hawahusiki katika kujua ubora wa vipimo hivyo.
Wahusika hapa wala sio TBS, bali wale wa madawa na vifaa vya afya.
Kwa hiyo kwa kumalizia ni kwamba, hawa waliotumbuliwa ni bhangusilo tu, uzembe upo sehemu nyingine kabisa.
Lakini siwezi kuondoka bila kulisema hili: kulikuwa na sabau gani ya kutafuta sampuli za mapapai, mbuzi, mafenesi,n.k.; vitu visivyoshabihiana kabisa na aina ya vipimo vinavyofanyika? Angalao hata wangechukua sampuli ya maji.
Usahihi zaidi, huo aliyekuwa na mashaka na ubora wa vipimo, alitakiwa achukue sampuli toka kwenye watu ambao wanajulikana hawana tatizo lolote la Coronavirus, na kuziwasilisha zipimwe. Majibu ya hizi kama ndio yangetokea na ugonjwa, ingekuwa alama sahihi ya kujua kuwa vipimo haviko sawa.
Lakini inaeleweka kwa nini ilifanyika hivi, kwa sababu tunaye mtu anayeamini kwamba yeye anajua kila kitu. Na alikuwa tayari na lengo lake akilini kwa nini ifanyike hivyo.
Mbona sampuli hizo hizo hakuziwasilisha kwenye maabara nyingine, hata nje ya nchi, ili fahamike wazi kuwa ni hizi hizi za kwake tu ndio zenye matatizo?
Waziri wa Afya na watu husika walipaswa kuwa walishajiuzuru, sio kwa tatizo hili la vipimo, bali kwa mambo mengi mengine yaliyotokea katika wizara hiyo.