Kama Kipimo kina matatizo wa kuwajibishwa ni Msimamizi wa Maabara au TBS?

Mkuu ninavyofikiria mimi hivi vifaa ni kutoka nchi za wenzetu. Ko hata hao TBS watalaumiwa bure, inawezekana ukaagiza kifaa na ukaambiwa specification yake ni kupima covid 19 kwa binadamu tu. Sasa sijui kwa akili ya kawaida kama utaanza kupima na ambavyo hujaambiwa.
 
Kwanini kila kitu nchi hii lazima wanasiasa ndo wanaumiza wataalamu..wanawapangia cha kusema wanawapingia cha kufanya....where are we heading as a nationa?
Wataalam wachache halaf hawadhaminiwi. Unafikiri watakuwa na moyo wa kufanya kazi kwa bidii kwa style hii?
Sisemi kuwa wadekezwe hapana. Panapo onekana uzembe wawajibishwe.. lakin si kwa sababu za kisiasa... ziwe za kisayansi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliagiza kivipi?
 
Labda mkuu alitaka hizo mashine zitoe majibu kuwa kilichopimwa ni papai, kondoo, mbuzi, nk.
Ilitakiwa kuangalia kama specifications zilizingatiwa wakati wa manunuzi ya mashine. Vinginevyo waliosimamishwa kazi wameonewa maana walisoma matokeo yalyoonekana kwenye mashine.
 
Unatetea usenge hadi unaboa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HTP umelia sana mkuu, na bila shaka umeumizwa sana kama wengi wengine wanavyoumizwa wanapoona mambo ya nchi yao yanakwenda shaghala baghala kila sehemu, na wanaoyasababisha mambo yawe hivyo wakijulikana na hakuna njia yoyote ya kuwawajibisha.

Wakati wote na sehemu zote ni lazima pawepo na 'Bhangusilo' mkuu, na hiyo huumiza sana inapokuwa bhangusilo hao ni matokeo ya upuuzi wa mtu mmoja tu kwa kufanya mambo yake nje ya taratibu zilizopo kwa kujisikia tu kwamba yeye anataka iwe hivyo hata kama hakuna ushahidi wowote wa matokeo yaliyokwishaonyeshwa na njia anazotaka yeye mambo yafanyike. Huyu mtu mmoja sasa ndie anayeshikilia uhai wa raia zake wote.

Hali hii ndio halisi ya taifa letu sasa, na hatutaenda popote wakati mambo yakiendelea hivi hivi.

Nikiangalia aya yako ya kwanza, unalia sana. Watu wenye elimu zao na wanaotaka kufanya mambo katika taratibu zinavyotakiwa katika maeneo yao, wanalia, hawajui wafanye nini.
Ushauri kwao wote, ni lazima, tena mhimu kabisa kufanya kazi ndani ya taratibu ya ujuzi wao walio nao na kazi zao zinavyoelekeza bila kumjali mtu mwingine yeyote toka nje, hata awe na cheo cha kumkaribia mungu au shetani.

Ukitimiza matakwa ya ujuzi wa kazi yako, hakuna sababu ya kuogopa chochote.
Tatizo la wasomi wetu sasa hapa Tanzania ni hili hili linalokuliza - njaa. Siasa imekuwa kila kitu na ndio sababu wataalam wetu mnapata taabu sana, kwa sababu mnajipendekeza kwa hao hao wanasiasa mpate fadhira na mjaze matumbo yenu, na ujuzi wenu mlioupata mnauweka pembeni

Kama si hivyo, kwa nini ulie sana namna hii mkuu wangu huku ukijua ujuzi unao, na kazi utafanya sehemu yoyote nchini au duniani?

Kwa hiyo, katika hili la kutumbuliwa kwenu, binafsi sina huruma nanyi, kwa sababu nyinyi mmekuwa sehemu ya tatizo kwa kujikomba komba kwenu ili mpate uteuzi na kusahau matakwa ya kazi zenu.

Sehemu ya pili ya mada yako.

Hapa pia wataalam hao hawawezi kujitoa moja kwa moja kwenye lawama, ingawaje sehemu yao ya lawama ni ndogo; na inawezekana pasiwepo na lawama kabisa. Nitaeleza.

Maabara yoyote ile inazo taratibu zake za kupokea sampuli, kufanya vipimo na kutoa majibu ya vipimo.
Sampuli zimeletwa toka nje ili zifanyiwe vipimo.
Kosa linaweza likatokea katika mfumo wa kukabidhiana/kupokea sambuli hizo na utambulishi wake. Sasa hapa sijui taratibu za maabara husika ni upi.
Je, kuna uwezekano wa kuvurugwa taratibu za kupokea sampuli hizo, kiasi cha kuvuruga na kupenyeza zisizohusika? Hili niliache likining'inia, kwa sababu sijui utaratibu kwenye maabara hiyo upoje. Lakini hapa ndipo panapoweza kuwa na udhaifu unaoweza kuwapa watumbuliwa lawama.

Vipimo, sioni tatizo kubwa katika eneo hili, kwa sababu aina ya vipimo vinavyofanyika hapa ni kufuata 'protocol' tu na hakuna mambo mengi ya mtu kuingiza makosa katika upimaji.

Ubora wa vipimo - hili haliwezi likawa kosa la waliotumbuliwa, kwa sababu wao hawahusiki katika kujua ubora wa vipimo hivyo.
Wahusika hapa wala sio TBS, bali wale wa madawa na vifaa vya afya.

Kwa hiyo kwa kumalizia ni kwamba, hawa waliotumbuliwa ni bhangusilo tu, uzembe upo sehemu nyingine kabisa.
Lakini siwezi kuondoka bila kulisema hili: kulikuwa na sabau gani ya kutafuta sampuli za mapapai, mbuzi, mafenesi,n.k.; vitu visivyoshabihiana kabisa na aina ya vipimo vinavyofanyika? Angalao hata wangechukua sampuli ya maji.
Usahihi zaidi, huo aliyekuwa na mashaka na ubora wa vipimo, alitakiwa achukue sampuli toka kwenye watu ambao wanajulikana hawana tatizo lolote la Coronavirus, na kuziwasilisha zipimwe. Majibu ya hizi kama ndio yangetokea na ugonjwa, ingekuwa alama sahihi ya kujua kuwa vipimo haviko sawa.

Lakini inaeleweka kwa nini ilifanyika hivi, kwa sababu tunaye mtu anayeamini kwamba yeye anajua kila kitu. Na alikuwa tayari na lengo lake akilini kwa nini ifanyike hivyo.

Mbona sampuli hizo hizo hakuziwasilisha kwenye maabara nyingine, hata nje ya nchi, ili fahamike wazi kuwa ni hizi hizi za kwake tu ndio zenye matatizo?

Waziri wa Afya na watu husika walipaswa kuwa walishajiuzuru, sio kwa tatizo hili la vipimo, bali kwa mambo mengi mengine yaliyotokea katika wizara hiyo.
 
Hii nchi ni bora uwe businessman or Businesswoman kuliko kujichanganya kwenye siasa angalia wataalamu wanavyofanywa sasa na wanasiasa its a shame, watu wabiashara tunasumbuliwa na authorities ila sio kwa kutiana aibu hivi, kulambana miguu tu
 
Hii nchi ni bora uwe businessman or Businesswoman kuliko kujichanganya kwenye siasa angalia wataalamu wanavyofanywa sasa na wanasiasa its a shame, watu wabiashara tunasumbuliwa na authorities ila sio kwa kutiana aibu hivi, kulambana miguu tu
We achatu
 
Wrong sample lazima upate unexpected results!!

Kipimo cha COVID-19 hakijatengenezwa kupima content ya sugar kwenye matunda kama papai ama fenesi hapana..

Uzuri wa sayansi huwa haidanganyi....hata hizo kits zina Technical specifications.!!

Tutajua mengi ni suala la kamda kadogo tu!!
 
Shida ipo
Kumbukeni hiki kifaa si Tz pekee kimeleta balaa
Tunamheshimu raisi ila wataalam wakitumiwa kwa nafasi zao itapendeza sana
Huyu tunayeona anaongelea vitu vya maabara leo alituambia tusitishane,tuombee taifa kwa siku 3
Tutatuma ndege Madagascar ilete dawa
Mambo mengi ya kitaalamu yeye ndo msemaji
Kulikua na haja gani ya task force ya Covid-19?

Tutaona sana mauzauza
Your browser is not able to display this video.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kukiwa na mengi nyuma ya pazia je unataka kutuambia Israeli naye anachukua watu kwa kufuata vipimo vya maabara, kwamba kipimo kikisema +ve anakutoa roho hata kama maabara imekosea. Maana kama maabara ilikuwa haitoi majibu sahihi watu wasingekuwa wanakufa kwa mpigo kama tulivyoshuhudia safari hii. Serikali yenyewe inajua kwamba watu wanaondoka kwa wingi ndio maana ikaja na wazo la kuwazika watu usiku ili isiwatie watu hofu kama inavyosisitiza. Error za maabara zipo lkn sio kwa kiasi ambacho tunaaminishwa lasivyo ununio isingepata umaarufu huo kwa muda mfupi kipindi hiki cha gonjwa la corona.
 
Huyu Mama ni mtu hatari sana...
Mungu yupo kwani yote yatapita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…