SoC04 Kama kondomu ni BURE!! kwanini isiwe kwa pedi?(taulo za kike)?

SoC04 Kama kondomu ni BURE!! kwanini isiwe kwa pedi?(taulo za kike)?

Tanzania Tuitakayo competition threads

change is inclusive

New Member
Joined
May 27, 2024
Posts
3
Reaction score
2
Nchini Tanzania, serikali inatoa kondomu bure ili kuhamasisha ngono salama na kupambana na kuenea kwa virusi vya UKIMWI. Hata hivyo, hedhi, ambayo ni hali ya kibiolojia isiyoepukika kwa wanawake na wasichana, mara nyingi haipati msaada sawa. Hii imekuwa ikiniacha nikijiuliza, ikiwa kondomu zinaweza kutolewa bure, kwa nini taulo za kike zisiweze kupatikana bure pia?

Wazo na kufikirika (conceptual framework)

Ingawa kondomu zinapatikana bure katika hospitali na maeneo mengine ya umma, taulo za kike bado zinauzwa kwa bei ambayo wengi hawawezi kumudu (sh. 2000-5000). Hii inasababisha matatizo makubwa kwa wasichana na wanawake, kwani hedhi ni sehemu ya kawaida ya maisha yao ya kila mwezi. Kwa mujibu wa takwimu, wasichana wengi hukosa shule kwa siku kadhaa kila mwezi kutokana na ukosefu wa taulo za kike, hali inayozorotesha elimu yao.

Picha; Takwimu za watoto wa kike kukosa shule.
9E21064F-D52D-44EC-A774-41219007C7CD.png

Chanzo; Danish Developement Research Network.

Hedhi ni hali ya kibiolojia ambayo haina hiari na hutokea kila mwezi kwa wasichana na wanawake. Kwa upande mwingine, ngono ni tendo la hiari. Hivyo basi, ni Muhimu kwa serikali kutoa taulo za kike bure kama inavyofanya kwa kondomu. Hatua hii haipingani na mapambano dhidi ya UKIMWI na VVU; badala yake, ni hatua ya kuhakikisha usawa na kuimarisha afya ya wanawake.

Takwimu zinaonyesha kuwa karibu asilimia 20 ya wasichana wa shule za sekondari nchini Tanzania hukosa shule kwa sababu ya ukosefu wa taulo za kike wakati wa hedhi (chanzo; unisef.org) Hii inamaanisha kuwa wanafunzi wasichana wanakosa takriban siku 45 za shule kila mwaka, hali inayowafanya wawe nyuma kimasomo ikilinganishwa na wenzao wa kiume.

Katika jamii nyingi nchini Tanzania, elimu ya afya ya uzazi na jinsia bado ni duni, hali inayosababisha matumizi yasiyo salama ya vifaa vya kujisitiri wakati wa hedhi (PIRDs – Periodic Items for Reproductive days). Wanawake na wasichana wengi Wanatumia vipande vya nguo, nyasi, au vifaa vingine visivyo safi kwa sababu ya ukosefu wa elimu na upatikanaji wa vifaa salama. Matumizi haya yasiyo salama yanaweza kusababisha maambukizi ya bakteria ambayo yanapokuwa sugu yanaweza kusababisha mabadiliko ya seli na hatimaye saratani ya shingo ya kizazi.

5413201B-482F-4885-B137-2D8AD597C7CA.jpeg

Chanzo: Océan Road cancer institute.

Uelewa duni wa afya ya uzazi na afya ya jinsia umepelekea wanawake wengi kupata saratani, hususan saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya matiti. Wanawake wengi wanaotumia njia zisizo salama kujisitiri wakati wa hedhi wanakumbana na hatari kubwa ya maambukizi ya bakteria, ambayo inaweza kusababisha mabadiliko ya kiafya na hatimaye kupelekea saratani. Kila mwaka, wanawake takriban 9,772 hugundulika na saratani ya shingo ya kizazi nchini Tanzania, na kati yao, takriban 6,695 hufariki kutokana na ugonjwa huo. Hivyo basi, elimu ya afya ya uzazi na jinsia ni muhimu sana katika kuzuia saratani na magonjwa mengine yanayohusiana na hedhi zisizo salama

Umuhimu wa Mabadiliko Kutoa taulo za kike bure ni hatua muhimu katika kuwawezesha wanawake na wasichana kuondokana na hatari za saratani.

Hii itasaidia:
• Kuongeza Mahudhurio Shuleni.

• Kuimarisha Afya ya Umma.

• Kuhakikisha Usawa wa Kijinsia.

• Kuzuia Saratani na Magonjwa Mengine.

Wito na rai ya Hatua na mpango unaotekelezeka.

Ningependa serikali izingatie hatua zifuatazo:

• Miaka 3 Ijayo: Kupunguza kabisa bei ya taulo za kike mpk kiasi cha shilingi mia tano (Tsh.500) kwa hatua zaidi kama vile ruzuku kwa wazalishaji wa ndani ili kuhakikisha upatikanaji wa bei nafuu zaidi.

• miaka 5 Ijayo : Taulo za kike zitolewe bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

• Miaka 10 Ijayo: Kutoa taulo za kike bure kwa wasichana na wanawake wote, kama inavyofanyika kwa kondomu. Hii itahakikisha kuwa wasichana hawakosi shule kwa sababu ya hedhi na wanakuwa na afya bora.

Namna ya kufika huko:

• Kuanzisha kiwanda cha Pedi(Taulo za kike) cha serikari, Tanzania pharmaceutical Industries inazalisha Dawa na kondomu ambazo zinagawiwa bure! Hivo inaweza kuanzisha kiwanda cha kuzalisha pedi pia.

• Kununua pedi( taulo za kike) kutoka viwanda vya ndani kwa bei ya jumla na kuzirasmisha ( customize) kuziweka nembo ya Taifa au alama kuonesha ni salama kwa matumizi yaani ubora.

• Kuungana na Mashirika yasio ya ki serikari na taasisi zinazosimamia Afya ya Uzazi kama Bill and Melinda gates na Ford foundation ili kupata msaada wa fedha, vifaa na machine kwaajili ya kufungua viwanda.

• Afya ya uzazi iwekwe kwenye mitaala ya Elimu kote Tanzania na isifundishwe zahanati tu, hasa kwa ngazi za sekondari Elimu iweke wazi magonjwa kama saratani, na vyanzo vyake na jinsi ya kujikinga nayo.

Katika jamii inayojali afya na elimu ya wanawake na wasichana, ni muhimu kuhakikisha kuwa wanapata vifaa vya hedhi bila gharama. Hii itaongeza ushiriki wao shuleni na kuboresha maisha yao kwa ujumla. Serikali inaweza kuchukua hatua hizi ili kuhakikisha usawa wa kijinsia na kuboresha afya ya umma. Hatua hii ni ya muhimu katika kuleta mabadiliko chanya na kuimarisha mustakabali wa wanawake na wasichana katika Tanzania.
 
Upvote 2
Hili suala linawahusu watu wa Marekani ndio wanaotoa Condom za bure na si Serikali ya watu wa Tanganyika.
Labda ongeeni na watu wa marekani kwanza
 
Back
Top Bottom